Ufafanuzi: Kuvunjwa Halmashauri ya Jiji la Dar kuipandisha hadhi Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kuwa Jiji

We hata hujaelewa,
Ilala haitaziongoza Temeke, Kino, Kigamboni na Ubungo. Kila moja itajiongoza kivyake.

Ila mmoja ataitwa Jiji, wengine wataitwa Manispaa
 
Petro mchango wako ni mzuti sana.
Kabla ya jana Mhe. Rais hajavunja Halmashauri ya jiji la DSM; eneo la kijiografia la DSM ndio lilikuwa eneo la Utawala wa jiji la Dar es Salaam.

Ukubwa wa eneo la kiutawala jijini DSM lilikuwa sawa na eneo la kiutawala Mkoa wa DSM.

Kwa lugha rahisi sana, mpaka jana jiji la DSM kiutawala lilikuwa ndio Mkoa wa DSM kiutawala.
Jiji la Dar likijihusisha na masuala ya serikali za mitaa na Mkoa ujihusisha na masuala ya serikali kuu.

Jiji la DSM lilikuwa na manispaa 5
Manispaa ya ILALA
Manispaa ya Kinondoni
Manispaa ya Temeke
Manispaa ya Ubungo na
Manispaa ya Kigamboni.
Kwa kitendo cha Mhe. Rais kuvunja jiji la Dar es Salaam lilikokuwa na manispaa 5; sasa tunabakiwa na Jiji la Dar es Salaam ambalo linachukua eneo la kijiografia la iloyokuwa manispaa ya ILALA na mamlaka ya Utawala ya Iliyokuwa manispaa ya Ilala, ndio inakuwa jiji la Dar es Salaam.
Maana yake manispaa zinabaki 4 tu, Temeke, Kinondoni, Ubungo na Kigamboni.

Aidha huenda mkurugenzi mmoja akakosa kazi.
Kwa kuwa aliekuwa Mkurugenzi wa jiji hana chake tena, na Mkurugenzi wa iliyokuwa manispaa ya Ilala anakuwa Mkurugenzi wa jiji; bila shaka aliekuwa mkurugenzi wa jiji la Dar akawa na kipindi cha mpito kukabidhi mafaili ya mali na madeni ya jiji la Daslam kwa manispaa zote 4 na jiji la "ILALA" ambalo kwa sasa linakuwa jiji la Daslam.

Hongereni Ilala kwa kuwa Daslam.
 
Yaani Mtu aliyeko Biafra yeye hayuko kwenye JIJI ila aliyeko Chanika MVUTI yuko kwenye JIJI.Aliyeko Msasani hayuko kwenye JIJI ila aliyeko Mchikichhini yuko kwenye JIJI ama sio hivyo Bwana Mkubwa?Nafikiri sasa inabidi ramani na mipaka ya jiji iwekwe upya na baadhi ya maeneo yaende kwenye halamashauri na baadhi ya maeneo yaingizwe kwenye JIJI.Ni maono yangu tu ili mipango iende sawa
 
Kifupi n hv Ilala ndo imekua ikitoa pato kubwa sana kuliko wilaya yeyote Mjin Dar.. sas wameamua kuichuku ilala ili waweze kucontrol hzo hela kwa kisingzio cha halmashauli ya jiji.. datz it.! OVER
 
Sasa Mayor wa jiji ndio kazi kwisha au?
Ambae alitakiwa kuwa Mayor wa Ilala atakuwa Mayor wa Jiji la Dar es Salaam.

Huko nyuma Dar ilikuwa na ma-mayor 5 kutoka kila manispaa na huyu wa 6 anaeongoza jiji.

Kwa sasa Mayor wa jiji hatakuwa akiongoza manispaa zilizobakia kama kule nyuma.
 
