Ufafanuzi: Kuvunjwa Halmashauri ya Jiji la Dar kuipandisha hadhi Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kuwa Jiji

Sasa nimeelewa, kwahiyo mwanzo ilikuwa wale madiwani wa halmashauri za kinondoni, ubungo, kigamboni, Ilala na temeke walikuwa wanaingia kwenye vikao kama wajumbe (madiwani) katika halmashauri ya Dar Es Salaam wakijairi yaleyale waliyoyajadiri katika halmashauri zao.
Kama sijaelewa naomba kukosolewa
 
umeanza vinzuri kabisa....but mwishoni ukaharibu..pale uliposema "jiji la dar ni sehemu yote ya Ilala tu". Hii siyo kweli kabisa...Kama ulivyosema wewe mwenyewe kuwa hadhi ya juu kabisa ya halmashauri ni jiji...na kwa kuwa Ilala ndio iliyopqndishwa hadhi na kuwa jiji, maana yake jiji hilo ambalo ndio iliyokuwa manispa ya Ilala....ina cover manispa zote...yani manispa za kinondoni,Ubungo,Tameke na kigamboni zitakuwa zinaongozwa na jij la dar...ambalo ni ndio ilikuwa manispa ya Ilala. Full stop.
 
KAMA UKO NJE YA KATA HIZI BASI KUNZIA 24.02.2021 JIHESABU UPO NJE YA JIJI LA DAR

1 Kisukuru
2. Jangwani
3. Minazi Mirefu
4. Buyuni
5. Chanika
6. Mchikichini
7. Zingiziwa
8. Kisutu
9. Kariakoo
10. Kiwalani
11. Majohe
12. Kimanga
13. Ukonga
14. Gerezani
15. Kivukoni
16. Tabata
17. Segerea
18. Liwiti
19. Ilala
20. Upanga MASHARIKI
21. Kipawa
22. Gongolamboto
23. Mchafukoge
24. Msongola
25. Kivule
26. Mnyamani
27. Kitunda
28. Kipunguni
29. Upanga MAGHARIBI
30. Buguruni
31. Kinyerezi
32. Bonyokwa
33. Pugu Stesheni
34. Pugu
35. Vingunguti
36. Mzinga

#FAHAMU Kiutawala Jiji Dar es Salaam lilikuwa limegawanyika katika Halmashauri sita za Serikali za mitaa ambazo ni:

1. Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam
2. Halmashauri ya Manispaa ya Temeke
3. Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni
4. Halmashauri ya Manispaa ya Ilala
5. Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo
6. Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni

SASA Ukiangalia hapo juu kulikuwa kuna chombo tu kinaitwa HALMASHAURI YA JIJI LA DAR ES SALAAM Lakini chombo hicho hakikuwa na eneo rasmi la kiutawala kwa maana nyingine halmashuri ya jiji haina ARDHI inayoitawala, kwa maana hiyo inategemea vyanzo vya mapato kutoka halmashauri za manispaa .

Chombo hiki yaani HALMASHAURI YA JIJI ilikuwa ina Meya wake na baraza lake huku halina vyanzo vya mapato, LAKINI WALITENGA BAJETI, SASA SWALI UNAPEWAJE BAJETI HUKU MIRADI INAWEZA KUHUDUMIWA NA MANISPAA ZENYEWE?

Hivyo kulikuwa na matumizi mabaya ya pesa kwa kuwa ni kama unampa MTU pesa hana matumizi nayo.

SASA kilichofanyika nikuvua KOFIA ya HALMASHAURI YA JIJI na kuipa ILALA.

Na manispaa za KIGAMBONI, KINONDONI, UBUNGO, TEMEKE Zitabaki kama manispaa.

Mchambuzi wa Maswala ya Kisiasa Michael Kosmas Sr.
 
Hujui chochote:
ILala inaishia daraja la Sarenda.
Posta, kariakoo, jangwani vyote vipo Ilala
 
Majukumu ya Jiji Dar es salaam sasa yatasimamiwa na Halmashauri ya Jiji la Ilala na mengineyo halmashauri za Manispaa husika.
Ni kama ilivyo kwa Tanzania Bara ambapo majukumu yake yanasimamiwa na JMT na ya Zanzibar kubaki SMZ, kwa uelewa wangu.
 
Kwa hio kuna jiji LA ilala na jiji LA dar es salaam
Au dar es salaam ndiyo eneo lote LA ilala tu?
Sijajua litaitwa jiji la Ilala au Ilala ndio itakuwa Dar na halmashauri za manispaa ziwe mkoani[emoji28][emoji28][emoji28]
 
Ukizungumzia Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam unazungumzia Wilaya ya Ilala pekee.

Ila ukizungumzia mkoa wa Dar es Salaam unazungumzia muunganiko wa Wilaya za Temeke, Ubungo, Kigamboni, Kinondoni na Ilala
 
 
Sijajua litaitwa jiji la Ilala au Ilala ndio itakuwa Dar na halmashquri za manispaa ziwe mkoani[emoji28][emoji28][emoji28]
Mambo mbona yanaenda ovyo ovyo tu siku hizi au kwa vile sifatiliagi siasa
Na matatizo ya upumuaji yanaanza kipindi hichi cha mvua na baridi ni ugonjwa gani?

Mi sina chama Mzee nataka tu kuelewa
Kwa nini siku hizi hakuna kauli za moja kwa moja kuwa ni HIVi au VILE
 
Hotuba za papo hapo na hatua za kushtukiza.
Hili jambo sijui kama wameshauriana au mzee baba alipita mjini akaona maghorofa na akawaza kichwani navunja jiji teh teh
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…