Ufafanuzi: Kuvunjwa Halmashauri ya Jiji la Dar kuipandisha hadhi Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kuwa Jiji

Kama nimekuelewa, Kinondoni, Temeke, Kigamboni na Ubungo hazipo tena ndani ya jiji la DSM.
Huko ni kuwachanganya wanafunzi na walimu mkumbuke kuchapisha vitabu vipya vya maarifa ya jamii.
 
... kwa maana hiyo ni sahihi kusema ifuatavyo?
  • ... kwamba eneo la jiji la Dar-es-Salaa (city proper) ni eneo la iliyokuwa Manispaa ya Ilala? Kwamba kieneo Dar-es-Salaam ya sasa ni ndogo kuliko Dar-es-Salaam ya kabla ya jana?
  • ... kwamba kwa idadi ya watu, Dar-es-Salaam ya kuanzia jana idadi yake ya watu ni sawa na idadi ya watu wa Ilala?
  • ... kwamba Dar-es-Salaam ambayo ilikuwa miongoni mwa majiji yanayokuwa kwa kasi zaidi duniani uanzia jana sifa hiyo imekoma? Petro E. Mselewa
 
Huu uamuzi wa Magufuli kimsingi umeturudisha nyuma, manispaa zikipandishwa hadhi ndio huitwa jiji, sasa tumeziporomosha kutoka kuwa majiji na kuzirudisha nyuma tena, sitashangaa huu uamuzi wa Magufuli ukija kutenguliwa na Rais ajaye.
 
Jiji halikua na vyanzo vya mapato kivipi wakati Ubungo Stand ya Mkoa ilikua chini ya Jiji? Zile 300 za kuingia ndani sio vyanzo?

Parking za kati kati ya Jiji zilikua zipo chini ya nani?
Yale ni mapato ya manispaa ya Ubungo
 
Mkoa wa Mwanza una wilaya 5: Nyamagana,Ilemela,Misungwi,Magu na Sengerema. Jiji la Mwanza lina Wilaya 2: Nyamagana na Ilemela. Wilaya ya Nyamagana ndiyo halmashauri ya jiji la Mwanza, Wilaya ya Ilemela ni Manispaa lakini iko ndani ya jiji la Mwanza. Je Dar es Salaam?
 
Halmashauri kuwa na eneo mahsusi ni faida. Kabla ya jana, Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ni kama ilikuwa ikielea huku mamlaka yalikuwa kwa kila Manispaa na maeneo yake
Kwa hiyo unamaanisha toka mwanzo kabisa mkoa wa Dar ulipewa hadhi ya jiji kwa sababu ya halmashauri ya Ilala tuu?

Ndio tuseme hizi halmashauri zingine zilikuwa hazicontribute chochote kwenye hiyo halmashauri ya jiji?
 
Moja ya manufaa yake ni kulifanya Jiji la Dar es Salaam kuwa na sehemu yake mahsusi ya kiutawala tofauti na ilivyokuwa awali. Awali, jiji la Dar es Salaam ni kama lilikuwa likielea kuhusu eneo hasa la kiutawala.
Hayo unayoita manufaa mimi naweza kuyaita ndio mapungufu....

Mwanzo ingeweza kuhakikisha resources zinagawanywa sawa kwa manispaa zote zilizopo bila upendeleo wala bila kusahaulika hata kule ambalo hakuna resources nyingi..., hivi sasa hiyo Ilala / Jiji itakusanya resources kwa manufaa yake na kila manispaa kivyake wakati mwanzo ingekuwa makusanyo ni kwa manufaa ya manispaa zote kulingana na uhitaji.., Huu naweza kuuita ni muendelezo wa kuondoa nadharia ya Umoja ni Nguvu....,
 
Ndiyo kwa maswali matatu ya juu na hapana kwa lililobaki. Ukuaji wa kiuchumi uko palepale
 
Jiji ni Ilala tu
 
Hivi Bunge, Rais n.k. wana vyanzo gani vya mapato
 
Kwa mbaaali nimeanza kuelewa.....

Ila nina swali, kwa hiyo kumbe kuna wilaya nyingi tuu hapa Tanzania tunaweza kuzipa hadhi ya majiji? Mfano Moshi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…