Ufafanuzi kuhusu kanisa Katoliki kutokuwafanyia maziko ya kikanisa baadhi ya waamini wake

Ufafanuzi kuhusu kanisa Katoliki kutokuwafanyia maziko ya kikanisa baadhi ya waamini wake

N
Je, hao mapadri na makardinali wenye hizo kashfa kanisa litakataa kuwazika au kwa sababu wanashiriki kanisani hayo madhambi hayawezi kuwatenga na kanisa?
Diyo maana nimesema waache ubaguzi kwani kila mtu ana mapungufu yake uwe askofu ,.mchungaji sheik au papaa, pia nyumba za ibada (kanisa , msikiti au hekalu vinapadwa kuwa chanzo cha upendo na msamaha na si ubaguzi)
 
Ukweli ni kwamba dini imekuwa biashara kila cku sharia na kanuni mpya zinatungwa ili kuwanufaisha wachungaji tangu lini maneno ya mungu yawe yanabadilibadilika kama cyo uhuni Wa kupiga hela.
Unaacha kumzika mwenzako kisa ndoa???? Wao wanafanya mangapi ya uchafu na masister??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lengo la ujumbe ni kutoa ufafanuzi wa taratibu za Kikatoliki....kama wewe sio mkatoliki hutakaa uelewe na kimsingi ni utaratibu unaofahamika na kila mkatoliki sasa sijui wengine nini kinawagusa hapo. Tatizo ni kuta ku rahisisha na ku liberalize masuala ya Imani jambo ambalo kamwe sio kwa Kanisa Katoliki. Wale wenye kukurupuka na kuzika watu wa aina hiyo waendelee tu sababu utaratibu wao unaruhusu kwani hawana taratibu za kiendesha imani zao. Kanisa katoliki sio kikundi cha kuyumba na muamua utakavyo... Ni taasisi imara yenye utaratibu unaoheshimika kwa wakatoliki
Hakuna kitu kanisa katoliki halina tofauti na makanisa tene afadhali makanisa mengine wako wazi, mapadre wengi wa kanisa katoliki wanamiliki wanawake huku mitaana na kuwafanyia mambo makubwa kama vile kuwajengea majumba na kuwanunulia magari. usalama wa binadamu ni mapenzi yake tu lakini kwa kupitia makanisa ni sifuri kabisa.
 
Lengo la ujumbe ni kutoa ufafanuzi wa taratibu za Kikatoliki....kama wewe sio mkatoliki hutakaa uelewe na kimsingi ni utaratibu unaofahamika na kila mkatoliki sasa sijui wengine nini kinawagusa hapo. Tatizo ni kuta ku rahisisha na ku liberalize masuala ya Imani jambo ambalo kamwe sio kwa Kanisa Katoliki. Wale wenye kukurupuka na kuzika watu wa aina hiyo waendelee tu sababu utaratibu wao unaruhusu kwani hawana taratibu za kiendesha imani zao. Kanisa katoliki sio kikundi cha kuyumba na muamua utakavyo... Ni taasisi imara yenye utaratibu unaoheshimika kwa wakatoliki
Ya roho ayajua roho n.a. ya mwili ayajua mwili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi kwa nini Yesu alikua mzungu/mweupe na mtume alikua mwarabu/mweupe?? Mi sielewi kwa kweli niambieni
 
UFAFANUZI KUHUSU KANISA KATOLIKI KUTOKUWAFANYIA MAZIKO YA KIKANISA BAADHI YA WAAMINI WAKE:

Jana mitandao ya kijamii nchini ilienea habari za kanisa kutokumzika tajiri mmoja kwa sababu alikufa katika hali ya "kinyumba" bila ndoa takatifu, na kwamba hakuwa mshiriki hai wa masuala ya kanisa.

Baada ya hapo kukatokea maneno mengi sana baadhi ya watu wakilishanbulia kanisa katoliki kwamba limekosea na linakosea kwa utaratibu huo, kwa maelezo mepesi kwamba suala la mtu kwenda mbinguni ni wajibu wa Mungu na siyo kazi ya kanisa kuhukumu (huenda wamesahau kwamba kanisa halijaihukumu roho ya marehemu bali limekataa kuuzika mwili wake tu ardhini).

Basi nimewiwa kufafanua kidogo niwezavyo kuhusu suala hili.

Karibu.......

Maziko ya kikanisa hayamfanyi mmoja aliyefariki aende mbinguni wala Jehanamu, bali yanamkumbusha mwombolezaji aliyebaki hai wajibu wake wa kuishi katika ushirika na kanisa ambalo ni mwili wa Kristo.

Kumzika au kutokumzika mtu kikanisa siyo jambo la kubeza ingawa ni kweli siyo linalompeleka marehemu mbinguni au motoni. Tukumbuke mwili wa marehemu unabaki ardhini. Kinachoenda mbinguni au motoni ni roho.

Lakini maziko ya kikanisa ni jambo lenye maana kubwa kutukumbusha tunaobaki duniani kwamba Kanisa ambalo ni mwili wa Kristo na ambalo Kristo mwenyewe ndiye kichwa chake *(Waefeso 5:23)* linataka waamini tuige mfano wa mwenzetu aliyeishi na kumaliza maisha yake akiwa na ushirika na kanisa, ndiyo maana linafanya maziko ya kikanisa kama sherehe ya kumpongeza, kumuaga na kutuonesha mfano wake ili tuufuate. Na kama ameishi na kumaliza maisha yake bila shirika kamili na Kristo kwa njia ya kanisa ambalo ni mwili wa huyo Kristo, kanisa linakataa kumzika ili kutuambia kwamba mfano wake siyo ufaao kuigwa.

*Kwa nini ni muhimu Mkristo ashiriki maisha ya kanisa badala ya kuishi kivyakevyake tu?*

Kwa sababu Kristo alitaka hivyo. Wakati anawaaga mitume wake na wanafunzi wake aliwataka WABAKI KATIKA UMOJA, NA WAKAE HIVYO HATA ROHO MTAKATIFU MZINDUZI RASMI WA KANISA AKIJA AWAKUTE WAKIWA PAMOJA NA WAMOJA.

Tutakumbuka hata sala ya Mwisho ya Bwana wetu Yesu Kristo kabla hajatiwa mikononi mwa wauaji aliwaombea wanafunzi wake WABAKI WAMOJA kama yeye na Baba walivyo MMOJA *(Yohane 17:11)*.

Hivyo maisha ya ukristo ya kivyakovyako kwa kujitenga na kanisa Siyo mpango wa Kristo bali mpango wako binafsi. Siyo mfano tunaopaswa kuuiga wala kuuendekeza.

Kungia mbinguni kuurithi uzima wa milele kunamdai mtu atimize masharti makuu mawili (Luka 10:25-28):

1. Mapendo kwa Mungu
2. Mapendo kwa jirani.

Lakini huwezi kumpenda Mungu nusunusu. Yaani ukampenda kichwa na ukamchukia mwili. Kama kanisa ni mwili wa Kristo, wawezaje kusema unampenda Yesu (Mungu nafsi ya pili) na bado huna muda na mwili wake yaani kanisa lake? Mnafiki wewe.....!

Na kama hukumpenda Mungu (kichwa na mwili) na hukumpenda jirani, utawezaje kuurithi uzima wa milele? Ni vigumu.

Ni vema kujitahidi kuiepuka njia hiyo, ndiyo maana kanisa linautumia msiba kutukumbusha njia njema na kutuonya juu ya njia isiyo njema.

Kumbuka Yesu alisema atakayemkiri yeye Yesu (ambaye kanisa ni mwili wake) mbele za watu, Yesu pia atamkiri mbele ya baba, na atakayemkana Yesu mbele za watu Yesu pia atamkana yeye mbele ya Baba yake wa Mbinguni atakapofika mbele ya kiti cha utukufu wa Mungu (Mathayo 10:32-33).

