UEFA yatangaza kikosi cha wachezaji bora Klabu Bingwa

poposindege

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2010
Posts
453
Reaction score
175
UEFA imetangaza orodha ya wachezaji 18 walio bora zaidi kuwahi kucheza katika ligi ya mabingwa wa Ulaya.

Kwa mujibu wa orodha ya wachezaji 18 bora kucheza katika Champions League inajumuisha Wahispania 5, wachezaji 2 kutoka kila nchi za Brazil, Uingereza, Ufaransa na Italia, mchezaji mmoja kutoka Ujerumani, Czech Republic, Uswizi, Ureno na Argentina.


Katika 11 bora Ilker Casillas analinda lango.

Safu ya Ulinzi inashikiliwa na Sergio Ramos, Carlos Puyol, Alessandro Nesta na Philipp Lahm.

Viungo bora waliochaguliwa ni Steven Gerrard, Andres Iniesta na Xavi Hernandes.

Safu ya washambuliaji inashikiliwa na Cristiano Ronaldo, Lionel Messi na Thierry Henry.


Katika wachezaji saba mbadala waliokamilisha orodha ya wachezaji 18 bora ni Zinadine Zidane, Zlatan Ibrahimovic, Gianluigi Buffon, John Terry, Pev Nedved na Wabrazil Kaka na Ronaldinho.

Chanzo: michezo365
 

Attachments

  • uefa.jpg
    37.3 KB · Views: 4,982
Mbona first eleven wote wa juzi tuu, yupo wapi rood van nestrory, Shevchenko, Edgar davis, Luis Figo, sebastian veron, rivaldo,??
 
Mbona first eleven wote wa juzi tuu, yupo wapi rood van nestrory, Shevchenko, Edgar davis, Luis Figo, sebastian veron, rivaldo,??

Dah enzi zao bana walitisha .
 
kwahiyo akina paul maldin+delima+lucio+zola+del piero wanazidiwa na hao??????
 
Ryan giggs mbona hayupo au wao wanamuona wa kawaida?
 
as long as chogo yupo sina lakubisha
 
wangetoa list ya wachezaji 50 ingeridhisha zaidi.. Majembe yako mengi.. List ya watu 18 ni ndogo sana
 
Hao jamaa wamechemsha!!
De Lima hayupo???

Mimi nadhani wapo sawa kwa kuangalia idadi ya mechi za Champions League alizocheza na mchango wake kwa nafasi aliyokuwa anacheza. Ronaldo Lima ni bonge la striker, lakini amefunga magoli machache na amecheza mechi chache za champions league. Kazi ya mshambuliaji wa kati ni kufunga magoli, ukiangalia orodha ya wafungaji wa muda wote wa champions league, Ronaldo de Lima hayupo hata 5 bora
 
De lima,deco,kluvert,beckan,rivalvo. roberto carlos. mbona wapo wengi tu.
 
Ushuzi mtu yaani Gerrad ni kiungo bora kuliko Paul Scholes !.
 
Duh!hiyo timu gaucho ana choma mahindi timu gani hiyo?kuna effenberg Paul Scholes de Piero Juan veron na Juan roman requeme siwaoni hapo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…