Uenyekiti wa CCM kwa Rais Samia ndio nyenzo ya kusimama imara kwenye Urais

Uenyekiti wa CCM kwa Rais Samia ndio nyenzo ya kusimama imara kwenye Urais

KARLO MWILAPWA

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2019
Posts
3,250
Reaction score
5,509
Mitandaoni kumeibuka kikundi cha watu ambao naamini ni wanasiasa ambao kwa namna moja au nyingine wanataka kukwamisha juhudi za Mhe. Rais katika kuwatumikia Watanzania. Kikundi hiki kipo nyuma na mbele katika kupingana na muelekeo na mtazamo wa Mhe. Rais na yote inatokana na kuona wapo kwenye nafasi ambazo hawawezi kuguswa na urais kwa kuwa ni wanasiasa.

Ili kikundi hiki kisiendelee kutamalaki na kuonesha dhihaka za wazi, naomba mchakato wa kumpatia uenyekiti wa CCM Rais wetu uharakishwe , ili apate rungu la kuchuma la kujilinda dhidi ya hila zozote ovu za kumdhoofisha.

Natumai Rais wetu akiwa mwenyekiti atakuwa kwenye nafasi nzuri ya kusimama imara kwenye Urais na ndoto alizonazo juu ya taifa letu kutimia kwa mapenzi yake Mungu.
 
Rais ni wa watanzania wote sio Chama tu uimara wake kwenye uraisi uko intact hata kabla kuwa Mwenyekiti .Uimara wake uko kwenye katiba ya nchi ndio inampa mamlaka na kumuimarisha
 
Binafsi Natamani awepo Mwenyekiti mwingine toka hilo kundi la Wanufaika wa CCM maslahi lililoasisiwa na utawala uliopita lenye lengo la kuaminisha Watanzania kwamba nchi hii bila Magufuli kuwa kiongozi haitaendelea.

Walitegemea Samia kuwa spika ya Marehemu utafikiri yeye hana utashi. Napendekeza Uenyekiti apewe mwingine ili tuone Wananchi watakubaliana na upuuzi wa kumkwamisha Rais mpya au watamuunga mkono?

Nitakupa orodha ya kundi hilo humu JF wenye ID chache za zamani na nyingi mpya.
 
Raisi ni wa watanzania wote sio Chama tu uimara wake kwenye uraisi uko intact hata kabla kuwa Mwenyekiti .Uimara wake uko kwenye katiba ya nchi ndio inampa mamlaka na kumuimarisha
Najua hilo lakini uenyekiti ni njia mojawapo ya kumuimarisha na kumfanya ajiamini zaidi.
 
Wewe ndiwe raisi unae. Ogoza Tanzania kwa mfumo umeonyesha faraja kwa watazania wewe Ni suruhu mfariji mwema sasa wewe wasihiri kushi mikamigi yabaraka amen
 
Raisi ni wa watanzania wote sio Chama tu uimara wake kwenye uraisi uko intact hata kabla kuwa Mwenyekiti .Uimara wake uko kwenye katiba ya nchi ndio inampa mamlaka na kumuimarisha
Usichokijua ni kwamba Rais hana nguvu bila kuwa na nguvu ndani ya chama kwa kifupi chama kina uwezo wa kumvua urais kupitia wabunge wake.
 
Usichokijua ni kwamba Rais hana nguvu bila kuwa na nguvu ndani ya chama kwa kifupi chama kina uwezo wa kumvua urais kupitia wabunge wake.
Weka kifungu cha katiba kinachosema hilo tafadhali tusipige porojo hapa
 
Rais ni wa watanzania wote sio Chama tu uimara wake kwenye uraisi uko intact hata kabla kuwa Mwenyekiti .Uimara wake uko kwenye katiba ya nchi ndio inampa mamlaka na kumuimarisha
Sijajua unaongelea swala hili kwa muktadha upi,maana sote tunajua Rais lazima awe mwanachama wa chama cha siasa,hadi hapo unaelewa chama kina nguvu linapokuja swala la kuamua hatima ya "urais" wa mtu pengine kuliko katiba.

Rejea ya Thabo mbeki wa SA. Rais kuwa mwenyekiti wa chama kinachotawala kwa siasa zetu hizi hill jambo haliepukiki.
 
Najua hilo lakini uenyekiti ni njia mojawapo ya kumuimarisha na kumfanya ajiamini zaidi.

..hapo mnamuimarisha mwenyekiti wa chama na genge lake.

..wakati huohuo, mnawadhoofisha wanachama ambao hawako ktk genge la mwenyekiti.

..mngekuwa na busara mngejipa muda wa kumsoma kama ni Rais anayefaa na kuaminika kukabidhiwa chama au la.

..mwenyekiti wa chama ambaye pia ni Rais, na Amiri jeshi mkuu, ni kiongozi asiyedhibitika.
 
Usichokijua ni kwamba Rais hana nguvu bila kuwa na nguvu ndani ya chama kwa kifupi chama kina uwezo wa kumvua urais kupitia wabunge wake.
Taratibu tafadhali × 2
Kabla hamjamvua urais atakuwa amekwisha wamaliza nyoote.
Hapana chezea wadhifa wa Amiri Jeshi Mkuu.
 
Back
Top Bottom