Ufafanuzi kuhusu kanisa Katoliki kutokuwafanyia maziko ya kikanisa baadhi ya waamini wake

Ufafanuzi kuhusu kanisa Katoliki kutokuwafanyia maziko ya kikanisa baadhi ya waamini wake

Umeandika na kufafanua vizuri sana.
Mwenyezi Mungu akubariki sana.
Tumsifu Yesu Kristu.
 
Mimi nimkatoliki lakini mambo haya sikubaliani nayo nahapo sababu kubwa ya kutomzika nikwamba alikua hapokei zike bahasha zenye namba kwaajili ya kuweka michango kama sio sadaka kwani huu utaratibu wakumpa mtu bahasha yenye namba na huko kwenu mkiwa mmerekodi nan anakadi namba ngapi lengo lake huwa ninini kama sio kutaka kujua nan katoa sh.ngapi ilihali sadaka ni siri ambayo ukono wa kulia utoapo mkono wa kushoto hautakiwi kujua kimetolewa kiasi gani sasa kwanini nyie mtake kujua nimetoa kiasi gani[emoji780]
unaongea ukweli kabisa..

rc now days wamejikita kwny hela mno hadi inatia mashaka

sadaka ni siri..
waliona hawaridhiki na makusanyo, wakaanza kuinua mmoja mmoja kwny bench ili uone aibu kutoamka..

sasa wamekuja kwny bahasha zenye namb, ili wajue fulani ametoa kiasi gani..
mtoa sadaka kama huyo mrema asipotoa sadaka.ya matarajio yao, wanamkomesha kutoenda kumzika..

na huko kwny jumuia ndio usisema hio michango
 
Ni Yesu huyo huyo ambaye alitoa mamlaka ya "Nendeni mkawabatize kwa jina la ...na lolote mtakalofunga duniani litafungwa hata mbinguni" samahani sina bible hapa ningekupa ni mistari gani nimenukuu inayotamka hivyo.
kutotoa sadaka ama zaka ipo kwny amri ya ngapi, ili iwe kosa kwa rc wasije kukuzika?
 
Ni Yesu huyo huyo ambaye alitoa mamlaka ya "Nendeni mkawabatize kwa jina la ...na lolote mtakalofunga duniani litafungwa hata mbinguni" samahani sina bible hapa ningekupa ni mistari gani nimenukuu inayotamka hivyo.
Kwani Yesu alitegemea kwamba mapadri watageuka kuwa walawiti, wazinzi na walevi?
 
UFAFANUZI KUHUSU KANISA KATOLIKI KUTOKUWAFANYIA MAZIKO YA KIKANISA BAADHI YA WAAMINI WAKE:

Jana mitandao ya kijamii nchini ilienea habari za kanisa kutokumzika tajiri mmoja kwa sababu alikufa katika hali ya "kinyumba" bila ndoa takatifu, na kwamba hakuwa mshiriki hai wa masuala ya kanisa.

Baada ya hapo kukatokea maneno mengi sana baadhi ya watu wakilishanbulia kanisa katoliki kwamba limekosea na linakosea kwa utaratibu huo, kwa maelezo mepesi kwamba suala la mtu kwenda mbinguni ni wajibu wa Mungu na siyo kazi ya kanisa kuhukumu (huenda wamesahau kwamba kanisa halijaihukumu roho ya marehemu bali limekataa kuuzika mwili wake tu ardhini).

Basi nimewiwa kufafanua kidogo niwezavyo kuhusu suala hili.

Karibu.......

Maziko ya kikanisa hayamfanyi mmoja aliyefariki aende mbinguni wala Jehanamu, bali yanamkumbusha mwombolezaji aliyebaki hai wajibu wake wa kuishi katika ushirika na kanisa ambalo ni mwili wa Kristo.

Kumzika au kutokumzika mtu kikanisa siyo jambo la kubeza ingawa ni kweli siyo linalompeleka marehemu mbinguni au motoni. Tukumbuke mwili wa marehemu unabaki ardhini. Kinachoenda mbinguni au motoni ni roho.

Lakini maziko ya kikanisa ni jambo lenye maana kubwa kutukumbusha tunaobaki duniani kwamba Kanisa ambalo ni mwili wa Kristo na ambalo Kristo mwenyewe ndiye kichwa chake (Waefeso 5:23) linataka waamini tuige mfano wa mwenzetu aliyeishi na kumaliza maisha yake akiwa na ushirika na kanisa, ndiyo maana linafanya maziko ya kikanisa kama sherehe ya kumpongeza, kumuaga na kutuonesha mfano wake ili tuufuate. Na kama ameishi na kumaliza maisha yake bila shirika kamili na Kristo kwa njia ya kanisa ambalo ni mwili wa huyo Kristo, kanisa linakataa kumzika ili kutuambia kwamba mfano wake siyo ufaao kuigwa.

Kwa nini ni muhimu Mkristo ashiriki maisha ya kanisa badala ya kuishi kivyakevyake tu?

Kwa sababu Kristo alitaka hivyo. Wakati anawaaga mitume wake na wanafunzi wake aliwataka WABAKI KATIKA UMOJA, NA WAKAE HIVYO HATA ROHO MTAKATIFU MZINDUZI RASMI WA KANISA AKIJA AWAKUTE WAKIWA PAMOJA NA WAMOJA.

Tutakumbuka hata sala ya Mwisho ya Bwana wetu Yesu Kristo kabla hajatiwa mikononi mwa wauaji aliwaombea wanafunzi wake WABAKI WAMOJA kama yeye na Baba walivyo MMOJA (Yohane 17:11).

Hivyo maisha ya ukristo ya kivyakovyako kwa kujitenga na kanisa Siyo mpango wa Kristo bali mpango wako binafsi. Siyo mfano tunaopaswa kuuiga wala kuuendekeza.

Kungia mbinguni kuurithi uzima wa milele kunamdai mtu atimize masharti makuu mawili (Luka 10:25-28):

1. Mapendo kwa Mungu
2. Mapendo kwa jirani.

Lakini huwezi kumpenda Mungu nusunusu. Yaani ukampenda kichwa na ukamchukia mwili. Kama kanisa ni mwili wa Kristo, wawezaje kusema unampenda Yesu (Mungu nafsi ya pili) na bado huna muda na mwili wake yaani kanisa lake? Mnafiki wewe.....!

Na kama hukumpenda Mungu (kichwa na mwili) na hukumpenda jirani, utawezaje kuurithi uzima wa milele? Ni vigumu.

Ni vema kujitahidi kuiepuka njia hiyo, ndiyo maana kanisa linautumia msiba kutukumbusha njia njema na kutuonya juu ya njia isiyo njema.

Kumbuka Yesu alisema atakayemkiri yeye Yesu (ambaye kanisa ni mwili wake) mbele za watu, Yesu pia atamkiri mbele ya baba, na atakayemkana Yesu mbele za watu Yesu pia atamkana yeye mbele ya Baba yake wa Mbinguni atakapofika mbele ya kiti cha utukufu wa Mungu (Mathayo 10:32-33).

Mfano wa taratibu za ki-kanisa ambazo ukijitenga nazo siyo rahisi kuupata uzima wa milele ni huu:

Ukiuishi ukristo wako peke yako nyumbani mwako huna nafasi ya kushiriki EKARISTI TAKATIFU au kwa maneno mengine KOMUNYO au wengine wanaita CHAKULA CHA BWANA au wengine wanaita MKATE WA BWANA.

Lakini Yesu mwenyewe alisema:

" Kweli nawaambieni, Msipokula huu mwili wangu na kuinywa damu yangu, hamtakuwa na uzima ndani yenu. Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu, anao uzima wa milele. Nami nitamfufua siku ya mwisho"

Yohane 6:53-54

Zingatia vizuri hayo maneno ya mwanzo niliyoya-bold. Yesu anaanza kwa kusisitiza akisema "Kweli nawaambieni,..

Kwa nini Yesu alisisitiza?

Kwa sababu alijua kuna wengi watapuuzia suala la kukomunika (kushiriki chakula cha Bwana) wakidhani watakuwa na uzima wa milele kwa kuishi tu majumbani kwao bila kuja kanisani ambako ndiko chakula hicho hutolewa, wakijidanganya kwamba maadam waliishabatizwa (na wengine walibatizwa kwa maji mengi ya mto wote au bahari nzima) basi hiyo inatosha kwa wao kuurithi uzima wa milele.

Pia alijua wapo ambao wanaweza kuwa wanasali na kutoa sadaka kubwakubwa lakini wanaishi maisha yanayowafanya wasistahili kushiriki chakula cha Bwana, wakidhani ni rahisi kuupata uzima wa milele bila chakula hicho.

By the way..., hatuokolewi kwa matendo yetu. Tunaokolewa kwa neema (Waefeso 5:2).

Neema ya Mungu (yaani uwepo wa Yesu Kristo katika maisha na mazingira ya mwanadamu) haipatikani katika kujitenga wewe binafsi, bali inapatikana kwa kuungana na wenzako kwa jina la Yesu.

Yeye mwenyewe alisema:

"Wakutanikapo wawili watatu kwa jina langu, mimi nipo hapo kati yao"

Mathayo. 18:20.

