lord atkin
JF-Expert Member
- Sep 30, 2018
- 257
- 922
UTANGULIZI
Nimekutana na video mitandaoni ikimuonesha mwanadada aitwaye Frola Shija akifafanua kuhusu nyumba ya wanandoa. Katika video hiyo ameeleza kwamba mwanaume akijenga nyumba kabla ya ndoa halafu akaoa mke na kwenda kuishi naye kwenye hiyo nyumba inakuwa ya kwao wote.
Pia ameeleza kwamba kama mwanaume akijenga nyumba kabla ya ndoa halafu akaoa mke asiishi naye kwenye hiyo nyumba nyumba hiyo itabaki ya kwake peke yake. Kauli hii imeibua hisia tofauti miongoni mwa wasikilizaji kwa sababu mwanasheria huyo hakuweza kueleza kiunagaubaga isipokuwa alitoa maelezo na mahitimisho ya jumla.
Kama mwanataaluma ya sheria nimewiwa kujitokeza katika jukwaa hili kueleza sheria inasema nini hasa kuhusiana na dhana ya nyumba ya wanandoa?.
MAANA YA NYUMBA YA WANANDOA
Katika sheria neno "nyumba ya wanandoa" au "matrimonial home" lina tafsiri ya pekee sana. Tafsiri fupi ya nyumba ya wanandoa ni " nyumba ambayo wanandoa wanaishi", hapa haijalishi ni nani anamiliki bali ni nani anaishi. Kama wanaoishi kwenye hiyo nyumba ni wanandoa basi hiyo ni nyumba ya wanandoa. Kuna mtu atajiuliza vipi kama tumepanga? Bado itakuwa ni "nyumba ya wanandoa" waliopanga humo.
Swali ambalo mtu atajiuliza vipi kama tumejenga nyumba kwa kushirikiana lakini hatuishi humo tumepangisha? Nyumba ambayo wanamiliki wanandoa na hawaishi itatambulika kama "matrimonial property" yaani mali ya wanandoa lakini si "matrimonial home" maana wanandoa hawaishi huko.
HAKI ZA MWENZI KWENYE NYUMBA YA WANANDOA
Katika "nyumba ya wandoa" yaani ambayo wanandoa wanaishi, kama hiyo nyumba inamilikiwa au imeandikwa jina la mwanandoa mmojawapo sheria inamzuia mwanandoa husika kuuza, kupangisha au kukopea bila kupata ridhaa ya maandishi kutoka kwa mwenzi wake. Kwahiyo hapa hata kama nyumba hiyo ipo kwa jina lako mwanaume ukiwaleta maafisa mikopo wa benki wakiiona tu kuna vitenge vimeanikwa nje watashtuka lazima wakuombe ridhaa ya mkeo.
Kuna wale ambao nyumba ya wanandoa wamepanga basi it means you can not sub-lease kwa mtu mwingine bila ridhaa ya mwenzi wako, natambua sheria inaruhusu mpangaji kupangisha /kufaulisha pango lake hivyo kama ni ya wanandoa hutaruhusiwa kufanya hivyo bila ridhaa ya mwenzi wako.
NINI HUTOKEA KWENYE NYUMBA YA WANANDOA MNAPOTALIKIANA
Ninajua hapa ndipo kuna trick, mwanasheria wetu alisema inakuwa ya kwenu wote, lakini ufafanuzi ni kwamba wakati wa talaka nyumba hiyo ya wanandoa itagawanywa kutokana na mchango wa kila mwanandoa. Kama ulikuta nyumba imekamilika asilimia 100 na wakati wote wa ndoa tulioishi humo hukuchangia hata kukarabati kitasa cha mlango utaondoka mikono mitupu kwenye nyumba hiyo.
Lakini kama wakati tukiishi hapo ulichangia kusombelea tofali za kujenga uzio, kukwetua nyasi nk unaweza pata hata 5% ya mgawo wa thamani ya nyumba. Kwa kifupi wakati wa talaka mali za wanandoa hugawanywa kutokana na mchango.
N.B: Ni ngumu sana kuishi pamoja kwenye ndoa miaka 15 halafu nyumba isikarabatiwe.
NINI HUTOKEA KWENYE NYUMBA YA WANANDOA MMOJA AKIFARIKI
Kama hati ilikuwa kwa jina la marehemu nyumba hiyo itaingia kwenye mali za mirathi ya marehemu na kama mwenzi aliyebaki anadai amechangia basi atadai haki yake wakati wa kugawanywa mirathi mahakamani. Na kama ipo kwenye jina la aliyebaki hai haitaingia kwenye mirathi ya marehemu na kama msimamizi wa mirathi anadai marehemu alichangia basi ataitaja mahakamani na mahakama ya mirathi itaangalia kiwango cha mchango wa marehemu.
Wakatabahu