UEFA Champions League kwenye Visimbuzi vya Dstv na Canal+

Star times ndio king'amuzi bora naangalia europa mechi za kimataifa ulaya fiba bundesliga frenc ligi na mengine mengi dstv nitaenda kibanda umiza kwenye mechi muhimu basi
 
Dawa ya dstv hapa Tanzania ni serikali iruhusu soko huria. Wawape ruhusa Canal na bein sport wafanye kazi kisheria. Hapo wenyewe watashusha bei. Haiwezekani Nigeria walipe elfu 50 za kibongo kifirushi cha premium
 
Mkuu DStv wanalipa Hela ndefu kuonyesha hio mipira na cost inabidi tulipe sisi wateja wa DStv.

Hela wanayolipa Ni fixed hivyo idadi ya wateja ndio inayoamua kiasi gani wacharge, ikitokea kusini mwa jangwa la Sahara kila mtu akaweka DStv Basi wanaweza hata kucharge chini ya 30,000 kuangalia mpira.

Canal+ Ni part ya Vivendi Ina subscribers milioni 16, Kila mtu akilipa hata 10,000 kwa mwezi tayari hio inakaribia trilioni 2 kwa mwaka, kwao Ni rahisi kumudu kulipia vitu Kama Epl na Uefa.

DStv wao Wana 7.7m subscribers hawafiki hata nusu ya hao jamaa, hivyo inabidi wacharge Hela kubwa kuweza kuhimili gharama.

Mfano ligi ya Uingereza tu Kuinunua DStv wamelipa Kama 300M pounds ambazo Ni Karibia trilioni 1. Hivyo unaona Hivi vitu vilivyo na gharama.
 
Dawa ya dstv hapa Tanzania ni serikali iruhusu soko huria. Wawape ruhusa Canal na bein sport wafanye kazi kisheria. Hapo wenyewe watashusha bei. Haiwezekani Nigeria walipe elfu 50 za kibongo kifirushi cha premium
Sio serikali Inayoamua Ni ligi ya Uingereza (sky sport, ama kampuni nyengine Kama mashindano Ni tofauti). Na hata beIN ama canal walionunua hizo haki za Africa wao pia itawalazimu kupandisha Bei kutokana na uchache wa wa Africa kwenye kulipia.
 
Kuangalia mpira siku hizi easy, Android tv box, Smart Tv na Simu. Kila mtu ana simu tena unacheki bila mazengwe na unaweza kudownload match nzima baadae ili uwe unajikumbusha.
 
Nimekusoma mkuu
 
Wewe una matatizo kichwani
Matatizo gani?
Huoni kama ni maoni yangu hayo na yanapaswa kuheshimiwa kwanza nimetumia neno "sidhani" hivyo naweza nikawa sahihi au siko sahihi.
.
Truth is bitter mimi ni fundi madish mzuri sana so naongea nachokijua
 
Miatano ni huko unakoishi ama Tanzaniana mzima?
Mia tano Tanzania nzima ambayo yako active kwa maana wanayalipia wenye nayo.
.
Mimi namalizaga hata miezi sita sijalipia sasa mimi ni mteja active au mteja hewa?
Alafu hawana hata wateja wengi sasa kwa taarifa yako dealers wa visimbuzi najuana nao sana kwa sababu ni sehemu ya kazi yangu
Dodoma yani ukitaka udodewe na biashara nunua DSTV ukitaka uuze nunua Azam
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…