Ufafanuzi: Kuvunjwa Halmashauri ya Jiji la Dar kuipandisha hadhi Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kuwa Jiji

Na kwakuongezea Dar inabaki kuwa mkoa wenye halamshauri ulizotaja hapo lakini ilala ikiwandio makao makuu yake. Watu wengi imewachanganya .
 
Acha upotoshaji usio na Tija.
Rejea taratibu za majiji yote duniani.
Ndicho kilichofanyika.
Iliyokua halmashauri ya jiji la DSM, Haikua na eneo la mamlaka hivo haikua na chanzo cha mapato kwaio tulikua tunagharamia kuendesha kitu kisichokuwepo.
Maeneo yote ya Dar mathalani
Ubungo, kibamba, mbezi beach, Tegeta mbagala nk bado ni sehemu ya jiji la Dar
Over.
 
Kwhyo wale walio nje ya Ilala tuwaite wamikoani!?
 
sasa ndo nmeelewa,
MFANO: ni sawa useme Moshi iwe jiji ila Mwanga, Same, na Rombo isiwe jiji. haiwezekani mkoa mzima wa Kilimanjaro uwe jiji ila Moshi pekee ndo inaweza ikawa jiji.

ni sawa Morogoro mjini iwe jiji ila Ifakara, Malinyi na Ulanga haziwezi kuwa jiji.

•Ni sawa Ilala kuwa jiji ila Temeke, Kinondoni na kigamboni haziwezi kuwa jiji.
kiufupi nmeelewa mkoa hauwezi kuwa jiji bali inayokuwa jiji ni manispaa au halmashauri, hivi ndivyo nlivyoelewa.
niko tayari kusahihishwa kama nmekosea
 
Huu UJINGA utalast kwa miaka 5 tu. Ifikapo Jan 2026 Rais mpya atatudisha hadhi ya Jiji la Dar es Salaam kwa kurudisha kwanza makao makuu toka Dodoma, na kulifanya Jiji liwe Kama zamani.

Huyu mrundi hana mapenzi na nchi yetu, Ni mtu wa KUVURUGA TU
 
Hapana, siyo upotoshaji. Ni mjadala tu na kila mtu ana haki ya kujadiliana na wenzake...

Ukisema hivyo, mwingine aweza kukuita hata wewe kuwa ni "mpotoshaji" kwa kuwa tu umetoa maoni yako kwa njia hii

Mimi kwa maoni yangu, DSM City Council iendelee kubaki kama chombo cha ku - oversee hizi mamlaka za manispaa zote tano...

Mapato ya uendeshaji yagharamiwe na hizi mamlaka tano...

Kama kuna changamoto, zitatuliwe kisheria na kimuundo kwa lengo la kuingozea kazi na mamlaka DCC...
 
Jiji litalazimika kuwa na special priority za kiujenzi ukivunja nyumba basi inayojengwa ni lazima iwe ya ghorofa nk nk
pia si jambo la kufurahia sana maana huenda ndani ya jiji hilo wanyonge wakashindwa kuishi humo due to living cost mfano unapoisikia new york city ogopa sana kila kitu ni ghalimpaka ilibidi tukimbilie harlem uswekeni kwa wahuni kupata cheap houses
 
Mkuu, Jiji la Dar es Salaam la sasa ni Wilaya ya Ilala tu
Mkuu hapa mwishoni unachanganya, tuchukue mfano kuna mikoa inaperform kuliko mingine : mfano Mwanza,

Kwa kufuatisha sentensi yako unamaanisha

"Mkuu, Nchi ya Tanzania kwa sasa itakuwa ni mkoa wa Mwanza tu?
 
Huu mfumo wa jiji huko huku Mwanza jiji tumeisha zoea ndo maana tunakimbilia kujenga manispaa ya Ilemela,Misungwi na manispaa mpya ya kisesa.Mwanza jiji(nyamagana manispaa) inasheria zake ukijenga nyumba ambayo sio gorofa ni nyundo tu.Ila ndo mabadiliko lazima tukubali.
 
Na kwa hivyo hatutakuwa na mkuu wa Wilaya ya Ilala? Maana wilaya sasa imefutwa... Au?
 
KWAHIYO CHANIKA IPO JIJINI DAR ES SALAAM WAKATI MIKOCHENI IPO MANISPAA YA KINONDONI....DAH
 
Ukizungumzia Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam unazungumzia Wilaya ya Ilala pekee.

Ila ukizungumzia mkoa wa Dar es Salaam unazungumzia muunganiko wa Wilaya za Temeke, Ubungo, Kigamboni, Kinondoni na Ilala
Uko sahihi sana
 
Hili swala sio geni mfano jiji la Mwanza linaundwa manispaa tatu ilemela,Nyamagana na kisesa(mpya) lakini kiutalawa Nyamagana ndo jiji na inaeleweka vizuri ila ukija mgeni uwezi elewa mipaka ya jij .
Jiji la Dar es Salaam lilipata hadhi ya kuwa Jiji tarehe 9.12.1961 siku ya Uhuru na wakati huo Kaskazini likiishia Salendar Bridge, Magharibi Magomeni Mapipa na Kusini Temeke pembeni mwa Barabara ya Airport, eneo likiitwa Ilala wakati huo mpaka leo. Ilichukua miaka kama miwili au mtatu kuandaa Muundo wa Jiji na Mfumo wa Utawala, wakati huohuo Kinondoni na Temeke zikiendelea kukua na kuingizwa kwenye Muundo wa Jiji wenye Wilaya Tatu. Kwa sababu ya Barabara ya Morogoro, Ilala, ikakua haraka sana kuelekea Kimara na Kigamboni nayo ikiwa sehemu ya Temeke, siku za karibuni ikakua haraka sana ikalazimu Wilaya hizi mbili zigawanywe kupata Wilaya ya Ubungo na Kigamboni kufanya Jiji kuwa na Wilaya Tano. Jiji lilifanywa Mkoa wa Wilaya 5 na kuongoza shughuli zake kama Mikoa na Wilaya zingine nchini, Jiji nalo likawa na Muundo na Mfumo wake wa Utawala ambao ndo umefikisha Jiji kutambuliwa Kimataifa kuwa ni moja ya Majiji 10 yanayokua haraka sana. Kwa kifupi hayo ni mafanikio makubwa ya kupongeza siyo ya mtu mmoja kubeza na kufanya mabadiliko kwenye Jukwaa la kisiasa. Mabadiliko wakati mwingine ni lazima yafanyike ikibidi lakini lazima yalete matokeo chanya, ila mabadiliko yasipofanywa ikibidi kwa utashi wa mtu, yatakuja yenyewe yakileta matokeo hasi. Awamu ya Tano inaogopa mabadiliko, mafanikio yake ni maneno na sifa tu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…