Na kama Yesu yupo katikati ya walio na umoja/ushirika katika yeye, basi neema ya Mungu inapatikana katika ushirika huo na siyo katika ubinafsi na kujitenga. Na kwa kuwa tunaokolewa kwa neema, ni rahisi zaidi kuokolewa tukiwa ndani ya kanisa kuliko kuokolewa tukiwa tumejitenga na mambo ya kanisa.

Kwa hiyo ndugu yangu..., ni muhimu sana kushiriki mambo ya kanisa. Na ni muhimu sana kwa kanisa kuonesha shukrani nanpongezi (appreciation) kwa yule anayekufa katika ushirika na kanisa, na kuonesha kuhuzunishwa na yule anayekufa akiwa hana shirika na kanisa.

Neno la Mungu linasema "Heri watu ambao wanakufa wakiwa wameungana na Bwana. Naam, watapumzika kutoka katika taabu zao, maana matunda ya jasho lao yatawafuata" (Ufunuo 14:13).

Mstari huo wa mwisho kunukuu ni muhimu sana kwako ndugu yangu. Kwamba ukifa umetengana na Bwana kwa matendo yoyote ikiwemo kutengana na mwili wa Bwana Yesu (Kanisa lake) una ole. Na ukifa ukiwa umeungana naye kwa matendo yoyote ikiwemo kuungana na mwili wa Bwama Yesu (Kanisa lake) una heri. Na amemalizia kwa kusema "matendo yako yataambatana nawe" hata baada ya kufa. Ndiyo maana umekufa, lakini sifa za jitihada za jasho lako tunazihubiri hata wakati wa mazishi yako. Na kinyume chake, sifa mbaya ulizoacha tunazikana hata baada ya kufa kwako kwa kuyakana mazishi yako.

Tumsifu Yesu Kristo.
Wengine tuliamua kulitenga kanisa kabla kanisa halijatutenga.

Hatutaki ujinga wa kutishiwa nyau.
 
Kanisa katoliki linaishi kwa vitisho and in darkness
Ndoa takatifu ?
Kwa hiyi wanaofunga ndoa kwa padri/mchungaji au kadinal ndoa zao ndiyo takatifu ?
Je Isaac alipoenda kuoa Rabeca je kylikuwa na mchungaji/kuhani gani ?(ilo neno limetoka kifungu gani ?)

umesema lengo la kwenda kumzika marehemu ni kwa ajili ta kuwakumbusha waliobaki … . Sasa ni kwanini hamkwenda kuwakumbusha waliyobaki kwenye msiba wa marehemu Mrema ?
Ni lazima taratibu za kanisa ziendane na maandiko au neno la Mungu (je, kuogopa sheria za kanisa kuliko neno ka Mungu hauoni ni hatari kwa afya yako kiroho ?)
 
Halafu kwa matendo yao kama hayo bado wanazikwa kwa ibada maalumu as if walistahili hivyo kuliko Mrema
Kweli ndugu, siku hizi hawa viongozi wako after money (ndiyo maana makesi ya dini yamekuwa mengi mdano wakina mokiwa, wale wa escrow na benk ya kanisa lao), pia viongoz hawa nao wanamakashfa mfano kulawiti watoto kutokana na sheria za kanisa kutoruhusu wao kuoa kisha ashki zao kumalizia kwa watoto wadogo wasiyo na hatialakini hatuwahukumu.
Pia , viongozi wengi wanapenda kuwa kama mafirisayo
 
Me sioni unachokitetetea hapa mkuu/hovyo kweli wewe
Lengo la ujumbe ni kutoa ufafanuzi wa taratibu za Kikatoliki....kama wewe sio mkatoliki hutakaa uelewe na kimsingi ni utaratibu unaofahamika na kila mkatoliki sasa sijui wengine nini kinawagusa hapo. Tatizo ni kuta ku rahisisha na ku liberalize masuala ya Imani jambo ambalo kamwe sio kwa Kanisa Katoliki. Wale wenye kukurupuka na kuzika watu wa aina hiyo waendelee tu sababu utaratibu wao unaruhusu kwani hawana taratibu za kiendesha imani zao. Kanisa katoliki sio kikundi cha kuyumba na muamua utakavyo... Ni taasisi imara yenye utaratibu unaoheshimika kwa wakatoliki
 
Huo ni utaratibu usiokuwa na mashiko kabisa, kama utaratibu huo uliwekwa ili kuwakumbusha watu wanaobakia juu ya ushiriki wao wa kanisa, basi huyo aliyeleta utaratibu huo wa ajabu hakufikiria mbali. unapokataa kumzika marehemu na kutomsomea misa haumkomoi huyu marehemu, maana wafu hawasikii lolote bali unawakomoa ndugu na jamaa ambao wanabaki, kuna matukio kama haya yamewafanya waumini wengi kujitenga na kanisa. Kwa mtazamo wangu sioni mantiki yoyote ya kumuumiza mtu kihisia kwa makosa ambayo hakuyafanya kutomsomea misa marehemu uleta simanzi kwa ndugu na jamaa, kila muumini anapenda kuona mpendwa wake amesomewa misa ya mazishi, kukataa kusoma misa kwa sababu yoyote ile kunaleta uchungu na hasira, je kuwaudhi wengine ni mpango wa Mungu?

