Ufafanuzi kuhusu kikokotoo cha mafao ya kustaafu

1/580 × Miezi ya uchangiaji × APE × 0.33 × 12.5

Miezi ya uchangiaji ipo, aliye fanya kazi miaka 20 na mwengine 30 hawawezi kuwa sawa kwenye pension hatakama wamestaafu na daraja moja.
 
Huwezi kuandika bila matusi..!? Niicho kijibu kipo sahihi na ndivyo ilivyo.
 
Mimi sio mtu wa ofisi, na sipo ofisi yoyote. Mimi ni mtaalamu wa hifadhi ya jamii ( Social protection expert ) Naongea kitu ambacho nimekisoma na nina uzoefu nacho

Hii Kiinua Mgongo ipo Tanzania tu, na baazi ya Developing countries, nchi zingine hazina mfumo wa kiinua mgongo ukisha staafu unaunganisha moja kwa moja na monthly pension.

Tanzania tunatatizo la maslai ( Mishaara kwa watumishi ) sio kikokotoo
 
Ni wale waliosumbuliwa hapo katikati mfuko ulipofilisika
Kipindi LAPF na PSPF zinakosa fedha za kuwalipa wastaafu, zilikuwa zina matumizi makubwa ya pesa ( Expenses ) kuliko kile wanacho ingiza.. Mtu kachangia Million 40 anakuja kulipwa kiinua Mgongo million 120 na Monthly pension inakuwa 700k, mara tatu zaidi ya kile alicho changia hapa sustainability ya mfuko lazima ufe.

Hatukatai serikali inakopa na kuna ufujaji wa pesa... Ila mapungufu ya kikokotoo cha PSPF na LAPF ilichangia zaidi ya 70%+ hiyo mifuko kushindwa kujiendesha.
 
Hicho kikokotoo ni Kwa watumishi wa hali ya chini tu, vipi diwani, mkuu wa wilaya,mkoa, wazri mbunge. Inamaana wao tu ndo wenye akili za matumizi ya pesa
Tumesha ongea sana kuwa madiwani, wakuu wa mikoa, wabunge sio wanachama na hawachangii kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii PSSSF/NSSF na hawalipwi na hiyo mifuko.
 
Sana lo Kikokotoo siooo kabisa!
Hakuna mtu ambaye hajalipwa na kikokotoo hii nchi, kiwe cha zamani au kipya vyote ni vikokotoo.

Mmoja anapata kingi mwanzoni Vs Mwengine anapata Kingi Mwishoni, Mmoja akifa tegemezi wake wanakuwa hawana cha kupata Vs Mwengine akifa tegemezi wake wanacho cha kilipwa.
 
Nasemea hiki cha sasa ni Hatari kwa afya ya mafao asee!

Cc Smart911
 
Nasemea hiki cha sasa ni Hatari kwa afya ya mafao asee!

Cc Smart911
- Kiinua Mgongo ni zaidi ya kile ulicho changia kwenye mfuko, simply mtu akisha lipwa kiinua mgongo inakuwa hakuna pesa ambayo umebakiza kwenye mfuko.

- Ni ngumu kuielewa zana ya Hifadhi ya jamii, kama unalengo la kupinga na kukosao sio kujifunza mfumo wa hifadhi ya jamii unafanya kazi vipi.
 
Sawasawa!
Asante kwa ufafanuzi

Cc Smart911
 
Kwamba kujibu hoja hiyo mpaka jumamosi?
Nipe muda lakini kwa kifupi:👇🏿


1. Kipya kwa walio kuwa PSPF na LAPF Kiinua Mgongo ni kidogo kuliko cha zamani.

2. Kipya kwa walio kuwa PSPF na LAPF pensheni ya kila mwezi ni kubwa kuliko cha zamani.

3. Kipya mstaafu akifariki tegemezi wake watalipwa ×36 yakile alicho kuwa anakipata kwa mwezi.

4. Kipya hakitumii Last Salary, kinatumia Wastani wa mishaara bora ya miaka mitatu ndani ya miaka 10 kabla ya kustaafu.. Amboyo ni faida kubwa kwa mtu ambaye alikuwa na kitengo alafu kabla ya kufikia kustaafu akapunguzwa mshaara.

5. Kipya kwa wanachama walio kuwepo LAPF na PSSSF kimepunguza Umri wa kuishi baada kustaafu hii ni kutokana na living standard ya nchi yetu, kwa Wanachama wa NSSF, GEPF na PPF umri wa kuisho baada ya kustaafu ni ule ule.

6. Kipya kimepungaza kikokotoo limbikizi kwa wanachama wa LAPF na PSPF kwa NSSF, GEPF na PPF kimebakia vilevile

7. Kipya kinafanya mfuko uendelee kujiendesha kikamirifu, na kuendelea kuwepo vizazi na vizazi

Haya yote inatakiwa uelewe zana ya Hifadhi ya jamii ni nini...!? Hifadhi ya jamii yaipo kwaajili ya kukupa utajiri, pesa ya kujengea nyumba kununua gari n.k hifadhi ya jamii ipo kwaajiri ya kukupa income security pale unapo poteza kazi/kipato iwe kustaafu, kuondolewa kazini, kuugua nk
 
Mimi sijakuelewa. Mfano nimestafu nikiwa na mshahara wa 1ml kwa mwezi. Kwa kikokotoo kipya fedha ya mkupuo (lump sum) itakuwa kiasi gani?
1. Kwenye kikokotoo hatutumii mshaara wa mwisho tunatumia wastani wa mishaara bora ya miaka mitatu ndani ya miaka 10 kabla ya kustaafu.

2. Miezi ya uchangiaji pia inanasafi kubwa katika kuongeza pension yako aliye fanya kazi miaka 40 vs 30 hawa wakistaafu kwenye daraja mmoja hawawezi kulingana kwenye pension.

3. Ni ngumu sana mtu kukokotoa utalipwa kiasi gani kwa kumwambia tu mshaara yangu ni huu, kifupi hawezi kukokotoa.
 
Mkuu umekosea. Mimi pia simuelewi mleta mada
1. Kwenye kikokotoo hatutumii mshaara wa mwisho tunatumia wastani wa mishaara bora ya miaka mitatu ndani ya miaka 10 kabla ya kustaafu.

2. Miezi ya uchangiaji pia inanasafi kubwa katika kuongeza pension yako aliye fanya kazi miaka 40 vs 30 hawa wakistaafu kwenye daraja mmoja hawawezi kulingana kwenye pension.

3. Ni ngumu sana mtu kukokotoa utalipwa kiasi gani kwa kumwambia tu mshaara yangu ni huu, kifupi hawezi kukokotoa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…