Hali hii haina afya na hasa kwa serikali ya SSH na washirika wake:
1. Jaji kakubaliana na upande wa utetezi kuwa hati ya mashtaka ni batili.
2. Jaji badala ya kutumia busara kuonyesha haki inatendeka kachagua kuwa upande wa mashtaka ili walete nyingine.
Effectively kutokea hapo na katika mazingira haya:
3. Mh. Mbowe yuko ndani pasipokuwa na hati ya mashtaka.
4. Mh. Mbowe yuko ndani kinyume cha sheria na kinyume cha katiba.
Mh. Mbowe kamlalamikia jaji "in person" wasiwasi uliopo kuhusiana na kutenda haki yakiwamo anayotuhumiwa nayo jaji huyu:
5. Jaji kakubaliana na hoja za Mh. Mbowe kujitoa.
Katiba inaendelea kusiginwa chini ya macho ya tuliyempa dhamana ya kuhakikisha inalindwa. Yeye mwenyewe akiwa kwenye "tour" kama zilivyo "Tour de France" au "Tour de Rwanda."
Mwendelezo huu wa kubambikiza watu kesi na kuweka majaji mahsusi wa kuhakikisha mahitajio yenu serikali yanatimilika kinyume cha katiba, kunaendeleza kukuzwa kwa chuki baina ya watu na serikali na baina ya watu na watu.
SSH na washirika wako mnako tupeleka siko tulikokubaliana. Kwamba hamuwajibiki kwetu bali mna ajenda zenu zenye maslahi yenu binafsi?
Hali hii bado tu haiwafikirishi?
Cc:
Jumbe Brown zandrano