johnthebaptist.
Hapajatokea mgombea mwenye ushawishi kumshinda Mbowe hasa wakati hii tulionao chini ya utawala wa awamu ya tano, wote tunaona wanavyohangaika na Mbowe, kuanzia kuharibu mali zake (mashamba, billicanas) mpaka kumsweka ndani hovyo kwa kesi za kutengeneza.
Walifikia hatua ya kutaka kumuua kwa risasi Mungu akamponya, bahati mbaya akafariki mtoto wa watu Mungu amlaze pema. Kwenye mazingira kama haya Mbowe atashinda sana, mpaka achoke mwenyewe.
Huyo Zitto alinyimwa uwenyekiti wakati ule alikuwa anafanya vikao vya siri na Kikwete, watu wakajua, then mtu wa aina hiyo ndio apewe uenyekiti wa CHADEMA?
Mwambe, huyo bado mchanga, alijaribu akashindwa, na CHADEMA wangekuwa wajinga kama wangempa uenyekiti wa chama, kuthibitisha asivyo mvumilivu leo keshakimbilia CCM.
Wote uliowaorodhesha hapo walipigiwa kura wakashindwa, wajumbe wanajitambua, wanajua wapi wanataka kuelekea kama chama chini ya mwenyekiti Mbowe.
Sasa kama hiyo sio demokrasia sijui kwako ni nini?
Sent using
Jamii Forums mobile app