UDSM yazidi kuchanja mbuga katika nyanja za kimataifa kwa ubora wa elimu

METAL

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2013
Posts
297
Reaction score
41
kwa ripoti niliyopata kutoka kwa profesa mmoja wa UDSM ni kuwa katika ranking za vyuo bora Afrika kwa kuwa nafasi ya tatu na siyo sita kwa South Africa kuwa mbele kwa nafasi mbili zaidi za juu,na akadokeza kuwa ilitakiwa tuwe wa kwanza ila watu wanavyotumia vigezo vya kupanga ranking ni vya kishamba lakini kitaaluma tuko juu.
 
Juu ndo wapi? Mbona ndo hao hao wanatusainia mikataba feki, ndo hao hao wanaoshindwa kusimamia Wizara kama ya Uchukuzi na Madawa ya kulevya yanapita kwenye viwanja vya ndege na mpaka Twiga anachukuliwa juu kwa juu kwenda ughaibuni?

Ndugu yangu hao wasomi wanaosema mwekezaji sasa awasaidie wananchi anakofanyia kazi kwa kujenga shule, barabara, maji, vituo vya afya wakati hayo ndo yalitakiwa yawe kwenye Mikataba? Si ndo wasomi wetu hao hao wanaokubali kupeleka vijana wetu kusoma nje ya nchi wakati huku nyuma wanatoa leseni na vibali vya kuchimba madini ya urani, Gesi na makaa ya mawe bila uwepo wa sheria wala sera?

Si ndi hao hao wanaopitisha muswada wa sheria ya kulipia kodi ya line za simu afu tena wanadai watairudisha mjengoni? Kwani jamaa wa Mjengoni hawakupitia mlimani? Kwani baadhi ya Mawaziri sio Wahadhiri wa UDSM? Bwana wewe tulia tu kama mimi na wewe tunyolewe tu.

TAFAKARI!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Habari kama hizi zinanitia kichefuchefu,udsm ndio walioleta uzembe zembe kwa watanzania na kutufanya tusijue vipaumbele vya uchumi,
leo hii et shirika la bima linakufa,ndege linakufa barabara hazikpo standard yoote ni wasomi vifua mbele udsm.soo sad
 
Source please!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! kila mtu anaweza kusema atakavyo.
 
-------..UDSM hakuna kilaza kama wewe. Hata kuandika insha ya Kiswahili inakushinda!
 
duuuhh,mbona hzi stori zinazidi sana,hv kweli kiuhalisia kitakuwa kina uwezo huu kweli,mbona promotion yake ipo ktk hali ya juu sana,tumwamini yupi sasa ktk kutoa taarifa za aina hii,kila siku UD,UD,UD,UD,aaaagh
 
Hata Mkuu wa Kaya ni zao la UDSM anayesema haelewi kwanin Tz inakuwa Maskini hali tuna rasilimali za Kutosha, anadai wanafunzi wanaopata Mimba ni Viherere na nimzazi UDSM ni Janga jingine kwa Taifa!
 
Ila coet haitakuja ione ndani kwa d.i.t,,,,,,since 1957 d.i.t has been the best,,
Malengo ya kuanzishwa hivi vyuo yaani coet na dit/AIT/MIST ni tofauti kabisa mkuu, jaribu kufuatilia utaelewa nini namaanisha.
 

unawazungumziaje watu kama Mnyika, Mdee, au Zitto ambae alikua mstari wa mbele kuwaokoa watanzania na janga la Dowans! Eh, au maybe S. Sitta, Magufuri na T.Lisu hao nao wapo kwenye kundi la watu uliowasema? Cause they were all UDs students. I too hua sipendezwi na mada hizi which School is better but criticizing it on the basis of personal behaviour of people and not on the Academic basis upsets me even more!
 


kufanya ranking hakuna ubaya wowote,na ata udsm kuwa ya kwanza duniani sio mbaya,
tatioz kubwa ni pale mtu anajiita profesa anatumia nguvu nyingi kumuaminisha mwanafunzi wake kuwa udsm ni bora(mambo ya kufikirika) wakati ata yeye mwenyewe (profesa) anajua kamwe udsm haiwezi kufikia vyuo vya afrika kusin,makarere,nairobi universt,vyuo vya misri,vyuo baadhi ya vyuo vya algeria.
na kibaya zaidi unakuta uyu profesa anatumia muda mwingi na nguvu nyingi kushindana (kwa porojo) na chuo kichanga kama udom amabacho bado kinakuwa.
majigambo yote unayoyaaona humu ni sumu wanaolishwa wanafunzi wa udsm na maprofesa wao wakati wa lecture.
ni bora hawa maprofesa watumie mda wao mwingi kufanya mambo yenye manufaa kwa nchi hii.

yote kwa yote udsm tunaijua ipo apa apatz,watz tunajua,wanaofundisha tunawajua,wanafunzi waketunawajua,mazuri yake tunayajua na mapungufu yake pia tunayajua.
udsm bado ni chuo bora kwa tz tu(may be kwa ranking) na sivinginevyo,na wala hatuta shangaaa kikipitwa vvyuo vipya kama udom miaka michache ijayo
 
jamani mnanikumbusha tulivyoingia chuo kipindi kile mara oh UDSM IS THE PLACE TO BE, MABIBO HOSTEL IS HALF LONDON,MARA OH UKIWA UD FULL SAKAFU HADI CHUMBANI,ila ukweli ni kwamba UD ina miundo mbinu mbovu sana vyoo vinakosa maji ata wiki kuna kipindi madent wanatoka main campus wanaenda kuoga mabibo hostel and vice versa, lecture room aziendani na idadi ya wanafunzi,chakula kibovu sana,usalama wa wanafunzi na mali zao ni finyu kwa leo naishia hapa yapo mengi nyuma ya chuo changu pendwa.
 
Udsm aiingii kwa mzumbe sembuse vyuo vya africa khaa
 

mh!? Ila kweli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…