Ufafanuzi kuhusu kanisa Katoliki kutokuwafanyia maziko ya kikanisa baadhi ya waamini wake

Utaratibu unatoka kwa paroko au kwenye Biblia? Acheni kupoteza watu..

Utaratibu unaouzungumzia wewe ni upi kwani mkuu?, mi nataka kujua utaratibu wa kujiunga na kanisa la katoliki, nafikiri hata madhehebu mengine pia yana taratibu zao
 
*_Anaandika Bernard Mukasa_*

UFAFANUZI KUHUSU KANISA KATOLIKI KUTOKUWAFANYIA MAZIKO YA KIKANISA BAADHI YA WAAMINI WAKE:

Jana mitandao ya kijamii nchini ilienea habari za kanisa kutokumzika tajiri mmoja kwa sababu alikufa katika hali ya "kinyumba" bila ndoa takatifu, na kwamba hakuwa mshiriki hai wa masuala ya kanisa.

Baada ya hapo kukatokea maneno mengi sana baadhi ya watu wakilishanbulia kanisa katoliki kwamba limekosea na linakosea kwa utaratibu huo, kwa maelezo mepesi kwamba suala la mtu kwenda mbinguni ni wajibu wa Mungu na siyo kazi ya kanisa kuhukumu (huenda wamesahau kwamba kanisa halijaihukumu roho ya marehemu bali limekataa kuuzika mwili wake tu ardhini).

Basi nimewiwa kufafanua kidogo niwezavyo kuhusu suala hili.

Karibu.......

Maziko ya kikanisa hayamfanyi mmoja aliyefariki aende mbinguni wala Jehanamu, bali yanamkumbusha mwombolezaji aliyebaki hai wajibu wake wa kuishi katika ushirika na kanisa ambalo ni mwili wa Kristo.

Kumzika au kutokumzika mtu kikanisa siyo jambo la kubeza ingawa ni kweli siyo linalompeleka marehemu mbinguni au motoni. Tukumbuke mwili wa marehemu unabaki ardhini. Kinachoenda mbinguni au motoni ni roho.

Lakini maziko ya kikanisa ni jambo lenye maana kubwa kutukumbusha tunaobaki duniani kwamba Kanisa ambalo ni mwili wa Kristo na ambalo Kristo mwenyewe ndiye kichwa chake *(Waefeso 5:23)* linataka waamini tuige mfano wa mwenzetu aliyeishi na kumaliza maisha yake akiwa na ushirika na kanisa, ndiyo maana linafanya maziko ya kikanisa kama sherehe ya kumpongeza, kumuaga na kutuonesha mfano wake ili tuufuate. Na kama ameishi na kumaliza maisha yake bila shirika kamili na Kristo kwa njia ya kanisa ambalo ni mwili wa huyo Kristo, kanisa linakataa kumzika ili kutuambia kwamba mfano wake siyo ufaao kuigwa.

*Kwa nini ni muhimu Mkristo ashiriki maisha ya kanisa badala ya kuishi kivyakevyake tu?*

Kwa sababu Kristo alitaka hivyo. Wakati anawaaga mitume wake na wanafunzi wake aliwataka WABAKI KATIKA UMOJA, NA WAKAE HIVYO HATA ROHO MTAKATIFU MZINDUZI RASMI WA KANISA AKIJA AWAKUTE WAKIWA PAMOJA NA WAMOJA.

Tutakumbuka hata sala ya Mwisho ya Bwana wetu Yesu Kristo kabla hajatiwa mikononi mwa wauaji aliwaombea wanafunzi wake WABAKI WAMOJA kama yeye na Baba walivyo MMOJA *(Yohane 17:11)*.

Hivyo maisha ya ukristo ya kivyakovyako kwa kujitenga na kanisa Siyo mpango wa Kristo bali mpango wako binafsi. Siyo mfano tunaopaswa kuuiga wala kuuendekeza.

Kungia mbinguni kuurithi uzima wa milele kunamdai mtu atimize masharti makuu mawili (Luka 10:25-28):

1. Mapendo kwa Mungu
2. Mapendo kwa jirani.

Lakini huwezi kumpenda Mungu nusunusu. Yaani ukampenda kichwa na ukamchukia mwili. Kama kanisa ni mwili wa Kristo, wawezaje kusema unampenda Yesu (Mungu nafsi ya pili) na bado huna muda na mwili wake yaani kanisa lake? Mnafiki wewe.....!

Na kama hukumpenda Mungu (kichwa na mwili) na hukumpenda jirani, utawezaje kuurithi uzima wa milele? Ni vigumu.

Ni vema kujitahidi kuiepuka njia hiyo, ndiyo maana kanisa linautumia msiba kutukumbusha njia njema na kutuonya juu ya njia isiyo njema.

Kumbuka Yesu alisema atakayemkiri yeye Yesu (ambaye kanisa ni mwili wake) mbele za watu, Yesu pia atamkiri mbele ya baba, na atakayemkana Yesu mbele za watu Yesu pia atamkana yeye mbele ya Baba yake wa Mbinguni atakapofika mbele ya kiti cha utukufu wa Mungu (Mathayo 10:32-33).

*Mfano wa taratibu za ki-kanisa ambazo ukijitenga nazo siyo rahisi kuupata uzima wa milele ni huu:*

Ukiuishi ukristo wako peke yako nyumbani mwako huna nafasi ya kushiriki EKARISTI TAKATIFU au kwa maneno mengine KOMUNYO au wengine wanaita CHAKULA CHA BWANA au wengine wanaita MKATE WA BWANA.

Lakini Yesu mwenyewe alisema:

" *Kweli nawaambieni,* Msipokula huu mwili wangu na kuinywa damu yangu, hamtakuwa na uzima ndani yenu. Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu, anao uzima wa milele. Nami nitamfufua siku ya mwisho"

*Yohane 6:53-54*

Zingatia vizuri hayo maneno ya mwanzo niliyoya-bold. Yesu anaanza kwa kusisitiza akisema *"Kweli nawaambieni,..*

Kwa nini Yesu alisisitiza?

Kwa sababu alijua kuna wengi watapuuzia suala la kukomunika (kushiriki chakula cha Bwana) wakidhani watakuwa na uzima wa milele kwa kuishi tu majumbani kwao bila kuja kanisani ambako ndiko chakula hicho hutolewa, wakijidanganya kwamba maadam waliishabatizwa (na wengine walibatizwa kwa maji mengi ya mto wote au bahari nzima) basi hiyo inatosha kwa wao kuurithi uzima wa milele.

Pia alijua wapo ambao wanaweza kuwa wanasali na kutoa sadaka kubwakubwa lakini wanaishi maisha yanayowafanya wasistahili kushiriki chakula cha Bwana, wakidhani ni rahisi kuupata uzima wa milele bila chakula hicho.

By the way..., hatuokolewi kwa matendo yetu. Tunaokolewa kwa neema (Waefeso 5:2).

Neema ya Mungu (yaani uwepo wa Yesu Kristo katika maisha na mazingira ya mwanadamu) haipatikani katika kujitenga wewe binafsi, bali inapatikana kwa kuungana na wenzako kwa jina la Yesu.

Yeye mwenyewe alisema:

"Wakutanikapo wawili watatu kwa jina langu, mimi nipo hapo kati yao"

Mathayo. 18:20.

Na kama Yesu yupo katikati ya walio na umoja/ushirika katika yeye, basi neema ya Mungu inapatikana katika ushirika huo na siyo katika ubinafsi na kujitenga. Na kwa kuwa tunaokolewa kwa neema, ni rahisi zaidi kuokolewa tukiwa ndani ya kanisa kuliko kuokolewa tukiwa tumejitenga na mambo ya kanisa.

Kwa hiyo ndugu yangu..., ni muhimu sana kushiriki mambo ya kanisa. Na ni muhimu sana kwa kanisa kuonesha shukrani nanpongezi (appreciation) kwa yule anayekufa katika ushirika na kanisa, na kuonesha kuhuzunishwa na yule anayekufa akiwa hana shirika na kanisa.

Neno la Mungu linasema "Heri watu ambao wanakufa wakiwa wameungana na Bwana. Naam, watapumzika kutoka katika taabu zao, maana matunda ya jasho lao yatawafuata" (Ufunuo 14:13).

Mstari huo wa mwisho kunukuu ni muhimu sana kwako ndugu yangu. Kwamba ukifa umetengana na Bwana kwa matendo yoyote ikiwemo kutengana na mwili wa Bwana Yesu (Kanisa lake) una ole. Na ukifa ukiwa umeungana naye kwa matendo yoyote ikiwemo kuungana na mwili wa Bwama Yesu (Kanisa lake) una heri. Na amemalizia kwa kusema "matendo yako yataambatana nawe" hata baada ya kufa. Ndiyo maana umekufa, lakini sifa za jitihada za jasho lako tunazihubiri hata wakati wa mazishi yako. Na kinyume chake, sifa mbaya ulizoacha tunazikana hata baada ya kufa kwako kwa kuyakana mazishi yako.

Tumsifu Yesu Kristo.

Ben Mukasa.
hili ndio kanisa pekee lililopotea, na lisilojua hata linakokwenda. wakatoliki mpokeeni Yesu awe Bwana na mwokozi wa maisha yenu, muokoke la sivyo moto wa milele unawasubiri. huwa nakereka nikihudhuria misiba yenu, unakuta padre aliyesoma miaka mingi dini, hajui hata anachokihubiri, mmesoma Bible lakini hamtakuja kuielewa na haitakuja kuwasaidia. mmebaki tu kama NGO na sio sehemu ya kusaidia watu kwenda mbinguni.
 
Huyo Bernard Mukasa kaandika kwa utashi wake na kuchagiza kile anachokiamini kwa nukuu za Biblia...

Ukweli ni kwamba mwanadamu akifa huzikwa kwa kuzingatia taratibu za kijamii (inaweza ikawa kidini, kiserikali, kimila n.k)...

Sasa kwa mantiki hiyo, kanisa linalokataa kuongoza ibada ya kuzika mwili uliokufa, huo ni utaratibu wa hilo kanisa na wala usiusishwe na kipengele au nukuu yoyote katika biblia...

Biblia inaeleza amri moja tu juu ya mtu mfu, nayo ni kuwa mavumbini atarudi kwa kuwa katoka huko...period!!

Kanisa lisijifiche nyuma ya kisingizio kuwa mazishi ni sehemu ya kutoa mahubiri juu ya kuishi maisha matakatifu duniani, la sivyo basi kanisa katoliki lisingelikuwa na ile sala ya kuombea wafu...
mkuu umeleza vema kabisa utaratibu wa jamii fulani au kanisa fulani, pia ikumbukwe hukum itaanzia kanisania kwa sababu kanisa sometimes hutumia uwezo lilopewa vibaya
 
Ben hongera kwa ufafanuzi mzuri kwanini kama mtu alilikataa kanisa akiwa hai nyie mumlazimishe kuzikwa nalo angeweza kuzungumza bado angekataa mwacheni aende kwa maisha aliyochagua Tumsifu Yesu Kristo .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata Cain akimzika Abel bila kanisa Na Mungu akampokea...

Kama ni mkristo mlimsajili kwa ubatizo hakuja futio so anabakia na Ukristo wake nyie wajaa dhambi hamna nafasi ya kuhukumu... jiulize watu wote wafe duniani wazikwe and then ukibakia wewe peke yako ukafa nani atakuzika?
hahahah nawe umekuwa Yesu sasa kujua mdhambi ni nani??
 
*_Anaandika Bernard Mukasa_*

UFAFANUZI KUHUSU KANISA KATOLIKI KUTOKUWAFANYIA MAZIKO YA KIKANISA BAADHI YA WAAMINI WAKE:

Jana mitandao ya kijamii nchini ilienea habari za kanisa kutokumzika tajiri mmoja kwa sababu alikufa katika hali ya "kinyumba" bila ndoa takatifu, na kwamba hakuwa mshiriki hai wa masuala ya kanisa.

Baada ya hapo kukatokea maneno mengi sana baadhi ya watu wakilishanbulia kanisa katoliki kwamba limekosea na linakosea kwa utaratibu huo, kwa maelezo mepesi kwamba suala la mtu kwenda mbinguni ni wajibu wa Mungu na siyo kazi ya kanisa kuhukumu (huenda wamesahau kwamba kanisa halijaihukumu roho ya marehemu bali limekataa kuuzika mwili wake tu ardhini).

Basi nimewiwa kufafanua kidogo niwezavyo kuhusu suala hili.

Karibu.......

Maziko ya kikanisa hayamfanyi mmoja aliyefariki aende mbinguni wala Jehanamu, bali yanamkumbusha mwombolezaji aliyebaki hai wajibu wake wa kuishi katika ushirika na kanisa ambalo ni mwili wa Kristo.

Kumzika au kutokumzika mtu kikanisa siyo jambo la kubeza ingawa ni kweli siyo linalompeleka marehemu mbinguni au motoni. Tukumbuke mwili wa marehemu unabaki ardhini. Kinachoenda mbinguni au motoni ni roho.

Lakini maziko ya kikanisa ni jambo lenye maana kubwa kutukumbusha tunaobaki duniani kwamba Kanisa ambalo ni mwili wa Kristo na ambalo Kristo mwenyewe ndiye kichwa chake *(Waefeso 5:23)* linataka waamini tuige mfano wa mwenzetu aliyeishi na kumaliza maisha yake akiwa na ushirika na kanisa, ndiyo maana linafanya maziko ya kikanisa kama sherehe ya kumpongeza, kumuaga na kutuonesha mfano wake ili tuufuate. Na kama ameishi na kumaliza maisha yake bila shirika kamili na Kristo kwa njia ya kanisa ambalo ni mwili wa huyo Kristo, kanisa linakataa kumzika ili kutuambia kwamba mfano wake siyo ufaao kuigwa.

*Kwa nini ni muhimu Mkristo ashiriki maisha ya kanisa badala ya kuishi kivyakevyake tu?*

Kwa sababu Kristo alitaka hivyo. Wakati anawaaga mitume wake na wanafunzi wake aliwataka WABAKI KATIKA UMOJA, NA WAKAE HIVYO HATA ROHO MTAKATIFU MZINDUZI RASMI WA KANISA AKIJA AWAKUTE WAKIWA PAMOJA NA WAMOJA.

Tutakumbuka hata sala ya Mwisho ya Bwana wetu Yesu Kristo kabla hajatiwa mikononi mwa wauaji aliwaombea wanafunzi wake WABAKI WAMOJA kama yeye na Baba walivyo MMOJA *(Yohane 17:11)*.

Hivyo maisha ya ukristo ya kivyakovyako kwa kujitenga na kanisa Siyo mpango wa Kristo bali mpango wako binafsi. Siyo mfano tunaopaswa kuuiga wala kuuendekeza.

Kungia mbinguni kuurithi uzima wa milele kunamdai mtu atimize masharti makuu mawili (Luka 10:25-28):

1. Mapendo kwa Mungu
2. Mapendo kwa jirani.

Lakini huwezi kumpenda Mungu nusunusu. Yaani ukampenda kichwa na ukamchukia mwili. Kama kanisa ni mwili wa Kristo, wawezaje kusema unampenda Yesu (Mungu nafsi ya pili) na bado huna muda na mwili wake yaani kanisa lake? Mnafiki wewe.....!

Na kama hukumpenda Mungu (kichwa na mwili) na hukumpenda jirani, utawezaje kuurithi uzima wa milele? Ni vigumu.

Ni vema kujitahidi kuiepuka njia hiyo, ndiyo maana kanisa linautumia msiba kutukumbusha njia njema na kutuonya juu ya njia isiyo njema.

Kumbuka Yesu alisema atakayemkiri yeye Yesu (ambaye kanisa ni mwili wake) mbele za watu, Yesu pia atamkiri mbele ya baba, na atakayemkana Yesu mbele za watu Yesu pia atamkana yeye mbele ya Baba yake wa Mbinguni atakapofika mbele ya kiti cha utukufu wa Mungu (Mathayo 10:32-33).

*Mfano wa taratibu za ki-kanisa ambazo ukijitenga nazo siyo rahisi kuupata uzima wa milele ni huu:*

Ukiuishi ukristo wako peke yako nyumbani mwako huna nafasi ya kushiriki EKARISTI TAKATIFU au kwa maneno mengine KOMUNYO au wengine wanaita CHAKULA CHA BWANA au wengine wanaita MKATE WA BWANA.

Lakini Yesu mwenyewe alisema:

" *Kweli nawaambieni,* Msipokula huu mwili wangu na kuinywa damu yangu, hamtakuwa na uzima ndani yenu. Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu, anao uzima wa milele. Nami nitamfufua siku ya mwisho"

*Yohane 6:53-54*

Zingatia vizuri hayo maneno ya mwanzo niliyoya-bold. Yesu anaanza kwa kusisitiza akisema *"Kweli nawaambieni,..*

Kwa nini Yesu alisisitiza?

Kwa sababu alijua kuna wengi watapuuzia suala la kukomunika (kushiriki chakula cha Bwana) wakidhani watakuwa na uzima wa milele kwa kuishi tu majumbani kwao bila kuja kanisani ambako ndiko chakula hicho hutolewa, wakijidanganya kwamba maadam waliishabatizwa (na wengine walibatizwa kwa maji mengi ya mto wote au bahari nzima) basi hiyo inatosha kwa wao kuurithi uzima wa milele.

Pia alijua wapo ambao wanaweza kuwa wanasali na kutoa sadaka kubwakubwa lakini wanaishi maisha yanayowafanya wasistahili kushiriki chakula cha Bwana, wakidhani ni rahisi kuupata uzima wa milele bila chakula hicho.

By the way..., hatuokolewi kwa matendo yetu. Tunaokolewa kwa neema (Waefeso 5:2).

Neema ya Mungu (yaani uwepo wa Yesu Kristo katika maisha na mazingira ya mwanadamu) haipatikani katika kujitenga wewe binafsi, bali inapatikana kwa kuungana na wenzako kwa jina la Yesu.

Yeye mwenyewe alisema:

"Wakutanikapo wawili watatu kwa jina langu, mimi nipo hapo kati yao"

Mathayo. 18:20.

Na kama Yesu yupo katikati ya walio na umoja/ushirika katika yeye, basi neema ya Mungu inapatikana katika ushirika huo na siyo katika ubinafsi na kujitenga. Na kwa kuwa tunaokolewa kwa neema, ni rahisi zaidi kuokolewa tukiwa ndani ya kanisa kuliko kuokolewa tukiwa tumejitenga na mambo ya kanisa.

Kwa hiyo ndugu yangu..., ni muhimu sana kushiriki mambo ya kanisa. Na ni muhimu sana kwa kanisa kuonesha shukrani nanpongezi (appreciation) kwa yule anayekufa katika ushirika na kanisa, na kuonesha kuhuzunishwa na yule anayekufa akiwa hana shirika na kanisa.

Neno la Mungu linasema "Heri watu ambao wanakufa wakiwa wameungana na Bwana. Naam, watapumzika kutoka katika taabu zao, maana matunda ya jasho lao yatawafuata" (Ufunuo 14:13).

Mstari huo wa mwisho kunukuu ni muhimu sana kwako ndugu yangu. Kwamba ukifa umetengana na Bwana kwa matendo yoyote ikiwemo kutengana na mwili wa Bwana Yesu (Kanisa lake) una ole. Na ukifa ukiwa umeungana naye kwa matendo yoyote ikiwemo kuungana na mwili wa Bwama Yesu (Kanisa lake) una heri. Na amemalizia kwa kusema "matendo yako yataambatana nawe" hata baada ya kufa. Ndiyo maana umekufa, lakini sifa za jitihada za jasho lako tunazihubiri hata wakati wa mazishi yako. Na kinyume chake, sifa mbaya ulizoacha tunazikana hata baada ya kufa kwako kwa kuyakana mazishi yako.

Tumsifu Yesu Kristo.

Ben Mukasa.
Milele amina

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huo utaratibu au uozo?Biblia ndio inautaratibu na si kanisa mnajipangia wenyewe, Kama mliambiwa muwe pamoja hapo ulipo mpo pamoja na papa? Acheni zenu shida yenu kuu ilikuwa ni pesa tu na si vinginevyo kama mnakula nguluwe na biblia imekataza nyie ndio mnamakosa zaidi.. makosa yaliyopo Roma yanakaribia makosa ya Shetani. ..
Pumbavu ww acha kutafuta kiki hapa.kwani ni lazima uchangie.ng'ombe ww

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hahahah nawe umekuwa Yesu sasa kujua mdhambi ni nani??
Dhambi zinaonekana ukifanya na ukishakuwa unafanya dhambi endelevu hufichiki.. like Malaya,wevi wanyang'anyi n.k tokea zamani Waliitwa hivyo... walijulikana kama wadhambi.. Biblia ndio imeandika na sio Sheria za kanisa Yesu alikuwa myahudi na Roma ilikuwa tawala ovu so ni uamuzi kufuata ya Yesu au ya Roma kanisa
 
Pumbavu ww acha kutafuta kiki hapa.kwani ni lazima uchangie.ng'ombe ww

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuweka wazi ukweli uliopo kwenye Biblia ndio kiki pole sana umepotezwa na ukapotea siku ukiujua ukweli ni too late mng'ang'anie Shetani tu hakuna hii pole sana nakupa.. kasome Biblia uwe huru umeelemewa na mizigo ya dhambi chuki ujinga n.k mengi mabaya hata tabia yako ni mbaya. Yesu bado anakupenda tumia nafasi yako kabla haijawa too late
 
Dhambi zinaonekana ukifanya na ukishakuwa unafanya dhambi endelevu hufichiki.. like Malaya,wevi wanyang'anyi n.k tokea zamani Waliitwa hivyo... walijulikana kama wadhambi.. Biblia ndio imeandika na sio Sheria za kanisa Yesu alikuwa myahudi na Roma ilikuwa tawala ovu so ni uamuzi kufuata ya Yesu au ya Roma kanisa
ninachoona nichuki uliyopandikizwa kwenye UKATOLIKI NDO MAANA MAPOVU YOOTE HAYO, mkuu nakuambia hakika mti wenye matunda ndiyo unatupiwa mawe ni haki yako kabisa kutukana.
 
Kuweka wazi ukweli uliopo kwenye Biblia ndio kiki pole sana umepotezwa na ukapotea siku ukiujua ukweli ni too late mng'ang'anie Shetani tu hakuna hii pole sana nakupa.. kasome Biblia uwe huru umeelemewa na mizigo ya dhambi chuki ujinga n.k mengi mabaya hata tabia yako ni mbaya. Yesu bado anakupenda tumia nafasi yako kabla haijawa too late
Kwendraaa.mchochezi ww huna adabu kabisa.unaleta upopompo wako.ww huko uliko nani anakujadili.acha kiherehere ng'ombe kabisa ww

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Safi sana mwalm B. Mukasa, hakika umeelezea vema sana.
 
mimi ni mkatoliki siendi jumuiya na wasinizike kazi ya kukusanya pesa ndo lengo kuu la jumuiya ,nilishaikataa jumuiya siku nyingi japo mamangu mzazi ni kiongoz huko jumuyani !!!!!!!!!!!!!!!!kama kwetu kule kunduchi hakuna sala ya maana mkifika ni blabla na kuongelea mambo ya pesa siendi nikitoa fungu la kumi tosha sasa kuna wawata sijui mavuno sijui nini unajukuta unachangisha pesa lukuki why????????????????????????? jumuia hasa za kikatoliki zinaongeza ugumu wa maisha na stress mimi nisizikwe na kanisa wala msikiti ni sawa tu
 
All in all

Mungu alisema hivi tena kwa kinywa chake mwenyewe kwamba

" ukiniheshimu nitakuheshimisha"

Bwana Yesu akasema hivi " na chochote mtakalo alifunga duniani na.mbinguni litakuwa limefungwa, na chochote mtakalo lifungua dunian na mbinguni litafunguliwa"

Mhubiri akasema hivi " kuliko mfu ukikosa maziko ni heri asingezaliwa"

Mtume PAulo alimaliza kwamba " ilipo hazina ya mtu ndipo moyo wake ulipo"

So kama bilionea aliweka hazina yake kwenye gurdoto, na kwa marais ndio ujue Sasa hazina yake aliiweka kwenye vitu viharibokavyo na ni sawa na kujilisha upepo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hili ndio kanisa pekee lililopotea, na lisilojua hata linakokwenda. wakatoliki mpokeeni Yesu awe Bwana na mwokozi wa maisha yenu, muokoke la sivyo moto wa milele unawasubiri. huwa nakereka nikihudhuria misiba yenu, unakuta padre aliyesoma miaka mingi dini, hajui hata anachokihubiri, mmesoma Bible lakini hamtakuja kuielewa na haitakuja kuwasaidia. mmebaki tu kama NGO na sio sehemu ya kusaidia watu kwenda mbinguni.
Asante kwa kuchukua nafasi ya Mungu ya kuhukumu wengine..!!!

Ila kwa akili yako unafikiri Wakatoliki hawajampokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi...????Je unaelewa maana ya kumpokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi...????

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huo utaratibu au uozo?Biblia ndio inautaratibu na si kanisa mnajipangia wenyewe, Kama mliambiwa muwe pamoja hapo ulipo mpo pamoja na papa? Acheni zenu shida yenu kuu ilikuwa ni pesa tu na si vinginevyo kama mnakula nguluwe na biblia imekataza nyie ndio mnamakosa zaidi.. makosa yaliyopo Roma yanakaribia makosa ya Shetani. ..
Kijana acha kuropoka ovyo,unaoneka uko shallow sana kwenye maandiko(Biblia),apo kwenye hilo LA nguruwe umeonesha ni jinsi gani ulivyo shallow.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwendraaa.mchochezi ww huna adabu kabisa.unaleta upopompo wako.ww huko uliko nani anakujadili.acha kiherehere ng'ombe kabisa ww

Sent using Jamii Forums mobile app
Hayo maneno ndio kakufundisha paroko au Papa? Kama mmegoma kumzika mtu aliyebatzwa kuwa Mkatoliki sishangai maneno yako mfuasi wa Shetani.. anayewaongoza... Catholic mpokeeni Yesu muwe wema
 
Hata Cain akimzika Abel bila kanisa Na Mungu akampokea...

Kama ni mkristo mlimsajili kwa ubatizo hakuja futio so anabakia na Ukristo wake nyie wajaa dhambi hamna nafasi ya kuhukumu... jiulize watu wote wafe duniani wazikwe and then ukibakia wewe peke yako ukafa nani atakuzika?
Umeshasema Cain alimzika Abel...!!Je umesoma vzuri hicho kitabu ili ujue maisha ya Abel hapa duniani kabla uja expose your foolishness humu...?????

Unasema Wakatoliki hawawezi kuhukumu..,ni kweli kabisa,Je kuna Mkatoliki aliyemuhukumu Mrema....????

Hebu onesha hukumu iliyotolewa dhidi ya marehemu ili tuanzie hapo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom