Ufafanuzi: Kuvunjwa Halmashauri ya Jiji la Dar kuipandisha hadhi Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kuwa Jiji

Ufafanuzi: Kuvunjwa Halmashauri ya Jiji la Dar kuipandisha hadhi Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kuwa Jiji

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2012
Posts
10,307
Reaction score
25,932
Tangu Rais Dr. John Pombe Magufuli kuvunja Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na kuipandisha hadhi Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kuwa Jiji la Dar es Salaam, kumekuwa na mijadala kemkem kuhusu jambo hilo runingani, redioni na hata mitandaoni. Mjadala hasa unajikita katika kuelewa kilichofanyika jana. Wapo wanaosema kuwa kwasasa Mamlaka tu ya lililokuwa Jiji la Dar es Salaam ndiyo yaliyowekwa chini ya Ilala na jiji liko vilevile na pale pale.

Wapo wanaosema kuwa kwasasa Ilala ndiyo jiji na wengine ni Manispaa ndani ya Jiji la Dar es Salaam. Katika kuelewa jambo hili kuna mambo ya kuyafahamu. Mosi, kabla ya jana, Dar es Salaam kama mkoa ulikuwa na Halmashauri za Manispaa tano: Ilala, Kinondoni, Ubungo, Temeke na Kigamboni. Halafu, kulikuwa na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ambalo kinadharia lilijumuisha Manispaa zote hizo.

Pili, hadhi ya juu kabisa ya kihalmashauri ni Jiji. Tatu, jana likavunjwa lililokuwa Jiji la Dar es Salaam (kwa maaa ya kuondolewa kwa iliyokuwa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam). Zikabaki Halmashauri za Manispaa tano. Moja ya Manispaa hizo-ya Ilala ikapandishwa hadhi kuwa Halmashauri ya Jiji na 'kubatizwa' jina la Dar es Salaam. Sasa kuna Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ambayo kimsingi ni iliyokuwa Hamlmashauri ya Manispaa ya Ilala.

Ndiyo kusema, Jiji la Dar es Salaam kwasasa ni sehemu yote ya Wilaya ya Ilala na si vinginevyo. Wilaya za Kinondoni, Temeke, Ubungo na Kigamboni si sehemu ya jiji la Dar es Salaam. Hizo zimebaki kuwa Halmashauri za Manispaa. Katika kueleweka zaidi, Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ya sasa imepakana na Halmashauri za Manispaa za Kinondoni, Temeke, Ubungo na Kigamboni. Kwahiyo, mtu wa Ubungo, Temeke, Kinondoni na Kigamboni hayupo ndani ya Jiji la Dar es Salaam.
 
kuna faida gani aswa
Mosi, kuwa na eneo mahsusi la kiutawala la Jiji la Dar es Salaam kama Halmashauri. Pili, kuondoa matumizi yasiyo ya lazima ya Madiwani waliokuwa wakishiriki vikao vya lililokuwa Jiji huku wao wakitokea na kushiriki kwenye Halmashauri zao.

Kiukweli, yalikuwa matumizi mabaya ya fedha kwa kuzingatia kuwa Halmashauri ya Jiji iliyovunjwa haikuwa na vyanzo vya mapato.
 
Moja ya manufaa yake ni kulifanya Jiji la Dar es Salaam kuwa na sehemu yake mahsusi ya kiutawala tofauti na ilivyokuwa awali. Awali, jiji la Dar es Salaam ni kama lilikuwa likielea kuhusu eneo hasa la kiutawala.
Kiuhalisia hapa hujataja faida.

Kuelewa kulikua na madhara gani kiuendeshaji ana kiuchimi? Maana ilikuwepo toka mwanzo na kasi ya ukuaji ilikua juu pia.
 
Kiuhalisia hapa hujataja faida.
Kuelewa kulikua na madhara gani kiuendeshaji ana kiuchimi? Maana ilikuwepo toka mwanzo na kasi ya ukuaji ilikua juu pia
Halmashauri kuwa na eneo mahsusi ni faida. Kabla ya jana, Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ni kama ilikuwa ikielea huku mamlaka yalikuwa kwa kila Manispaa na maeneo yake
 
Mosi, kuwa na eneo mahsusi la kiutawala la Jiji la Dar es Salaam kama Halmashauri. Pili, kuondoa matumizi yasiyo ya lazima ya Madiwani waliokuwa wakishiriki vikao vya lililokuwa Jiji huku wao wakitokea na kushiriki kwenye Halmashauri zao. Kiukweli, yalikuwa matumizi mabaya ya fedha kwa kuzingatia kuwa Halmashauri ya Jiji iliyovunjwa haikuwa na vyanzo vya mapato.
Jiji halikua na vyanzo vya mapato kivipi wakati Ubungo Stand ya Mkoa ilikua chini ya Jiji? Zile 300 za kuingia ndani sio vyanzo?

Parking za kati kati ya Jiji zilikua zipo chini ya nani?
 
Pamoja na maelezo mengi ila umewaingiza chaka wasomaji wa Makala hii

Jiji la Dar es Salaam liko pale pale kimajukumu, kieneo na kiutaratibu was watu kutambulisha Maeneo yao,
Mkoa wa Dar es Salaam Ni jiji, ila kwenye masuala ya maulaji yao ndo wamepunguza, Cha msingi rejea maelezo yako yapange upya

Nanukuu

"Jiji la Dar es Salaam litaendelea kuwepo lakini tutachukua eneo fulani nafikiri Ilala inafaa kuwa jiji, ndio katikati ya jiji la Dar es Salaam, wewe Ubungo utasubiri kwanza kwasababu hata barabara bado hazijatengenezwa tengenezwa lakini nafanya haya ndugu zangu kwa kuangalia matumizi mazuri ya fedha zetu". Mwiso wa Nukuu
 
Back
Top Bottom