*Mfano wa taratibu za ki-kanisa ambazo ukijitenga nazo siyo rahisi kuupata uzima wa milele ni huu:*

Ukiuishi ukristo wako peke yako nyumbani mwako huna nafasi ya kushiriki EKARISTI TAKATIFU au kwa maneno mengine KOMUNYO au wengine wanaita CHAKULA CHA BWANA au wengine wanaita MKATE WA BWANA.

Lakini Yesu mwenyewe alisema:

" *Kweli nawaambieni,* Msipokula huu mwili wangu na kuinywa damu yangu, hamtakuwa na uzima ndani yenu. Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu, anao uzima wa milele. Nami nitamfufua siku ya mwisho"

*Yohane 6:53-54*

Zingatia vizuri hayo maneno ya mwanzo niliyoya-bold. Yesu anaanza kwa kusisitiza akisema *"Kweli nawaambieni,..*

Kwa nini Yesu alisisitiza?

Kwa sababu alijua kuna wengi watapuuzia suala la kukomunika (kushiriki chakula cha Bwana) wakidhani watakuwa na uzima wa milele kwa kuishi tu majumbani kwao bila kuja kanisani ambako ndiko chakula hicho hutolewa, wakijidanganya kwamba maadam waliishabatizwa (na wengine walibatizwa kwa maji mengi ya mto wote au bahari nzima) basi hiyo inatosha kwa wao kuurithi uzima wa milele.

Pia alijua wapo ambao wanaweza kuwa wanasali na kutoa sadaka kubwakubwa lakini wanaishi maisha yanayowafanya wasistahili kushiriki chakula cha Bwana, wakidhani ni rahisi kuupata uzima wa milele bila chakula hicho.

By the way..., hatuokolewi kwa matendo yetu. Tunaokolewa kwa neema (Waefeso 5:2).

Neema ya Mungu (yaani uwepo wa Yesu Kristo katika maisha na mazingira ya mwanadamu) haipatikani katika kujitenga wewe binafsi, bali inapatikana kwa kuungana na wenzako kwa jina la Yesu.

Yeye mwenyewe alisema:

"Wakutanikapo wawili watatu kwa jina langu, mimi nipo hapo kati yao"

Mathayo. 18:20.

Na kama Yesu yupo katikati ya walio na umoja/ushirika katika yeye, basi neema ya Mungu inapatikana katika ushirika huo na siyo katika ubinafsi na kujitenga. Na kwa kuwa tunaokolewa kwa neema, ni rahisi zaidi kuokolewa tukiwa ndani ya kanisa kuliko kuokolewa tukiwa tumejitenga na mambo ya kanisa.

Kwa hiyo ndugu yangu..., ni muhimu sana kushiriki mambo ya kanisa. Na ni muhimu sana kwa kanisa kuonesha shukrani nanpongezi (appreciation) kwa yule anayekufa katika ushirika na kanisa, na kuonesha kuhuzunishwa na yule anayekufa akiwa hana shirika na kanisa.

Neno la Mungu linasema "Heri watu ambao wanakufa wakiwa wameungana na Bwana. Naam, watapumzika kutoka katika taabu zao, maana matunda ya jasho lao yatawafuata" (Ufunuo 14:13).

Mstari huo wa mwisho kunukuu ni muhimu sana kwako ndugu yangu. Kwamba ukifa umetengana na Bwana kwa matendo yoyote ikiwemo kutengana na mwili wa Bwana Yesu (Kanisa lake) una ole. Na ukifa ukiwa umeungana naye kwa matendo yoyote ikiwemo kuungana na mwili wa Bwama Yesu (Kanisa lake) una heri. Na amemalizia kwa kusema "matendo yako yataambatana nawe" hata baada ya kufa. Ndiyo maana umekufa, lakini sifa za jitihada za jasho lako tunazihubiri hata wakati wa mazishi yako. Na kinyume chake, sifa mbaya ulizoacha tunazikana hata baada ya kufa kwako kwa kuyakana mazishi yako.

Tumsifu Yesu Kristo.
Kanisa la Katholiki ni "an Institution" tu kam vile club ya Yanga au Simba. Ukiwa member watakujali kama myenendo yako inaenda na maadili ya hiyo member wenig was hiyo institution. Kama sio member kwanini ikuthamini na kukujali?

Nasema hivi kwa sababu kanisa halijaumbwa na mungu isipokuwa ia " a man made model of life". Kwa namna hiyo member wake lazima wawe na "Emotion" kwa sababu ni binadam. Ni kipaji au tuseme mwenendo ambao tumepewa na muumba. Lazima liyakatae baadhi ya matendo ya watu kwa sababu ni nature ya binadam kutokubaliana na baadhi ya mambo ambayo hayaendani na aadili ya majority ya kanisa. Ni kawaida!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante sana kwa hili somo. Wapo wengi waliopinga bila kujua. Baadhi yao ni Wakatoliki. Nawashauri kwamba ni vema kuwa humble na kufuata mafundisho ya Kanisa.
 
Asante.

Naomba twende taratibu...

Nabaki kwenye katazo,biblia kupitia kupitia agano la kale ilikataza aina nyingi ya viumbe wasiliwe kwa kuwa ni najisi mfn,Sungura,Ngamia,Nguruwe nk pia baadhi ya samaki wasio na magamba kama Kambale nk na ndege wa angani kama Tai nk,kwa ufafanuzi pitia Walawi 11:1-14

Swali;Ninyi mnaokataa kula nyama ya Nguruwe kwa mujibu wa biblia,Je Sungura,Ngamia pia mnawakataa...???Vp samaki wasio na magamba(Kambale)..????

Naomba tubaki kwenye Katazo(Torati) kwanza alafu tuendelee.

Sent using Jamii Forums mobile app
Swali lako ni rahisi sana jibu lake hatuli tulivyokatazwa na tunatimiliza amri...

Hakuna sheria rahisi kama ya mtu kuzuiliwa kula chakula aina furani it's very simple.. ila ubishi tu wa watu na sikuhizi hadi muambiwe na daktari msile hiki na hiki na kile mnafuata
 
Amri ipi mkuu..??? Me naongea kupitia maandiko na wala sio ushauri wowote toka duniani,I mean doctor/nurse/witchdoctor or whoever...!!!

Naomba turudi kwenye biblia tena agano la kale ambalo lilikataza.

Nimejikita kwenye KATAZO kwanza ili nikupe elimu.

Usikimbie tafadhali....

Nakusubiri.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Swali lako ni rahisi sana jibu lake hatuli tulivyokatazwa na tunatimiliza amri...

Hakuna sheria rahisi kama ya mtu kuzuiliwa kula chakula aina furani it's very simple.. ila ubishi tu wa watu na sikuhizi hadi muambiwe na daktari msile hiki na hiki na kile mnafuata
Na Luna maswali hapo juu hujanijibu....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maelezo yaliyotolewa hpo mbona sioni msingi wowote wa kiimani zaidi tu ya kisasi na kukomoana kwamba eti kwa kua alikua hajatimiza baadhi ya vifungu Fulani basi kanisa nalo linagoma kutoa huduma kwake, enyi mafarisayo wanafiki. Yule mwanamke aliekamatwa akizini alipofikishwa mbele ya Kristo Ili ahukumiwe Kristo alijua dhahiri kua sheria iliruhusu yeye kupigwa mawe ila alichora kwa kidole chake chini kua asiekua na dhambi na awe wa kwanza kumpiga mawe ila hakurusha jiwe hata mmoja hta wale waliojiita makuhani watakatifu. Kanisa kugoma kumzika mtu kisa hakua na ndoa ya kihalali huku kanisa hilohilo likiwa na kashfa za kulawiti watoto wadogo wanaotumikia madhabahuni ni unafiki suala linalojulikana dunia nzima ni unafiki uliopita kiwango. Kufanya hvyo c utakatifu na wala hamtojisafisha uovu wenu duniani kwa kugoma kuwazika walio na mapungufu kwa sababu ninyi wenyewe hamjakamilika na matendo yenu yanadhihirisha sura halisi iliyopo kwenu

Mkuu sijajua wewe kama ulishawahi kupitia/uko ktk Imani gani..???hicho unachonukuhu kwa Yesu sidhani kama kina-reflect unachotaka ku-expose hapa.

