DOMINGO THOMAS
JF-Expert Member
- Feb 16, 2023
- 365
- 365
Hapa tunarudi nyuma kidogo kabla ya kuanza kutumika kikokotoo cha Asilimia 33% kwenye kiinua mgongo na asilimia 67% kwenye pensheni ya kila mwezi, kulikuwa na mifuko 5 ambayo kila mfuko ulikuwa na Formula yake kwenye ukokotoaji mafao ya uzee ambapo :-
1. LAPF na PSPF ilikuwa ni asilimia 50% kwenye kiinua mgongo na asilimia 50% kwenye malipo ya kila mwezi (Monthly pension)
2. PPF, NSSF na GEPF ilikuwa ni asilimia 25% kwenye kiinua mgongo na asilimia 75% kwenye malipo ya kila mwezi
Kwa kauli hii ya waziri wa fedha Dkt. Mwigulu Nchemba - 13/06/2024.
1. Kwa walio kuwa wanachama wa LAPF na PSPF wao kwa sasa watalipwa asilimia 40% kama kiinua mgongo kutoka asilimia 33%, na Malipo ya kila mwezi yatakuwa asilimia 60% sio tena asilimia 67%.
2. Kwa walio kuwa wanachama wa GEPF, NSSF na PPF wao kwasasa watalipwa asilimia 35% kama kiinua mgongo na sio tena asilimia 33% na Malipo ya kila mwezi kwa sasa yatakuwa ni asilimia 65% na sio tena asilimia 67%.
3. Na kwa-walio kuwa wanachama wa PPF, GEPF, PSPF na LAPF (PSSSF) kabla mifuko kuungana na baada ya kuungana waka-hamia NSSF, na walio kuwa NSSF kabla mifuko kuungana na baada ya kuungana waka-hamia PSSSF hawa wanatumia Totalization formula.
NOTED
Kauli hii bado haija-anza kufanya kazi, mpaka pale miongozo na taratibu zitakapo tolewa.
Imeandikwa na
Thomas Ndipo Mwakibuja.
Social Protection Expert