DOMINGO THOMAS
JF-Expert Member
- Feb 16, 2023
- 365
- 365
- Thread starter
- #181
Cha sasa.Acha porojo nyingi,
Wewe ungekuwa mtumishi ungependa ulipwe pensheni yako kwa kikokotoo kipi?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Cha sasa.Acha porojo nyingi,
Wewe ungekuwa mtumishi ungependa ulipwe pensheni yako kwa kikokotoo kipi?
Kikokotoo kipya kimeanza kutumika July 2022, unaweza kwenda kwenye mfuko ( ofisi ) ambayo ipo karibu na wewe kupata utaratibu.Ok..so hapo kastaafu july 2018, na kwa document hiyo nitajuaje kama ni kipya au cha zamani
Ukisha lipwa kiinua mgongo, hakuna pesa inayo baki kwenye mfuko ambayo wewe umechangia.Ass hole, kuna ubaya kulipwa pesa yako yote?wewe utakuwa umerogwa! Yaani kulipwa mkwanja wako wote ni jambo baya!
Nani anakufa...!?Hii habari ya mfuko uweze kujiendesha ndiyo inawaumiza watu, fedha zinawekezwa kwenye madude yasiyo na maslahi kwa wanachama mwisho wa siku wanaishia kuumia na kufa kwakuwa kuna genge la wahuni wanacheza kamari na hayo mafao ya watu
Hujashuhudia wastaafu wakifa kwa kupata mshituko baada ya mafao yao kuyumbishwaNani anakufa...!?
Shukran mkuuKikokotoo kipya kimeanza kutumika July 2022, unaweza kwenda kwenye mfuko ( ofisi ) ambayo ipo karibu na wewe kupata utaratibu.
Mtumishi wa serikali anachakia 5% kutoka kwenye mshaara wake kwaajiri ya pensheni, asilimia zaidi 90% ya mshaara wake anabaki nao.Hujashuhudia wastaafu wakifa kwa kupata mshituko baada ya mafao yao kuyumbishwa
asante mkuu.View attachment 2975825
Soma hapo.
na jingine mbona hiyo formula haizingatii umri wa mtu kwenye ajira. maana inaangalia wastani wa mishahara ya miaka 10 tu ambayo maana yake mtu aliyefanya kazi kwa miaka 30 atakuwa hana tofauti ya maslahi yake ya mwisho na yule alifanya kazi kwa miaka 15 na pengine kama huyu wa miaka 15 alikuwa na mshahara mkubwa basi atamwacha mbali sana huyo wa miaka 30 au hilo likoje? nini kitakachowatofautisha hao watu wawili kwenye maslahi watakayopata?View attachment 2975825
Soma hapo.
Mapungufu ya hiyo formula ndio imefanywa ifutwe ( Iondolewe ). Ilikuwa inaua mifuko.
2014 - 2018 wastaafu walio kuwa wakistaafu PSPF na LAPF walikuwa wakisubiri zaidi ya mwaka kulipwa CP kwasababu mifuko ilikuwa haina pesa na kilicho sababisha mifuko hiyo kushindwa kujiendesha 70% ilikuwa ni formula ya kikokotoo wanacho tumia.
mkuu DOMINGO THOMAS kwanini mnapost haya mambo muhimu kwa maslahi ya maisha ya wengi kwa kutumia akaunti za uchepe?Watumishi wa umma wengi sasa hivi wanafuatilia issue ya kikokotoo cha mafao yao ya baadaye.
Hata hivyo wapo watumishi wa umma ambao wapo kimya kuhusu kikokotoo labda kwa kuwa miaka yao ya kustaafu bado iko mbali saaana.
Wapo wengine wanaoongea kwa kuwa kikokotoo kipya kimewagusa kwa namna moja ama nyingine.
Kama Mwanazuoni wa Hifadhi ya Jamii, Naomba nifafanue baadhi ya mambo kuhusu kikokotoo cha mafao ya kustaafu.