Pengine ujipange upya ili U- translate ulichonacho.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi ule mstari wa ''samehe saba mara sabini'' hautumiki hapa? Au huu mazingira yake ni pale mtu akiwa hai? Je, Bibilia inatumika tofauti katika mazingira tofauti? Je, kwa uweza wa Mungu mazingira yanatumika?
 
hajahukumiwa anaeyehukumu ni mungu,ila marehem kajitenga na kanisa na hata wana jumuiya wenzake wanajua,lazima tuishi kwa utaratibu,kila sehemu kuna utaratibu wake,hata nyumbani kwako unaweka utaratibu wa kuendesha familia,kwenye masuala ya imani tusililaumu kanisa katoliki ndo maana imani ni yako waweza hama ukaamia kwa lusekelo,gwajima,rwakatale na ukiona ukristo/ukristu hauna tija hamia kwa waislamu au buddha au hindu nk,
rais wa urusi mara nyingi wapinzani wake na wahamiaji wa urusi wamekuwa wakililia haki na favour inayopata kanisa la orthodox wakitaka nao imani zao zipewe hizo feva,putin aliwahi kusema mtu anayeuliza au kuhoji utaratibu wa urusi na kanisa la orthodox na waorthodox ni punguani kwa kuwa hata huko kwako kuna utaratibu na unaheshimika na wa upande huo na waarusi hawawezi kuhoji wala kujisumbua kwa nini iwe ivyo,kwa kua ni maamuzi yao na ni asili yao,na sisi wa nje hatupaswi kuuliza ni mungu yupi kaamlisha haya kwa kuwa wote ni binadamu na tuna machaguzi
Ninacho uliza ni "wewe ni nani kujiona mkamilifu mubashara na kumuona mwingine si mkamilifu,nani kakupa mamlaka ya kuhukumu...
Je wanadam wote tu na safari moja..(kufa)
Iweje leo tufikie mahali tu hukumu...
Tukumbuke hata Yesu alipokuwa Msalabani mda mfupi kabla ya kukata Roho alimwambia mmoja wa mwizi aliyekuwa naye pale Msalabani (jion ya leo utakuwa nami kwa baba yangu)
Who are you to judge.....????
 
hajahukumiwa anaeyehukumu ni mungu,ila marehem kajitenga na kanisa na hata wana jumuiya wenzake wanajua,lazima tuishi kwa utaratibu,kila sehemu kuna utaratibu wake,hata nyumbani kwako unaweka utaratibu wa kuendesha familia,kwenye masuala ya imani tusililaumu kanisa katoliki ndo maana imani ni yako waweza hama ukaamia kwa lusekelo,gwajima,rwakatale na ukiona ukristo/ukristu hauna tija hamia kwa waislamu au buddha au hindu nk,
rais wa urusi mara nyingi wapinzani wake na wahamiaji wa urusi wamekuwa wakililia haki na favour inayopata kanisa la orthodox wakitaka nao imani zao zipewe hizo feva,putin aliwahi kusema mtu anayeuliza au kuhoji utaratibu wa urusi na kanisa la orthodox na waorthodox ni punguani kwa kuwa hata huko kwako kuna utaratibu na unaheshimika na wa upande huo na waarusi hawawezi kuhoji wala kujisumbua kwa nini iwe ivyo,kwa kua ni maamuzi yao na ni asili yao,na sisi wa nje hatupaswi kuuliza ni mungu yupi kaamlisha haya kwa kuwa wote ni binadamu na tuna machaguzi
Mkuu hawa watu hawajielewi,wameng'ang'ani HUKUMU..!!!ukiwauliza wapi au nani ametoa hiyo hukumu wanakimbia hawasikiki,

Kuna mmoja nimemkita maswali naona amekimbia..!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom