Geofrey_GAMS
JF-Expert Member
- Feb 15, 2012
- 496
- 229
Naona wasomi mnachambuana vilivyo, sisi huku kwetu hata neno "chuo" ni msamiati mgumu sana kijiji kizima. Ukiuliza msomi ni nani utaambulia kutajiwa vijana "tuliohitimu" kidato cha nne ktk shule za upili zilizoanza kujengwa kwa amri ya mzee Ngoyayi.
Wasomi wetu tangu wapate astashahada na shahada zao hawajawahi kujikomboa kutokana na utumwa wa kisiasa uliotamalaki nchini petu.
Wasomi wetu pia pamoja na tafiti zao sijawahi kusikia wameweza kutatua tatizo la umasikini, ajira na huduma za jamii kama maji, umeme na afya.
Heri yao wasomi, sina mengi ila najiuliza ni kwa nini wasomi warumbanie majina ya vyuo badala ya kupanga mipango ya kuleta maendeleo ktk familia, jamii na hata taifa kwa ujumla?
Namm ndo huwa mara zote nashangaa, umeongea point sana mkuu... Mbaya zaidi wasomi wasikuhizi akili zao zinawaza kuajiriwa tu na hii ndo sababu tatizo la umaskini linazidi kuwa kubwa