Mimi huwa nafanya hivi,
Kwakuwa mi mwenyewe ni bdbd, huwa nawatambua vijana wapiga kazi. Nawapa kwa mkataba wa mwaka mmoja. Yaani siku 365 najumlisha na siku40 ambazo ni jumapilizote kwa mwaka. Napata siku 405. Kwa siku on sh 10,000/= so inakuwa ni 4,050,000/= lakini siku zile ambazo nilizitoa kwa maana 40 days ni jumapili ambazo ni kwa akili ya service na kama akipiga kazi ni za kwake.
Na lazima awe na leseni, ajishimu yeye na kazi yake. Utanashati NASA Usafi wa ngyo ni muhimu. Usafi wa chombo husika.katuka mkataba lazima ajue kiwa kikiibiwa ama kupotea kwa uzembe anawajibika kukilipa kwa fharama halisi. Hii itamfanya kuwa makini. Lazima awe na wadhamini wawili ambao wana elewa mini maana ya mkataba.
Akikatisha mkataba inakiwa imekula kwake, kwa sababu wengi wao wakupata MTU akawadanganya huwa wanakurudishia Pkpk ama wanaitelekeza.
Kwa hayo machache utakuwa umepata mwanga.
Kuhusu service, spoket na chain kwa maana ya full package anawajibika mwenyewe isipokuwa tairi ya mbele na nyuma anawajibika tajiri.
Wa kwangu mmoja amemaliza, sasa ni mmiliki.
Ila inabidi kuwajua hawa bdbd
Bdbd psychology. Usikaze saaaaaaana kuna siku anabanwa unamuelewa kikubwa lakini hatakiwi kuzidisha siku NNE bila kuleta maelezo ya kwanini anakwama. Lakini kuna wakati mwingine mvua kubwa inaweza sababisha akashindwa kufikia lengo.
Lakini pia, anaweza pata janga LA ajali, usipanik sana Bali ni namna gani mnakaa chini na kuna namna ya kusaidiana. Kama amegonga mtoto na anahitaji matibabu, huwa namkopesha na kusimamia shoo NASA kuweka mahusiano sawa kati ya malezi ama mzazi wa mtoto.
Ila kama na were mwelewa wa mambo ya barabarani utajua namna ya kwenda nao sambamba.
Sent using
Jamii Forums mobile app