Ufafanuzi: Halima Mdee na wenzake waliingizwa Bungeni na Serikali ya CCM, hawakuingizwa na Ndugai. Hawatafukuzwa

Hii nchi ina mauzauza mengi mno. Inafikia hatua mtu aaingia hadi kwenye chombo cha kutunga sheria kwa kutumia mauzauza kweli ? aisee tujitafakari sana kama taifa.

Watanzania hatuko serious.
 
Anae mfukuza mwenzie nani🤔?
 
Ukiweza kunijibu swali langu hili utakuwa umeyapata majibu ya maswali yako:-
Ikiwa Baraza Kuu la Chadema Lina nguvu ya kuweza kuingilia Mahakama na kumtoa mtuhumiwa Nusrat Hanje gerezani tena usiku na kwenda kuhakikisha kaapishwa kuwa Mbunge. Je iweje lishindwe kutumia nguvu ile ile na kuhakikisha M/Kiti wake anakuwa Huru??
 
Mwenyekiti na Makamu wake hawapo.Nadhani hiyo ndio inafanya kuitisha huo mkutano wa baraza kuu kuwa mgumu.
Hawapo tangu lini
Hebu tuwe factual and focused
Siku zote Lissu amekuwa akishiriki vikao vya chama kwa mtandao.
Watu siku hizi wanashinda SPACE kule twitter lakini kufanya vikao hiwezekani huoni kama ni unafiki
Na je Mbowe kuwa Remand kwa miezi kadhaa ndio kumezuia vikao??
Akidi haitimii?
Katina inasemaje?
 
Unataka kusemaje ?
 
Unachanganya mada. Hapa suala sio kufukuzwa uanachama. Suala ni utaratibu wa kuwatambua kama wabunge. Hawa walitakiwa wateuliwe na chama chao na Tume ya uchaguzi itaarifiwe na Katibu Mkuu wa chama chao kuhusu uteuzi huo. Ndio maana Katibu Mkuu wa kilichokua chama chao aliwaandikia Spika na Tume wa uchaguzi waweke wazi nyaraka kutoka chama chao zilizowatambulisha kuwa hawa wameteuliwa na chama chao. Mpaka leo wote wako kimya. Spika, Tume na wahusika wote wamejikausha. Hivi unadhani Ndugai angekuwa na barua ya utambulisho kutoka kwa Mnyika au Mbowe angeacha kuiweka wazi ili kuonyesha unafik wao? Kusikilizwa au kutosikilizwa kwa rufaa yao ni masuala ya chama chao cha zamani na haina uhusiano na ubunge wao. Au unadhani kuwa rufaa yao ikisikilizwa na kukataliwa na chama chao cha zamani ndio watapoteza ubunge?
Hawa wapo mpaka itakapokuwa convenient kwa waliowaweka kuachana nao. Na dalili ni kuwa watafika 2025 na wataweza kupewa tena ubunge kupitia chama kingine. Au watateuliwa wawe wabunge. Au watapewa nafasi nyingine za kuwafuta machozi. Chama chao cha zamani kinajua hilo ndio maana hawajisumbui nao. Kilichobaki ni wapambane na nafsi zao.

Amandla...
 
Kwa hiyo MDEE anawakilisha CCM?😳
 
Umemaliza kila kitu
 


Kwahiyo Halima Mdee na wenzake hawataondolewa bungeni kwa vile hawakuingizwa na Ndugai.
HAPANA , SEMA,

"Kwa hiyo Halima Mdee na wenzake hawataondolewa Bungeni kwa vile KATIBA YA NCHI NA SHERIA ZA NCHI ZINAVUNJWA NA WANANCHI WANAONA SAWA TU".

Hivyo kinyume cha tungo hiyo pia ni kweli!






 
Kwanza mtoeni Spika kwenye issue hii. Yeye analetewa mbunge na tume. Wala hana nafasi ya kuhoji.
Pili nashangazwa sana na Chama kama Chadema KUSHINDWA kuleta mbinu ya Kuthibitisha kuwa Wabunge wale hawakutokana na Chama.
Leo niwape mbinu moja nyepesi
1. Kamilisheni taratibu za kuwafukuza ikiwemo kusikiliza rufaa na kufanya maamuzi(Hiki ndio kichaka kinachotumiwa na spika kuwalinda wale Wabunge)
2. Nadhani wataenda mahakamani ili wajaribu kuvuta muda au kubaki wabunge wa mahakama.


Wakienda mahakamani bila kujali itachukua muda gani lakini yafuatayo yatajulikana kwenye mwenendo wa kesi
(a) mchakato wa kupata wabunge viti maalum ndani ya chama ulifanyika na kama ndio ulifuata katiba ya chama?
(b) Barua ya kuwatambulisha tume ni halali
(c) Tume ilikuwa ikiwasiliana na nani ndani ya chama ktk kupata wabunge na alikuwa na mamlaka hayo kikatiba?

Kifupi ni kwamba NYARAKA mnazozidai zitatolewa mahakamani .

Mwisho kabisa findings hizi ni very significant kwa context kwamba Kama kweli Tume ilichakachua haki ya chama kuteua wabunge je tutaiamini vip ktk kutekeleza majukumu yake ya kusimamia na kutangaza washindi wa uchaguzi?

Tuache siasa nyepesi. Tunakimbia vita rahisi na kukimbilia vita nzito kama katiba wakati kuna 10% ya watu wetu bungeni
 
Chama kinaelewa mchezo mzima.wasipokuwepo akina Halima bungeni Chadema wanapoteza kuwa chama kikuu cha uoinzani.Tuliopo nje ndio tinatoa mapovu.unavyoshauri vyote chama kinajua cha kufanya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…