UEFA EURO 2024: Special Thread | Final: FT: Spain 2-1 England (Spain aibuka bingwa)

Huwa nashangaa sana hawa wachezaji wa miaka hii roho mbaya hawana kabisa....

Hivi mtu anakokota mpira anaelekea golini kwenu na wakati huo muda umeshaisha mnahesabu sekunde tu, unashindwa nini kumchezea technical foul pale kisha ukala kadi yako ya njano halafu wakapewa hiyo freekick mkajipanga vizuri, mkaokoa kisha mpira ukaisha, ukawa umeiokoa timu yako na heartbreaking kama hii...?

Yaani mnamuacha mtu anakokota mpira anaenda kutoa assist nyie mnamsindikiza tu, halafu mnafungwa eti mnaanza kushika vichwa? Haloo Sergio Ramos asingekubali ule ujinga aliyefanya Brozovic na mwenzie.
 

Brozovic ni katili dizain ya kina Pepe ila pale angepiga buti tu angekula red kwsbb tayari ana njano na ameshaonywa sana...mwenzie pia ana njano
 
Brozovic ni katili dizain ya kina Pepe ila pale angepiga buti tu angekula red kwsbb tayari ana njano na ameshaonywa sana...mwenzie pia ana njano pia
Katika situation kama ile unaogopa redcard ya nini na muda umeisha?

Kwani hata asipocheza mechi ijayo hakuna wachezaji wengine wakucheza nafasi yake?

world cup ya 2018 wakati brazil anakufa 2-1 mbele ya ubeligiji goli la pili walilofungwa ni la mazingira kama hayo, fernandinho alimsindikiza lukaku mpaka anampa assist debryne....

Ronaldo Delima alimlaumu sana Fernandinho kwamba na uzoefu wake wote alishindwa kucheza technical foul....
 
Kwenye AFcon iliyopita fainali,yule beki wa ivory cost ,alifanya hiyo,Akala red kadi yake,lakini ubigwa wamechukua
 
Huwa nawaambia na hata hapa nawahakikishia...France ikishapita hapa hakuna nchi itaifunga tena, Spain hawezi kumfunga France
Ngoja tuone.

Maana hata mimi naamini baada ya hii group stage England itabadilika sana, na hakuna timu itakaweza kuwafunga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…