UEFA EURO 2024: Special Thread | Final: FT: Spain 2-1 England (Spain aibuka bingwa)

UEFA EURO 2024: Special Thread | Final: FT: Spain 2-1 England (Spain aibuka bingwa)

Actually the final of this tournament was played in quarterfinal stage which was Germany vs Spain clash.... baada ya hapo ilikuwa ni kama formalities, yeyote aliyekuwa anapita hapo alikuwa anaenda kuwa bingwa.

Angalia kati ya wapinzani wote waliokutana na Spain ni mjerumani pekee tu ndio alimpa shida, kwanza ndio timu pekee iliyomlazimisha kwenda extra time, ndio timu pekee iliyomzidi ball possesion hasa zile dk 30 za nyongeza na ndio timu pekee iliyomzidi expected goal(Xg) 1.8 kwa 1.6.

Hao wapinzani wengine wote walikuwa wanazidiwa kila kitu.
Final ilikuwa Germany na Spain hizi zingine Spain hajapata challenge yoyote
 
Mfano msuva na Samatta wale viwango hakuna tena wanaziba nafasi za vijana

Pogba angekuwa bongo bado angeitwa national team hata kama hachezi

Tanzania tunaijua sisi hii

Fikiria Sergio Ramos kaachwa Spain sababu wanajua jamaa kashachoka ila ingekuwa huku angeitwa tu

Spain walianza muda ule kujijenga upya baada ya kuona wazi wachezaji wao maji yamefika shingoni

Leo wana kina yamal, Nico, zubimendi, Dani olmo nk
Tanzania furaha ya mpira imeishia kwenye vimbwanga na mafanikio ya timu mapacha wa kariakoo tu basi, ambazo na zenyewe mafanikio yao yanategemea zaidi wageni.

Hakunaga anayejali kuhusu timu yetu ya taifa sio serikali, sio TFF sio wabongo wenyewe.

Ukitaka kuamini hakuna yoyote anayejali kuhusu taifa stars, angalia tukitolewa au tukishindwa kufuzu kwenye michuano yoyote ile mikubwa huwezi kuskia kelele za aina yoyote ile wala maoni.... ila sasa angalia Yanga na Simba wakitolewaga kwenye michuano ya kimataifa jinsi inavyokuwepo mijadala isiyoisha tena iliyojaa hisia kali sana kutoka kila kona ya nchi.
 
Back
Top Bottom