UEFA Zamani, sasa ni mfano tu.

UEFA Zamani, sasa ni mfano tu.

Misimu mitano makombe matano still gaucho hakua mbaya kama unavyodhani
Hayo ya nje ya uwanja mimi hayanihusu akhui...nnachoongelea hapa ni ufundi + mafanikio ndani ya uwanja.. hii ndio point yangu.

Gaucho atakumbukwa kwa lipi pale Barca?

GAUCHO 2003-2008 [emoji116]

Winner:
La Liga (2): 2004–05, 2005–06 mara 2

UEFA Champions League: 2005–06 mara 1

Supercopa de España (2): 2005, 2006 mara 2

Ballon d' ore amechukua mara 1 tu....haya ndio mafanikio katika timu!!

Sasa huyu utamlinganisha na Messi kweli! Mwenye La liga 10..Uefa 4..Copa del-rey 6..Supercopa de espana 8..Uefa super cup 3..Fifa club w/c 3..na Ballon de' ore 5 and 6 is download....!!!!!

La liga best player mara 8..La liga best foward mara 7..Fifa Club World Cup Golden Ball ameshinda mara 2..Pichichi Trophy ameshinda mara 6..ana magoli mengi zaidi + freekicks goals nk!!!

Jamani hata kama ni chuki sio hivyo tena, mpeni haki yake huyu mja ndivyo Mungu alivyomjaalia kiumbe chake! Duh! Sipati picha mafanikio haya angeyapaya Gaucho naamini kabisa pasingezungumzika humu!

G_real
 
Hao hao AC Milan, Liver anapindua matokeo? Au umeamua tu kutukumbusha kua alikuwepo beki anaitwa Gattuso.
Msimu uliopita Messi ndo mchezaji aliyezifunga magoli mengi timu kubwa sita za uingereza japo hachezi uko. Ndo useme hao mabeki wangeweza kumzuia Messi.
Messi na CR 7 ndo wachezaji bora wa dunia wa muda wote, acha kuwafananisha na akina Kaka. Hao jamaa daraja lao ni tofauti kabsa.

Ronaldo alitiwa mfukoni na Gatusso dakika 360. walizowahi kukutana. huwezi kumbuka dogo
 
Naomba uambatanishe mafanikio yao hapa, Messi na Gaucho! Maana mmeshupalia alikuwa fundi [emoji3] ufundi wake umeipatia mafanikio gani timu yake zaidi ya kuruka ruka na kupiga watu kanzu hayo ndio mafanikio katika timu mkuu!!! Kama ni skills, dribbling, playmaker, goals scorers, freekicks na maudambwi yote + mafanikio Messi is everything...Gaucho nimemfuatilia hata kwa Zidane, Iniesta na Cr7 ni kimeo tu hana lolote unampamba tu..sembuse Messi anaeshindanishwa na akina Maradona na Pele!!! Kuwa serious Wanjiru!

Ukija kwenye magoli katika career zao jamaa yako kafunikwa vibaya sana, ila unaona aibu kuyaanika hapa...hata jamaa yako hapo juu ameshindwa kuweka ukweli badala yake akaamua kanitukana,it's okay...

Okay mimi nitakusaidia mkuu [emoji116]

Gaucho kaanza kucheza 1998 na kumalizia soka lake huko brazil mwaka wa 2015 na magoli yake ni kama yafuatayo.

Gaucho Mechi 717=Magoli 280 [emoji23][emoji23][emoji23]
Messi Magoli 828=Magoli 672 [emoji7][emoji7][emoji7]Just think mpaka anastaafu huyu kiumbe unategemea atakuwa na magoli mangapi katika career yake!!!

GAUCHO[emoji116]
Kwa miaka yote 10 kazitumikia hizi klabu alizocheza PSG+BARCELONA+AC MILAN ana vigoli 145 [emoji23][emoji23]

Haya huko nchini mwao brazil kwenye ligi nyepesi ameshindwa kutamba kwa miaka 7 na kuambulia vigoli 135, si aibu jamani [emoji23][emoji23]


Tatizo la wabongo mlishakaririshwa kitu cha zamani ni bora kuliko cha sasa..hayo ni magari/Vipuri jamani ni tofauti na sisi binadamu.. Binadamu hatubadiliki tuko vile vile ni vipaji tu kutoka kwa Mungu anampa amtakae..Hivyo Wanjiru mkubali tu Messi na Maradona ni namba zingine hizi [emoji3]

Cc G_real
Kuna ile hoja/dhana kutoka kwa mashabiki wengi kuwa, Ubora wa mchezaji unaonekana pale atakapocheza katika club mbalimbali tofauto ama za nchi mbalimbali zenye mifumo na itikadi tofauti za soka.