Pengine ninaweza kuwa sifahamu biblia vizuri ila hakika naamini hata Yesu mwenyewe akuagiza watu wabaguane kwa namna yoyote ile sasa huu ubaguzi naona ni kama mpango wa shetani, tunaweza kuwa tunajiuliza shetani anafananaje lakini tunasahau matendo yetu maovu ndio shetani mwenyewe, kuumiza hisia za wengine nao ni ushetani, lakini ubaguzi nao ni ushetani wa hali ya juu. Adhabu ya kutosomewa misa nayo imekaa kibaguzi kibaguzi na kiunafiki, mara nyingi adhabu au utaratibu huu ulenga baadhi ya makosa tu ila sio yote tujiulize kwanini sio yote, inafurahisha kuona Padri anakataa kumsomea marehemu misa kisa tu marehemu hakuwa na ndoa ya kikatoliki wakati wa uhai wake, lakini Padri huyo huyo anakuwa mstari wa mbele kusoma misa ya mazishi kwa ajili ya muumini aliyekuwa na ndoa ila alikuwa jambazi, mfitinishaji au yule aliyekuwa na vimada kila kona. Sasa tujiulize je Mungu uangalia dhambi kwa uzito tofauti? naamini jibu ni hapana kama ni hivyo mamlaka ya kuwahukumu wengine tunayatoa wapi? Je tunatofauti gani na yule aonaye kibanzi ndani ya jicho la mwezake wakati yeye ana bolt?

1 Yohana 1: 8-10
, inasema tukisema hatuna dhambi twajidanganya wenyewe, wala kweli haimo ndani yetu, kwa mantiki hii ni nani aliye chini ya jua ambaye hana dhambi? kama hakuna kwanini tunahukumu wengine! 1 petro 2, 1-10 inatueleze kuwa tuache maovu yetu yote ikiwemo unafiki, ni unafiki wa hali ya juu kukataa kumsomea marehemu misa kwa madai kuwa alikuwa ana ndoa ya kikanisa, mzinzi au kwa sababu ya kujitoa uhai wake wenyewe, swali la kujiuliza mbona wakati yu hai pesa zake za sadaka na michango mingine ilikuwa inapokelewa! tena bila zengwe wala maswali, yaani hii sawa na kusema mtini mbaya umezaa matunda mazuri, eti licha ya kuwa mdhambi kipindi cha uhai wake pesa zake ni nzuri tu ila akiondoka yeye anakuwa mbaya. Acheni unafiki, narudia tena acheni unafiki kwa kuleta sheria za kijinga kutoka katika vichwa vyetu, sheria ambazo hazina lile pendo tuliloachiwa, ambazo haziangali ndugu wanaobaki watajisikia vipi, nina uhakika maelefu ya watu wamejitenga na kanisa na kuwa wapagani kabisa kwa sababu ya hasira juu ya sheria au taratibu hizi, je tunajua adhabu ya yule awapotezaye wengine?

Mwisho kabisa namalizia kwa kusema, tufuate zile amri tulizoachiwa ambazo zina huruma, msamaha na pendo la kweli ndani yake na tuachane na taratibu au sheria za kanisa zilizojaa ubaguzi na unafiki, Mungu hapendi unafiki. Sheria au taratibu za kanisa zimeletwa na wanaadamu, tunatakiwa kuzingatia kuwa sio kila linaloletwa na watunga taratibu hizo ni sahihi maana nao ni dhaifu kama sisi, tunapoona uwalakini, tukumbushane na tujirekebishe, kama tunaweza kubadili baadhi ya sala, tunashindwa nini kubadili utaratibu huu wa kizindaki, kipuuzi ulijaa unafiki!​
 
Bahati mbaya Afrika hii ndo sehemu pekee unakuta Padri analawiti mtoto halafu anaachiwa na kufichwa Vatican. Huko Ulaya sasa wanawachomoa kwa kesi za miaka mingi na kuwatia kibano. Walawiti hawa!
 
Back
Top Bottom