UEFA Champions League: Atletico Madrid Vs Real Madrid

Jamani labda sioni vizuri, hivi nani kamuona Torres akigusa mpira????

BACK TANGANYIKA
 
Griezmann ndie wa nyota Athletico Madrid maana ndie pekee aliejaribu mashuti mawili on target.
 
Ni mapumziko na Real Madrid wanastahiki kuwa mbele kwa goli 1.

Wanacheza kwa nidhamu ya hali ya juu, wanajipanga vizuri na wanashambulia inapobidi, hii ndiyo timu ya Zizou.

Diego Simeone inabidi arudi kwenye ubao wa michoro kupanga timu yake upya.

Tunazidi kujifunza ubora wa hawa mameneja wawili ambao ni miongoni mwa the best managers.
 
Real wameshawalizimisha atletico kucheza game yao ....mpira umeisha huu
 
Madrid wamepaki bus ila kipindi cha pili lazima aachie

Hapana mkuu, huu mtindo ndio unapendwa sana siku hizi na timu nyingi zenye kuhofia timu pinzani ambazo hucheza kwa kasi kama Athletico Madrid, hutumia mbinu hiyo.

Lakini sio kupaki basi, mbinu ambayo mnajipanga na mnaishia katikati ya uwanja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…