Ufafanuzi kuhusu Bima ya Afya kwa wote itakavyokuwa

Ufafanuzi kuhusu Bima ya Afya kwa wote itakavyokuwa

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Wizara ya Afya, imetoa ufafanuzi wa maswali yaliyokuwa yakiulizwa mara kwa mara na wananchi kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kuhusu muswada wa Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote.

Muswada huo umeshafikishwa Bungeni na Oktoba 19, Kamati ya Kudumu ya Bunge Huduma na Maendeleo ya Jamii inataanza kupokea maoni ya wadau kuhusu muswada huo.

Pia muswada wa Sheria ya Bima ya Afya kwa wote inatarajiwa kujadiliwa na kupitishwa na Bunge la Novemba mwaka huu.

ata hivyo, utekelezaji wake rasimu unatarajiwa kuanza rasmi Julai Mosi, 2023 baada ya kuridhiwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

Miongoni mwa maswali yaliyoulizwa na wananchi na kutolewa ufafanuzi na Serikali ni pamoja na je kutakuwa na Mfuko wa Taifa ya Bima ya Afya (NHIF), peke yake?
Je uchangiaji utakuwa ni kiwango gani kwa mwananchi mmoja mmoja na familia ambao siyo waajiriwa rasmi?

Mengine ni Je kwa wananchi ambao ni kaya masikini watahudumiwa kwa utaratibu gani?
Mwanachama atapata huduma za matibabu sehemu yoyote nje ya mkoa anakoishi? kutakuwa na ukomo wa idadi ya wategemezi katika kaya?

Kwa mujibu wa taarifa ya wizara hiyo imeeleza kuwa wananchi waliuliza kwamba je huduma za magonjwa yote zitatolewa kwenye mfumo wa bima ya afya kwa wote? mwanachama ana haki ya kuhama kutoka mfuko mmoja kwenda mwingine bila masharti yoyote?

Katika majibu yao kwa umma Serikali imesema kupitia Sheria inayopendekezwa, mfumo wa bima ya afya nchini utajumuisha bima ya afya ya umma na binafsi.

Pia sheria inayopendekezwa itaitambua NHIF kama Mfuko wa Bima ya Afya wa Umma utakaohudumia watumishi wa umma na wananchi wengine watakaochagua kujiunga na mfuko huo

“Sheria pia inaruhusu kuwepo kwa Skimu binafsi za Bima ya Afya zitakazotoa huduma za Bima ya Afya kwa wananchi katika sekta rasmi binafsi na isiyo rasmi,” imeeleza taarifa hiyo.

Kuhusu uchangiaji utakuwa ni kiwango gani kwa mwananchi mmoja mmoja na familia ambao siyo waaajiriwa rasmi.

Serikali imesema waziri mwenye dhamana ya masuala ya afya kupitia Kanuni ataweka viwango vya uchangiaji kwa kuzingatia uhitaji wa huduma, gharama halisi za matibabu na uwezo wa wananchi kuchangia na mapendekezo yaliyopo yatategemea maoni ya wananchi na ridhaa ya mamlaka zingine.

Suala la ukomo wa idadi ya wategemezi katika kaya Serikali imesema Sheria inayopendekezwa itaweka ukomo wa utegemezi ambapo mwanachama anaweza kusajili mwenza na wategemezi wasiozidi wanne kama wanufaika.

Kuhusu magonjwa yote zitatolewa kwenye Mfumo wa Bima ya Afya kwa wote Serikali imesema kitita cha mafao kitakachotolewa kwa wananchi kitazingatia huduma zote zilizopo katika mwongozo wa tiba (STG), orodha ya Taifa ya Dawa Muhimu (NEMLIT) na aina ya magonjwa kama ilivyoainishwa katika Miongozo ya Tiba ya Kimataifa (ICD 12).

Aidha wananchi watapata huduma hizo kuanzia ngazi ya zahanati hadi hospitali ya Taifa.
 
Hizi ni afya za watu ilitakiwa itolewe elimu Kwa wananchi wote ,maana mfuko wa awali hatujaambiwa sababu za kufa Sasa unakuja mfuko huu Kwa manufaa au siasa
 
Tatizo bei waliyoweka, 340,000 ni ya kada ya kati kwa Tanzania. Vipi kuhusu zile kaya za kipato cha chini ambazo ni zaidi ya 50% hawataweza kulipa kiasi hicho. Je Watawaletea na wao Bima yao?
 
Hzo tozo ndo zingelipa BIMA ya Afya Kwa wote vizur Sana
 
Tatizo bei waliyoweka, 340,000 ni ya kada ya kati kwa Tanzania. Vipi kuhusu zile kaya za kipato cha chini ambazo ni zaidi ya 50% hawataweza kulipa kiasi hicho. Je Watawaletea na wao Bima yao?
Ni kwa ajili yako, kazi kwako kuchagua
Ina maana unakosa 7000 kwa mwezi?
Au unakosa 340000
Kwa watu 6?
 
Lakini kwa wazee wastaafu ambao walikuwa na mkataba na NHIF kwamba baada ya kustaafu wataendelea na bima zao pasipo kulipa fedha yeyote nini nafasi Yao katika mfumo wa bima mpya? Walikuwa wakilipia fedha kupitia mishahara Yao na mwajiri alilazimika pia kuwalipia asilimia fulani wafanyakazi hao. Kwa mfano Mimi Hadi nastaafu nilikuwa nimechangia jumla ya shilingi 16M, je nitaanza kulipia tena huduma hii. Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom