Masiya
JF-Expert Member
- Apr 2, 2012
- 7,602
- 7,332
Inaelekea mifumo yetu haijatengemaa bado. Tuna level 3 toka basic certificate hadi ordinary diploma. NTA 4 basic certificate, NTA 5 Certificate na NTA 6 Ordinary Diploma. Tofauti inakuja kwenye packaging. Kuna vyuo vinatoa cheti kila ngazi, kuna vyuo vina tenganisha level 4 na level 5 ikienda na level 6 yaani certificate level 4 mwaka mmoja halafu unaingia "diploma course" ambayo ni muunganiko wa 5 na 6. Kana kwamba haitoshi kuna wanao package zote 3 pamoja yaani unadahiliwa kama mwanafunzi wa diploma lakini unapitia level zote 3 kwa mfano hizi technical cilleges za serikali.
Upande wa mifugo na kilimo zamani ilikuwa cheti miaka 2 na diploma miaka 2 lakini naona sasa wanatakiwa wafiti kwenye level 4 hadi 6, hivyo vyuo vingi vinatoa cheti level 4 na 5 pamoja hii inamaanisha unatoka na cheti cha 5. Ukichukua diploma unasoma kwa mwaka mmoja level 6.
Nisichoelewa hizo GPA za Diploma zinahusisha miaka mingapi-NTA level 6 peke yake au miwili level 5 na 6 au yote mitatu level 4 hadi 6. Naona pana kizungu mkuti hapa.