Uekezaji kwenye bodaboda

shylock

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2017
Posts
795
Reaction score
1,334
Habari za usiku ndugu zanguni,,,
Ngoja niende direct to the point.
Nataka kuwekeza kwenye bodaboda ila ni buashara ambayo sijawahi kumfanya wala kuiwaza.
Kuna jamaa mmoja kanishawishi ninunue pikipiki yeye ataniunganisha na dereva. Kila wiki nakula 70. Mkataba ni mwaka mmoja. Naomba yeyote mwenye utaalam na hii biashara anisaidie.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni biashara ngumu kidogo, hasa ukizingatia madereva walivyo... Kikubwa kama una nia kweli wape mikataba. Mnakubaliana kwamba anakupa kiasi fulani cha pesa na baada ya miezi kadhaa zinakuwa zao.... Hakikisha mnaandikisha panapojulikana.... na lazima mseme ikiibiwa inakuwaje, mmojawenu akifa inakuwaje...
 
Hapo kwa kuibiwa si anaweza akafanya maujanja. Ionekane imeibiwa kumbe kauza.?
Unahisi mkataba unachukuww mda gani. Maana naskia pikipiki pendwa yaan TV'S na Boxer ni 2million
Sent using Jamii Forums mobile app
 



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi huwa nafanya hivi,
Kwakuwa mi mwenyewe ni bdbd, huwa nawatambua vijana wapiga kazi. Nawapa kwa mkataba wa mwaka mmoja. Yaani siku 365 najumlisha na siku40 ambazo ni jumapilizote kwa mwaka. Napata siku 405. Kwa siku on sh 10,000/= so inakuwa ni 4,050,000/= lakini siku zile ambazo nilizitoa kwa maana 40 days ni jumapili ambazo ni kwa akili ya service na kama akipiga kazi ni za kwake.
Na lazima awe na leseni, ajishimu yeye na kazi yake. Utanashati NASA Usafi wa ngyo ni muhimu. Usafi wa chombo husika.katuka mkataba lazima ajue kiwa kikiibiwa ama kupotea kwa uzembe anawajibika kukilipa kwa fharama halisi. Hii itamfanya kuwa makini. Lazima awe na wadhamini wawili ambao wana elewa mini maana ya mkataba.
Akikatisha mkataba inakiwa imekula kwake, kwa sababu wengi wao wakupata MTU akawadanganya huwa wanakurudishia Pkpk ama wanaitelekeza.
Kwa hayo machache utakuwa umepata mwanga.
Kuhusu service, spoket na chain kwa maana ya full package anawajibika mwenyewe isipokuwa tairi ya mbele na nyuma anawajibika tajiri.

Wa kwangu mmoja amemaliza, sasa ni mmiliki.

Ila inabidi kuwajua hawa bdbd
Bdbd psychology. Usikaze saaaaaaana kuna siku anabanwa unamuelewa kikubwa lakini hatakiwi kuzidisha siku NNE bila kuleta maelezo ya kwanini anakwama. Lakini kuna wakati mwingine mvua kubwa inaweza sababisha akashindwa kufikia lengo.

Lakini pia, anaweza pata janga LA ajali, usipanik sana Bali ni namna gani mnakaa chini na kuna namna ya kusaidiana. Kama amegonga mtoto na anahitaji matibabu, huwa namkopesha na kusimamia shoo NASA kuweka mahusiano sawa kati ya malezi ama mzazi wa mtoto.

Ila kama na were mwelewa wa mambo ya barabarani utajua namna ya kwenda nao sambamba.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nahitaji kukutafuta mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante umenipa darasa tosha.
Je, kwa ubora we pikipiki ni ipi zuri . Boxer,hero au tvs
 
GOOD
 
Biashara nimeifanya sana hii! ila ni risk kubwa sana, usiweke 70000 uhakika kwa wiki.....bodaboda wanachangamoto lukuki.......Unaweza nunua mpya ukamkabidhi akabebea bangi na ikakamatwa, kuja kutoka ushaenda nje ya malengo yako.....

Ina faida ila ni Changamoto saaaana, tena saaaana tu, kuanguka, kuibiwa, matengenezo, dereva kuumwa, kukamatwa ni common

Unaweza kupata 280,000/= kwa mwezi hlf ukaingia hasara ya matengenezo ya 100,000/=

kila la kheri mkuu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu kama huna cha muhimu cha kufanya na pesa yako iweke benki ukae ufikiri vzr, hivi kwanza unaanzaje kuiita shughuli ya boda boda eti ni biashara!
 
Aisee unanikatisha tamaa kabisa
Mkuu kama huna cha muhimu cha kufanya na pesa yako iweke benki ukae ufikiri vzr, hivi kwanza unaanzaje kuiita shughuli ya boda boda eti ni biashara!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…