Kufuatia yaliyotokea (sitayarudia hapa), kuna wenye mtazamo kwamba ni matokeo ya ujumbe vs usahihi wa jukwaa ulipotolewa.
Binafsi nimejikuta na fikra tofauti. Je, ni sahihi kuhitimisha kwamba siasa za tutawafanyia/tutawajengea hiki zimepitwa muda wake? Kwa akili zangu za kawaida, naamini wenye kujua siasa na mikakati yake zaidi yangu wanajua haya:
1. Si kazi rahisi kwa serikali za sasa na zijazo "kuwajengea" kuzidi ilvyofanya serikali ya awamu ya tano.
2. Pamoja na kazi kubwa ya "kuwajengea" iliyofanywa na awamu ya tano, uchaguzi kuelekea kwenye awamu yao ya pili haukuwa mrahisi kwao. Yaliyotokea yakatokea.
Pamoja na kweli hizi, kwa nini bado kuna imani kwa watawala wetu kwenye siasa za ahadi za "kuwaletea"? Kwa nyakati na kizazi cha sasa, bado mikakati hii inabakki kuwa sahihi au ni kiashiria cha kukosa mbadala? Na ikiwa hii imani waliyo nayo ni ya kweli, mikakati sahihi si kuwaletea wanachotaka? Kama ndivyo, kwanini mianya ya walengwa kusikika juu ya wanachotaka inaonekana kukumbana na misuguano?