UEFA EURO 2024: Special Thread | Final: FT: Spain 2-1 England (Spain aibuka bingwa)

UEFA EURO 2024: Special Thread | Final: FT: Spain 2-1 England (Spain aibuka bingwa)

GOAL! Scotland 0-1 Hungary Kevin Csoboth
CgAGVWZ4jHSAS8I-APQxCmo4Y0w012.gif
 
Asanteni sana Hungary kweli mlikuwa na njaa ya kupata kitu tangu mechi ya kwanza na hatimae mmekipata, nataka kuona jinsi mnavyowakazia Spain kwenye mtoano na hatimae kumfulumusha mapema sana.
 
Kwa hii aggressive high pressing waliyo nayo ujerumani hili kuwazuia wasikufunge nyingi inakubidi uwe na mabeki watulivu sana wenye confidence ya hali ya juu na sio mabeki wa kubutua butua tu...!! Maana waki uwin mpira ndani ya eneo lako wanakumaliza, na leo mabeki wa Switzerland walijitahidi sana kukabiliana na hilo.
 
Kingine ambacho nimekiona mpaka sasa, hawa wenzetu wanajua kwenda na momentum ya mchezo, wakiwa wanatafuta goli basi ujue linapatikana muda wowote na watalitafuta kwa nguvu zote.....

Huku kwetu Africa ubao ukiwa unasomeka 0-0 mpaka dk ya 70 basi ujue kuna uwezekano mkubwa sana mechi ikamalizika hivyo hivyo na hata wachezaji wenyewe kadri muda unavyozid kuyoyoma unawaona kabisa wanajikatia tamaa.
 
KDB ni mchezaji mzuri sana anaweza kuwa level moja na zidane

Tofauti yao ni kwasababu KDB amecheza timu ndogo ndio maana haimbwi km zidane

KDB angecheza
real madrid
Manchester united
Barcelona

Angekuwa na heshima zaidi

Kombe la dunia ndio linamtofautisha zidane na kdb
Acha matusi wewe, kdb anaweza kuwa level moja na nani etii?

Bila shaka wewe ni miongoni mwa wale ambao Zidane mmekuja kumuangalizia YouTube baada ya kuwa ameshaacha mpira na hamkumuona akicheza kama mnavyomuangalia kdb sasa.
 
Hujui ball wewe. Striker anapimwa kwa magoli aliyoweka kambani otherwise niambie striker apimwe kwa kutumia kigezo gani?
Bana wewe mtu wa kizazi cha takwimu kubishana na wewe ni kupoteza muda tu maana unavyojibu unajionesha jinsi gani ulivyo mweupe kama jamaa yako Lukaku...

Labda kwa kukusadia tu kwa kutumia hicho hicho kigezo chako cha takwimu, ubora au uwezo wa striker unapimwa kwa goal contribution(G+A) pamoja na Expected goal(XG) sasa lukaku wako msimu huu peke yake tu akiwa na Roma kwenye mechi 47 kafunga goli 20 na katoa assists 5 tu kwa hiyo G+A yake ni 25 wastani ambao kikawaida ni wa mastriker wa daraja la tatu kabisa.... tukiachana na hilo yeye ndio kapiga mashuti mengi nje akifuatana na Osimhen na XG yake ni 0.46 ambapo watu kama Lautaro wana 0.9.

Sasa wewe ukiulizwa striker wa maana utamtaja huyu Lukaku?

Tukiachana na hivyo vigezo vyako vya kitakwimu, kingine kinachoangaliwa kwenye ubora wa striker ni individual brilliance ambayo Lukaku hana, sijawahi kumuona lukaku akipunguza hata mabeki wawili, uwezo wa ku hold mpira kwenye eneo la mpinzani huku ukiwasubiri wenzio wafike labda hili kidogo anajitahidi, correct movements ajue jinsi ya kuchota attention za mabeki kwa mikimbio sahihi na kutoa mwanya kwa wenzake kufunga.

Sasa haya yote striker wako Lukaku anayo kwa uchache sana...

Ukiulizwa striker wa maana na akili zako timamu bado utamtaja Lukaku?
 
Nchi zote zinacheza Euro 2024 zipo karibu na Ujerumani isipokuwa Sweden ndio kila mechi mashabiki wanajaa. Halafu miundombinu ya usafiri iko vizuri
Usiseme hivyo huko enzi na enzi tu, huwa mashabiki wanajaa uwanjan hata iwe wapi, wezetu kwenye mambo ya maisha wako juu sana, watu wengi wana uhakika na kipato, ndo bara lililoendea zaidi'!
 
Labda kwa kukusadia tu kwa kutumia hicho hicho kigezo chako cha takwimu, ubora au uwezo wa striker unapimwa kwa goal contribution(G+A) pamoja na Expected goal(XG) sasa lukaku wako msimu huu peke yake tu akiwa na Roma kwenye mechi 47 kafunga goli 20 na katoa assists 5 tu kwa hiyo G+A yake ni 25 wastani ambao kikawaida ni wa mastriker wa daraja la tatu kabisa.... tukiachana na hilo yeye ndio kapiga mashuti mengi nje akifuatana na Osimhen na XG yake ni 0.46 ambapo watu kama Lautaro wana 0.9.
Nilichopenda umekubali kigezo cha Goal involvement ni kigezo cha kwanza kwa striker. Kinachobaki nadhani ni nature ya ubishi tu kwa sababu kama striker kacheza mechi 47 kahusika kwenye magoli 25 unasema ni striker wa daraja la 3 🤣🤣
Tukiachana na hivyo vigezo vyako vya kitakwimu, kingine kinachoangaliwa kwenye ubora wa striker ni individual brilliance ambayo Lukaku hana, sijawahi kumuona lukaku akipunguza hata mabeki wawili, uwezo wa ku hold mpira kwenye eneo la mpinzani huku ukiwasubiri wenzio wafike labda hili kidogo anajitahidi, correct movements ajue jinsi ya kuchota attention za mabeki kwa mikimbio sahihi na kutoa mwanya kwa wenzake kufunga.
Unageuka geuka maneno yako mwenyewe. Unasema hana individual brilliance halafu unasema labda kuhold mpira huku akisubiri wenzake wafike anajitahidi sasa kipi ni kipi.? Nakuongezea nyingine Lukaku ana uwezo wa kushuka chini kutafuta mipira na kupandisha juu hiyo ni moja brilliant skill pengine huja notice kwake.
 
Back
Top Bottom