Mkoa wa Mwanza una Wilaya 7
Nyamagana (ndio jiji la Ng'wanza)
Ilemela (manispaa ya Ilemela)
Misugwi (halmashauri ya wilaya ya Misugwi)
Ukerewe (halmashauri ya wilaya ya Ukerewe)
Kwimba (halmashauri ya wilaya ya Kwimba)
Magu (halmashauri ya wilaya ya Magu)
Sengerema Wilaya ikiwa na Halmshauri 2
Halmashauri ya wilaya ya Sengerema na Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa.
 
Kanzu jipya shekh yule yule
 
Hili swala sio geni mfano jiji la Mwanza linaundwa manispaa tatu ilemela,Nyamagana na kisesa(mpya) lakini kiutalawa Nyamagana ndo jiji na inaeleweka vizuri ila ukija mgeni uwezi elewa mipaka ya jij .
 
Kwa hiyo kwa utaratibu huu meya wa jiji atapatikana kutoka kwa madiwani wa Ilala tu?

Na je ana mamlaka na hizi Halmashauri zilizobaki?
 
Moja ya manufaa yake ni kulifanya Jiji la Dar es Salaam kuwa na sehemu yake mahsusi ya kiutawala tofauti na ilivyokuwa awali. Awali, jiji la Dar es Salaam ni kama lilikuwa likielea kuhusu eneo hasa la kiutawala.
Unataka kusema jiji la Dar es Salaam lilikuwa sawa na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kiutawala? Je, ni sawa kufikiri kwamba JPM anaifanya hoja ya "serikali Tatu" kuwa na mashiko zaidi?
 
Bado sijaelewa kwa maana hiyo Kinondoni,kigamboni,Ubungo,na Temeke siyo jiji la Dar es salaam tena?Kama ni hivyo hayo ni maamuzi ya ajabu sana.Kwa muono wangu huwezi kuondoa tatizo kwa kuongeza tatizo yaani leo jiji liishie pale keko,feri,jangwani au salendar Bridge au mimi ndio sielewi.

Kwanza kitendo cha kusema Muundo wa uongozi ufanane na majiji mengine ambayo ya na manispaa moja na mwanza tu ndio ina manispaa mbili sio sawa.

Dar es salaam ni complex na kilichopaswa kufanya ni kutengeneza Halimashsuri tendaji na ambayo ingekua ndio chombo cha maamuzi kwa manispaa zote na sio kufanya kama kweli ndio ilivyofanyika.

Anyway labda tuendelee kufanya utafiti juu ya miundo ya wenzetu kwenye mega na complex cities kama Dar es Salaam.Nimejaribu kuangalia Madrid ni kama wana Mayor mmoja na disricts kadhaa ambazo zinaunda Jiji la madrid.
 
Ndiyo. Jiji la Dar kwasasa ni Ilala tu
 
Dar es Salaam in its whole is still a city.
Ilala zimeenda ofisi za jiji tuu. Acheni Ujinga.
 
Halmashauri kuwa na eneo mahsusi ni faida. Kabla ya jana, Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ni kama ilikuwa ikielea huku mamlaka yalikuwa kwa kila Manispaa na maeneo yake
Utatuzi haukupaswa kuwa wa namna hii...

In fact, jiji la DSM lote (Kigamboni, Ubungo, Ilala, Temeke na Kinondoni) lilikuwa ni eneo la mji mmoja tu lenye wakazi (population) inayokadiliwa kuwa 6,400,000 (takwimu za mwaka 2020)...

Kiutawala Jiji likagawanywa ktk manispaa tano. DSM City Council ikabaki pekee yake independent kama chombo cha ku - oversee manispaa hizi tano...

In my opinion, utatuzi ulipaswa uwe wa kisheria na kimuundo zaidi ili kulipa mamlaka makubwa zaidi "Jiji la DSM" kuzimamia manispaa hizi tano ili ziweze ku - perform vizuri ktk kutoa huduma kwa wananchi...

Alichokifanya Rais, kwa maoni yangu, hajatatua changamoto na matatizo ya mkoa wa DSM ambalo by then likiitwa "Jiji la DSM" badala yake hii inaweza kuwa chanzo cha matatizo mengine...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…