Kwa mfano Zidane, De Lima, Gaucho, Cr7 na wengine tofauti na Messi.

Unalizungumziaje hili?
 
Kila time na moments zake. Kila Eufa ni nzuri kwa kipindi chake. Sijui Messi angempita Gatusso hutakaa upate jibu maana kila mmoja kacheza wakati tofauti.
Enjoy soccer Bwana. Tukutane tarehe 22/10,23/10.Fainali yangu ya kwanza kuangali ni pale Man united walifanya come back na ndo chanzo mimi kuwa shabiki wa Man united. Sijaacha kuangalia UEFA CL tokea kipindi hicho na ninaenjoy kila moments.
Weye mrembo ni mwanamichezo kweli umefanya iwe rahisi sana mtu kukuelewa kila zama na kitabu chake waqt wa hao alowataja mabeki shupavu walipitwa na washambuliaji hodari mpira unapita katika nyakati na mbinu tofauti sana
 
mpira umeisha ladha,lukaku ananunuliwa kwa 70m+!!!...wanarukaruka tu
Huo ndio upuuzi uliopo siku hizi sio kiwango cha mchezaji kinachoamua thamani yake ila soko ndio linkulazimisha ununue hivyo ukiacha wenzio wanachukua ni ujinga wa hali ya juu
 
Mbona haikufanya maajabu kama hii ya kina CR7 ?

Time mkuu, Enzi zile kulikua na ushindani wa ukweli. Hivi sasa ulaya nzima timu za mana unazihesabu mastaa wote wamekusanyika kwenye timu chache.
 
Dogo umekua juzi weye inaonekanwa
Mtu kucheza zamani haimaanishi yeye ni bora kuliko wachezaji wa sasa tunaangalia statistics zao na hao unaosifia kisa wa zamani tu kwa uefa sina shaka na Ronaldo hata ukimlinganisha na. hao wa zamani
 
Hivi upo serious kuwa Madrid ya cr7 ilikuwa tishio kushinda ya akina raul zidane figo carlos kuwa makini na unachosema
Hivi tishio unamaanisha majina au matokeo? kwa upande wa matokeo ni wazi Madrid ya Cr7 Uefa ni bora kuliko hiyo ya kina Raul,zidane,de lima kwa ujumla wao
 
Mkuu hiyo Real ingechukuaje mara mbili mfululizo au zaidi wakati timu zilikuwa zimeshegeni vipaji. Niatakupa mfano, Mwaka 2002 Real ilichukua ndoo kwa kuifunga Buyern Liverkusen ya kina Ballack goli moja bila, mwaka 2003 Real hii ikiwa na Iker Casilas, Roberto Carlos, Claude Makele, Zidane, Ronaldo De Lima, Raul Gonzales, Ruis Figo, Fernando Redondo waliitoa Machester United kwa Jumla ya Magoli 6-4, Manchester wakifa 3-0 bila Bernabeu lakini wakashinda 4-3 Old Traford, hii ilikuwa bonge la Mechi hasa ya marudio. Nusu Finally Real akapangwa na Juventus, Juve wakaenda Bernabeu wakala 3-0, Madrid akaenda Pale Turin akachezea 4-0, hapa Casilass hawezi kumsahau Del pierro, Hawa Juventus waliotoka kumchakaza Madrid wanaingia finally na Ac Milan na Milani anachukua ndoo. Ninachotaka kukuonyesha hapa ni namna gani miaka hiyo ikikuwa ngumu kuchukua ndoo ya EUFA back to back kwakuwa timu zilikuwa na wanaume kweli kweli, Mzee Fergie pamoja na umaarufu wake wote pamoja na heshima zake, muulize amechukua EUFA mara ngapi!? Mzee Wenger ndio usiseme! Nenda kaangalie battle za Chelsea na Barcelona miaka hiyo ya 2004-2005, 2005-2006, hadi kuja 2008 uone wanaume walivyokuwa wanatoana jasho, halafu urudi useme kama Huyu Zidanw angeweza kuchukua EUFA back to Back miaka hiyo!
Kusema Real Madrid kachukua back to back uefa eti kisa vilabu vingine sio bora si kweli kuna vilabu vingi vimeshindwa fanya hivyo katika zama hizi Mfano, Barcelona,Juventus,Atletico,Bayern usifosi tuamini kuwa timu zimekuwa nyepesi kwahiyo ni madrid pekee ndio imebaki timu ngumu ulaya hadi ionee wengine na kwa uelewa wako kuanzia mwaka gani unahisi uefa imeanza kuwa nyepesi?
 
Inatamba vipi ulaya kaka wakati toka upo makundi mpaka fainali unakutana na first eleven iliyosheheni vipaji tupu tofauti na sasa...
Hiyo haiondoi ukweli kuwa wote hao hawana rekodi yoyote ya kutisha kuizid Madrid ya cr7 wanachozid ni ukongwe na Majina najua kuna kasumba ya kusifia sana vitu vikishapita ila hiyo isitufanye tubadili uhalisia najua miaka kumi ijayo maneno kama haya yatakuwepo na watu watakuwa wanazungumzia ubora wa kina Messi na Ronaldo kwa wakati huo
 
Akina kaka ni kama akina Aguero, Neimar, Dybala, Pogba n.k...wangelikuwepo kipindi hiki wangelikuwa wanachuana na akina aguero tu...na Ballon wasingeambulia...tatizo la watanzania kitu cha zamani wanakiona kina thamani kuliko cha sasa, wakati binadamu ni wale wale tu basi ni akili ya mchezaji tu..alafu kipindi hiki sheria kibao + VAR.
Hili ndilo linalowatesa wao majina ya zamani wanaona kama Miungu hao wachezaji anaowataja wengi ni wa kawaida tu sawa na kina lewandowsk,Aguero,suarez,De bruyne Neymar,Dybala na Mbappe wala sio wa maajabu kama wanavyotuaminisha
 
Hili ndilo linalowatesa wao majina ya zamani wanaona kama Miungu hao wachezaji anaowataja wengi ni wa kawaida tu sawa na kina lewandowsk,Aguero,suarez,De bruyne Neymar,Dybala na Mbappe wala sio wa maajabu kama wanavyotuaminisha


Kabisa kamanda, na records/Statistics zinajionyesha dhahiri lakini mmatumbi hakuelewi kabisa 😀😀
 
Kusema Real Madrid kachukua back to back uefa eti kisa vilabu vingine sio bora si kweli kuna vilabu vingi vimeshindwa fanya hivyo katika zama hizi Mfano, Barcelona,Juventus,Atletico,Bayern usifosi tuamini kuwa timu zimekuwa nyepesi kwahiyo ni madrid pekee ndio imebaki timu ngumu ulaya hadi ionee wengine na kwa uelewa wako kuanzia mwaka gani unahisi uefa imeanza kuwa nyepesi?
Mkuu miaka ambayo Real Madrid amechukua back to back, team nyingi zilikuwa hovyo,.lakini hata kiwango Cha team miaka hii kinapungua mno, atleat Madrid walikuwa na kikosi ambacho bado kilikuwa na binasaba vile. Hivi kwa akili zako unategemea Manchester hii ya kina Rashiford ilete ushindani. Angalia viwango vya timu Kama Chelsea, Juventus, Ac Milan, Arsenal, Intermilan n.k katika miaka aliyochukua Madrid vilikuwaje, halafu urudi useme neno!
 
Kuna ile hoja/dhana kutoka kwa mashabiki wengi kuwa, Ubora wa mchezaji unaonekana pale atakapocheza katika club mbalimbali tofauto ama za nchi mbalimbali zenye mifumo na itikadi tofauti za soka.

Kwa mfano Zidane, De Lima, Gaucho, Cr7 na wengine tofauti na Messi.

Unalizungumziaje hili?


Hawana hoja za msingi hao ni chuki tu zinawasumbua kamanda...kama ni hivyo basi Anelka aliecheza Klabu12 katika nchi 7 tofauti na hajachukua uchezaji bora hata moja..
 
Misimu mitano makombe matano still gaucho hakua mbaya kama unavyodhani


Hakuna aliesema mmbaya, alijitahidi kiasi chake ndani ya miaka mitatu, ila kumfananisha na hawa jamaa ni kosa kubwa sana

Messi
Maradona
Pele
Johan Cruiff
Alfredo de Stefano
Zidane
Cr7
Ferenc Puscas
Iniesta
Ronaldo 9
 
Hakuna aliesema mmbaya, alijitahidi kiasi chake ndani ya miaka mitatu, ila kumfananisha na hawa jamaa ni kosa kubwa sana

Messi
Maradona
Pele
Johan Cruiff
Alfredo de Stefano
Zidane
Cr7
Ferenc Puscas
Iniesta
Ronaldo 9
Mkuu Zidane alifanya nin cha maana kumshinda Dihno?
 
Back
Top Bottom