Kikokotoo kipya cha:
1/580 × APE x PoS x 12.5 x 33%
Na kikokotoo cha zamani cha LAPF na PSPF yaani
1/540 × LAS x PoS x 15.5 x 50%
(LAS = Last Annual Salary na PoS = Period of Service)
APE = Annual Pensionable Emoluments
1/540 = Acrual factor
15.5=Commutation Factor
50%=Commutation Rate
Usipojifunza jinsi ya vikokotoo hivyo viliundwa utashindwa kuishawishi Serikali kipi kirekebishwe na kwa nini. Ni kama unakuwa unaongea kitu usichojua.
Kusema Serikali ikulipe pesa yako yote ni ujinga ujinga mkubwa saaana ambao watumishi wa umma wenye ujinga ndiyo watapromoti hoja hii.
Vikokotoo vyote hivyo vina uzuri na ubaya wake. Kama wewe siyo mchambuzi utashabikia tu lolote bila kujua vizuri matokeo yake.
Sheria za Kikokotoo cha PSPF na LAPF kilikuwa na mapungufu meengi sana. Bahati mbaya mapungufu hayo hakuna watalaam wanaoyadadavua sasa hivi.
Wanachama waliokuwa PSPF na LAPF kikokotoo chao kilikuwa na mapungufu kibao ukiacha upande wa Kiinua mgongo tu vipengere vingine vyote havikuwa vizuri.
Kikokotoo cha wanachama waliokuwa PPF, GEPF na NSSF kilikuwa hiki hapa:
1/580 × APE x PoS x 12.5 x 25%.
(APE = Annual Pensionable Emoluments na PoS = Period of Service/Contribution)
Makundi haya ya wanachama ambao ni zaidi ya 81% ya wanachama wote wa mifuko iliyokuwepo kwao kikokotoo kipya kimewaongezea mkupuo wa mafao waliokuwa wanapata kwa 8%. Yaani iko hivi:
1/580 × APE x PoS x 12.5 x 25%
Hapo kwenye asilimia 25 kwa kikokotoo kipya wao imekuwa 33% ambayo ni ongezeko la 8%.
Sasa watumishi wa umma wote wamepewa kikokotoo kimoja bila kujali wako idara ipi.
Zamani (2004 hadi 2018) waliokuwa Serikali kuu na serikali za mitaa yaa LAPF na PSPF walikuwa wakilipwa Mkupuo Mkubwa saaana kwa Kikokotoo hiki hapa cha 1/540 × LAS x PoS x 15.5 × 50% kwa sababu kikokotoo hicho cha Serikali Kuu kilizingatia Last Month Salary
Na wale wa sekta binafsi chini ya NSSF na PPF walitumia kikokotoo kilichozingatia Wastani wa Mshahara wa miaka mitatu.
Kwa hiyo tunafanyaje? Tuchukue kikokotoo cha serikali Kuu kiwe cha wanachama wote wa sekta binafsi na umma halafu mfuko uishiwe nguvu kulipa mafao baada ya miaka 5???
Au tuchukue kikokotoo cha sekta binafsi kilichokuwa kinatumika NSSF, PPF na GEPF kiwe cha wote na kiboreshwe kidogo from 25% to 33% na mfuko uweze kujiendesha kwa miaka mingi???? Kipi bora??
Maamuzi yaliyochukuliwa na serikali mwaka 2018 yalikuwa ya kuwatazama wanachama 81% waliokuwa mifuko ya NSSF, PPF, na GEPF ili wafanyakazi wote wafanane kwenye mafao ya uzeeni.
Yaani serikali ililenga kufanya pensheni ya kila mwezi na malipo ya Mkupuo yawe na usawa pamoja na watumishi wa umma waliokuwa na kikokotoo kikubwa kwa kutazama factors za uendelevu wa mfuko mpya wa PSSSF.
Mwaka 2014 hadi 2018 wastaafu wa serikali Kuu waliokuwa chini ya PSPF walikuwa wamefikia mahali Papaya sana hadi mafao yao yalikuwa hayapatikani tena kutokana na PSPF kushindwa kujiendesha kwa sababu ya madeni makubwa ambayo serikali ilikuwa inadaiwa tangu 1999.
Watu waliokuwa wanastaafu miaka hiyo 2014 hadi 2018 walikuwa wanaambiwa wasubiri. Walisubiri saaana mpaka Mwaka 2018 December mifuko ilipounganishwa zikachukuliwa fedha za LAPF na PPF kuwalipa wastaafu waliokuwa wamekaa mtaani bila mafao kwa zaidi ya miaka 2 hadi 3 bila mafao.
Ni bahati mbaya saaana kwamba tuna wanasiasa na wanachama wanaosahau mapema tulipotoka.
USHAURI MBAYA NI HUU
Kudai Kwamba wastaafu walipwe pesa zote (100%) na waendelee na maisha yao. Huu ni ushauri mbaya saaana kuishauri serikali.
Kwamba kwa nini wastaafu wawekewe pesa za kulipwa kila mwezi kidogo kidogo? Hili ni swali la kitoto litokanalo na kutojua maana ya Society Protection
Ukisikia mtumishi wa umma anadai hataki pensheni ya kila mwezi anaomba alipwe pesa zake zote aendelee na maisha yake ujue kuwa huyo siyo mtumishi wa umma. Ni Mjasiriamali.
Na Bahati mbaya watumishi wa umma asilimia 95 siyo wajasiriamali. Ni wategemezi wa mishahara ya kila mwezi.
Akilipwa pesa yote halafu ikaisha social economic crisis itakayotokea katika jamii ya wazee itazidi ile ya wazee wa East Africa Community waliovua nguo barabarani wakidai Pension ya kila mwezi.
Ukitaka kujua utamu wa pension ya kila mwezi kabla hujashauri utaratibu wa pension ufutwe, nakuomba ukawaulize waliostaafu miaka 10 iliyopita.
Waulize kama pesa kubwa ya kikokotoo kikubwa walicholipwa 2010 mpaka leo pesa ipo?
Kawaulize Tegemeo lao kuu la pesa ya kila mwezi ni wapi? Hawa wazee ukitaka ukosane nao ondoa utaratibu wa pension ya kila mwezi.
Waulize utamu wa pension na utamu wa kiinua mgongo ni kipi kitamu zaidi.
Kawaulize wazee waliostaafu 2010 kati ya Pension na Burungutu la pesa unayopewa ukistaafu ni kipi kiongezwe kiwe kikubwa?
Waulize kati ya Pension ya kila mwezi na kiinua mgongo(gratuity) wanashauri kipi kiongezwe?.
Ukiwauliza waliostaafu miaka 10 iliyopita wao wanaomba pension iongezeke iwe kubwa saaana.
Ukiwauliza wazee wastaafu Watarajiwa kipi kiongezwe, wao wataomba kiinua mgongo ndicho kiongezwe.
Hii inatokana na kwamba ni vigumu sana mstaafu mwenyewe tarajiwa kupendekeza alipwe nini kama hajafika huko uzeeni.
Wazee waliolipwa mafao kwa kikokotoo cha LAPF na PSPF miaka 5 iliyopita asilimia 90 yao tegemeo lao kuu kwa sasa ni pension ya kila mwezi pamoja na kwamba walilipwa kikokotoo kikubwa.
Hoja nyingine inayopotoshwa ni hii kwamba mstaafu analipwa pesa fulani na nyingine inabakia kwenye Mfuko kwa ajili ya kulipwa kidogo kidogo kama pension.
Huu nao ni uongo wa Mtaani umeshageuzwa kuwa kama ukweli.
Ukweli ni kwamba Hakuna pesa inayobakia kwenye Mfuko.
Mstaafu huwa analipwa pesa zote alizochangia yeye na Mwajiri wake (5% na 15%) halafu Mfuko unaongeza nyingine kutoka kwenye uwekezaji na kisha anaanza kulipwa pension kila mwezi. Hapo unasemaje kuna pesa imebakia PSSSF au NSSF.
Ukweli ni kwamba Mstaafu akishalipwa kiinua mgongo ambacho huwa mara nyingi ni zaidi ya hata michango yake yote anaanza kulipwa Monthly Pension ambayo mara nyingi huwa ni zaidi ya 40% hadi 50% ya mshahara wake (Net pay) aliyokuwa analipwa akiwa kazini.
Ukweli ni kwamba Pension hiyo atalipwa maisha yake yote yaliyoko mbele Hata kama akiishi miaka 50 au zaidi baada ya kustaafu.
Ndugu wafanyakazi wenzangu kama tunaomba mafao makubwa tuwe tayari kuongeza uchangiaji yaani badala ya kuchangia 5% au 10% ya mishahara yetu tukubaliane kiasi kiongezwe kiwe 10% au 15% na Mwajiri atuongezee 15% au 20%
Au pia kama tukitaka mafao makubwa tukubaliane mfumo wa pension ya kila mwezi uondolewe ili kila mtu akistaafu alipwe Kiinua mgongo kama wabunge na Madiwani halafu pension isiwepo.
Au tuchague mfumo wa pension kwa wote ambapo hakuna kuchangia chochote kila mwezi na kila mwananchi akitimiza miaka 55 au 60 anaenda HAZINA kuu ya Serikali kuchukua Kiinua mgongo chake bila kujali alikuwa mwajiriwa au Mjasiriamali.
Au tuchague kuwa na Mifuko mingi ya pension na kila mfuko ujipangie mafao utakayotoa chini ya Sheria za ushindani na serikali isiingilie lolote zaidi ya kuweka Sheria na sera za kuwalinda wateja wa Skimu hizo.
Imeandikwa na
FADEMO DIRECTOR.
Social Security Practioner with 19 years of Field Experience
Ni wale waliosumbuliwa hapo katikati mfuko ulipofilisikahuyu aliye kufa ni wale walio tumia 90%+ ya mshaara wao kwenye starehe, huku wakitegemea 5% ya mshaara wao uje kutumiza malengo yao yote hapa duniani
Wasio pensionable ni kizazi cha sasa ambacho hakina ajira zenye ujira...., uzee wao tutakuwa hatuongelei wanapata kidogo bali watakuwa hawapati kabisaWasio pensionable ni wepi tena?
Hapana tena hao ndio wa kuwaongelea sababu pension zingekuwa hazina faida kwa taifa hata hawa wa sasa sheria insingepitishwa ya kukatwa percent yako kwa lazima na mwajiri kulazimishwa kukuongezea ili uzeeni upate security...., Na kuna nchi hakuna kabisa kiinua mgongo wewe ukifikia miaka kadhaa sababu ulikatawa national insuarance directly unaingia kwenye pension...., hio sio kwa faida yako tu bali ni kulinda ustawi wa jamiiWasio pensionable are out of this discussion.
Pension funds hazihitaji kucheza kamari au kuwekeza kwenye volatile investments..., shida kuna watu hapo katikatika walijiwekea marupurupu na kujipa pesa za unono zaidi ya uwezo wa uwezo wa mfuko kulipa watu..., ofcourse hio ni pamoja na ufujaji mwingine..., lakini kutenda kosa moja hakufanyi tufanye makosa mengine, na mimi nasimamia palepale pesa ya kila mwezi kwa mstaafu angalau inayokidhi basic needs ni muhimu sana kwa ustawi wa taifa...., kwa bahati mbaya ukifa kabla haujavuta yote wengine watakaoishi zaidi watafaidi ila mnufaika zaidi ni jamii iliyokuzunguka kutokupigwa mizinga.....Issue iliyopo ni kuwa pesa ya mifuko imewekezwa sehemu isiyolipa na nyingine imeliwa, hawana uwezo wa kulipa
Unaweza kuuliza tena, na ukaachana na matusi.Wewe popoma DOMINGO THOMAS naomba Sasa swali langu kwenye post #170 lijibiwe
Hii haiwekwi tu, kinacho angaliwa ni uwezo wa kuishi Tanzania ni 67 - 72.5 pitia uko Data utaona.asante mkuu.
sasa apo kwanini mmepunguza umri wa kuishi wa mstaafu baada ya kustaafu kutoka miaka 15.5 hadi hiyo 12.5? ni kwamba mmegundua hawakatizi hiyo miaka 12.5 au ndo mnataka wawe wanakufa wakifika hiyo miaka 12.5?