Ufafanuzi wa leseni za Magari ya Barabarani

Ambivert88

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2022
Posts
3,609
Reaction score
6,388
Wakuu.

Nimekuja kwenu hapa wale wenye ujuzi wa leseni za magari nina maswali naomba majibu kupatiwa majibu, najua natakiwa kwenda kuwauliza askari wa barabarani au TRA Tanzania ila sasa naomba majibu yenu hapa kwanza

Swali namba 1:
Leseni ya kuendesha pikipiki zipo makundi kuna Class A, A1, A2 na A3 sasa nikijifunza kuendesha pikipiki najaziwa zote hizo kwenye leseni yangu yaan Class A, A1, A2 na A3 au najaziwa moja moja?

Swali namba 2:
Leseni ya kuendesha magari ya Umma zipo makundi kuna Class C, C1, C2, na C3, sasa nikisomea Class C1 ambayo ipo juu ya C2 na C3 je najaziwa zote kwenye leseni yangu yaan C1, C2 na C3 au najaziwa moja tu?

Soma pia: Namna rahisi ya kupata leseni ya udereva

Naombeni ufafanuzi wenu wakuu kwa faida ya wengine pia.
 
Una ujuzi wa kuendesha gari/mashine/pikipiki ya aina fulani basi omba leseni husika...
 
Mkuu
Vuta Subira Kidogo Wakati
Kamanda Anakuja Na Majibu
 
A - Leseni ya kuendesha pikipiki yenye kg 230 ambayo uwezo wake unazidi 125cc.

A1- Leseni ya kuendesha pikipiki yenye uwezo chini ya 125cc au 230Kg.

A2 - Leseni ya kuendesha vyombo vya moto vyenye miguu 3 au 4.

A3 - Leseni ya kuendesha pikipiki ambao uwezo wake hauzidi 50cc

B - leseni ya kuendesha gari aina zote za isipokuwa pikipiki na magari ya biashara.

C - Leseni ya kuendesha yenye uwezo wa kubeba abiria 30 na zaidi. C1 - leseni ya kuendesha magari ya umma yenye uwezo wa kubeba abiria wasiopungua 15 lakini wasizidi 30

C2 - Leseni ya kuendesha magari ya umma na yenye uwezo wa kubeba abiria si chini ya 4 na wasiozidi 15.

C3 - Leseni ya kuendesha magari ya huduma za umma yenye uwezo wa kubeba abiria 4 au chini ya hapo

D - Leseni ya kuendesha kila aina ya gari isipokuwa pikipiki, magari yenye ujazo mkubwa na magari ya umma.

E - Leseni ya kuendesha kila aina ya magari isipokuwa pikipiki na magari ya abiria (magari makubwa ya mizigo)

F - Leseni ya kuendesha magari makubwa au ya migodini.

G - Leseni ya kuendesha magari ya shamba au ya kuchimbia.

H – Leseni ya muda kwa madereva mwanafunzi, mara nyingi hutambulika kama ‘Learner’
 
Safi sana mkuu haya ni maelezo mazuri sasa tujibu swali pale juu mfano nina leseni Class D nataka kusomea Class C1 je nikimaliza kusoma udereva kwenye kujaziwa leseni yangu najaziwa Class C1, C2 na C3 au najaziwa Class C1 tu?

Na kwenye pikipiki nikijifunza kuendesha Class A najaziwa zote Class A, A1, A2 na A3 au najaziwa Class A tu?
 
Mku, dereva ndiye anayeomba aina fulani la daraja/madaraja kulingana na uwezo wake kwenye kumudu aina ipi ya chombo kama ilivyofafanuliwa. Huwa TRA hawakujazii kwa utashi wao bali kulingana na ulichoomba, ulichosomewa na ulivyojaribiwa trafiki.

Mara nyingi dereva mwenye uwezo wa kuomba daraja C lolote, anaweza kumudu magari ya daraja D na B.

Unapoomba leseni huwa haujaziwi pasipo matakwa ya mwombaji, wewe mwombaji ndio unayeomba upewe leseni zenye madaraja yapi.

Ipo dhahiri kama una uwezo wa kuomba daraja A basi unaweza ukaomba pia A1, A2, A3.
 
Hapa mkuu nimepata mwanga kidooogo, ila bado nina maswali kwa hio inabidi nikajaze form ya maombi TRA Tanzania ?

Naomba ufafanuzi na hapo na hio form hua unaandikaje kwamba unataka leseni yako ijaziwe Class A, A1, A2 na A3 maana si wanajaza km ulivyoomba au?

Na kwenye magari nikisomea udereva Class C1 kwenye form ile ya maombi naijaza nataka leseni yangu ijazwe Class C1, C2 na C3 si ndio hivyo au unamaanisha nini?
 
A - Leseni ya kuendesha pikipiki yenye kg 230 ambayo uwezo wake unazidi 125cc.

A1- Leseni ya kuendesha pikipiki yenye uwezo chini ya 125cc au 230Kg.

A2 - Leseni ya kuendesha vyombo vya moto vyenye miguu 3 au 4.

A3 - Leseni ya kuendesha pikipiki ambao uwezo wake hauzidi 50cc

B - leseni ya kuendesha gari aina zote za isipokuwa pikipiki na magari ya biashara.

C - Leseni ya kuendesha yenye uwezo wa kubeba abiria 30 na zaidi. C1 - leseni ya kuendesha magari ya umma yenye uwezo wa kubeba abiria wasiopungua 15 lakini wasizidi 30

C2 - Leseni ya kuendesha magari ya umma na yenye uwezo wa kubeba abiria si chini ya 4 na wasiozidi 15.

C3 - Leseni ya kuendesha magari ya huduma za umma yenye uwezo wa kubeba abiria 4 au chini ya hapo

D - Leseni ya kuendesha kila aina ya gari isipokuwa pikipiki, magari yenye ujazo mkubwa na magari ya umma.

E - Leseni ya kuendesha kila aina ya magari isipokuwa pikipiki na magari ya abiria (magari makubwa ya mizigo)

F - Leseni ya kuendesha magari makubwa au ya migodini.

G - Leseni ya kuendesha magari ya shamba au ya kuchimbia.

H – Leseni ya muda kwa madereva mwanafunzi, mara nyingi hutambulika kama ‘Learner’
Umefafanua vizuri sana mkuu
 
Kulingana na uelewa wangu kwenye hayo mambo
*Kwenye madaraJa "A
Ni madaraja ya pikipki ila ukiendq kusoma kuendesha pikipiki unapewa daraja "A plain ila ukisoma na Bajaj ynapewa madaraja yote ya "A

*Na kuhusu madaraja ya "C¹
Kuhusu lazima uwe umesoma psv(public service vehicle,au daladala)au vip watakupa madaraja yote ya c¹ c² c³ ila ispokuwa c plai ambayo ni ya mabus
 
Mku, dereva ndiye anayeomba aina fulani la daraja/madaraja kulingana na uwezo wake kwenye kumudu aina ipi ya chombo kama ilivyofafanuliwa. Huwa TRA hawakujazii kwa utashi wao bali kulingana na ulichoomba, ulichosomewa na ulivyojaribiwa trafiki.

Mara nyingi dereva mwenye uwezo wa kuomba daraja C lolote, anaweza kumudu magari ya daraja D na B.

Maelezo ya Makundi​

  1. Daraja A: Leseni hii inahusisha pikipiki zenye uwezo mkubwa wa injini, ambazo zinaweza kuwa hatari ikiwa dereva hana ujuzi wa kutosha.
  2. Daraja A1: Hii ni leseni inayohusisha pikipiki ndogo, ambayo ni maarufu miongoni mwa vijana.
  3. Daraja A2: Inahusisha pikipiki za magurudumu matatu na manne, ambazo mara nyingi hutumiwa katika usafiri wa umma.
  4. Daraja B: Leseni hii inaruhusu waendesha magari madogo, ambayo ni maarufu kwa matumizi binafsi.
  5. Daraja C: Inahusisha magari makubwa kama lori na mabasi, ambayo yanahitaji ujuzi maalum wa udereva.
  6. Daraja D: Hii ni leseni inayohitajika kwa waendesha magari yanayobeba abiria wengi, ikiwa ni pamoja na mabasi.
  7. Daraja E: Inatumika kwa waendesha magari maalum kama vile yale yanayotumiwa katika shughuli za ujenzi au kilimo.
  8. Daraja F: Hii ni leseni inayohitajika kwa waendesha magari yanayokokota trela.
  9. Daraja G: Inajumuisha magari yanayotumiwa katika shughuli za shambani na migodini.
  10. Daraja H: Leseni hii ni ya muda inayotolewa kwa wanaojifunza udereva kabla ya kupata leseni rasmi.
 
Mku, dereva ndiye anayeomba aina fulani la daraja/madaraja kulingana na uwezo wake kwenye kumudu aina ipi ya chombo kama ilivyofafanuliwa. Huwa TRA hawakujazii kwa utashi wao bali kulingana na ulichoomba, ulichosomewa na ulivyojaribiwa trafiki.

Mara nyingi dereva mwenye uwezo wa kuomba daraja C lolote, anaweza kumudu magari ya daraja D na B.

Umuhimu wa Leseni za Udereva​

Leseni za udereva zina umuhimu mkubwa katika jamii zetu kwa sababu zifuatazo:

  • Usalama Barabarani: Leseni zinahakikisha kuwa waendesha magari wana ujuzi wa kutosha wa kuendesha salama, hivyo kupunguza ajali barabarani.
  • Kisheria: Kuwa na leseni ni kigezo cha kisheria kinachomruhusu mtu kuendesha gari bila kukiuka sheria.
  • Ushauri wa Kitaaluma: Watu wengi wanahitaji leseni ili kufanya kazi katika sekta mbalimbali kama vile usafirishaji na huduma za abiria.

Mchakato wa Kupata Leseni​

Ili kupata leseni ya udereva nchini Tanzania, mtu anahitaji kufuata hatua zifuatazo:

  1. Kujiandikisha kwenye chuo cha udereva: Mtu anapaswa kujiandikisha katika chuo kinachotambulika na Mamlaka husika.
  2. Kufanya mtihani wa nadharia: Baada ya kumaliza mafunzo, mteja anahitaji kufanya mtihani wa nadharia kuhusu sheria za barabarani.
  3. Kufanya mtihani wa vitendo: Ikiwa atafaulu mtihani wa nadharia, atapewa nafasi ya kufanya mtihani wa vitendo.
  4. Kupata leseni: Baada ya kufaulu mitihani yote, mteja atapata leseni yake rasmi.
 
Mku, dereva ndiye anayeomba aina fulani la daraja/madaraja kulingana na uwezo wake kwenye kumudu aina ipi ya chombo kama ilivyofafanuliwa. Huwa TRA hawakujazii kwa utashi wao bali kulingana na ulichoomba, ulichosomewa na ulivyojaribiwa trafiki.

Mara nyingi dereva mwenye uwezo wa kuomba daraja C lolote, anaweza kumudu magari ya daraja D na B.

Vigezo vya Kuomba Leseni​

  • Kuwa na umri wa miaka 18 au zaidi.
  • Kuwa na cheti cha kumaliza mafunzo kutoka chuo cha udereva.
  • Kupitia mtihani wa afya kubaini uwezo wake wa kuendesha gari.

Changamoto katika Upatikanaji wa Leseni​

Katika baadhi ya maeneo nchini Tanzania, changamoto mbalimbali zimekuwa zikijitokeza katika upatikanaji wa leseni za udereva:

  • Gharama za Usafiri: Watu wengi wameshindwa kupata leseni kutokana na gharama kubwa za usafiri kwenda miji mikubwa kama Musoma au Dar es Salaam ambapo huduma hizo zinapatikana.
  • Foleni Ndefu: Wakati mwingine watu wanakutana na foleni ndefu wanapofuatilia huduma hizi, jambo ambalo linawakatisha tamaa.
Madaraja ya leseni za udereva ni muhimu sana katika kudhibiti usafiri nchini Tanzania. Kila kundi lina vigezo vyake ambavyo vinahakikisha kuwa dereva ana uwezo sahihi wa kuendesha aina fulani ya gari.

Kwa hivyo, ni muhimu kwa kila mtu anayepanga kuendesha gari kuwa na leseni sahihi ili kuhakikisha usalama wao na wengine barabarani.
 
*Na kuhusu madaraja ya "C¹
Kuhusu lazima uwe umesoma psv(public service vehicle,au daladala)au vip watakupa madaraja yote ya c¹ c² c³ ila ispokuwa c plai ambayo ni ya mabus
Hapa mkuu nimekuelewa vizuri sana na umeweza kunijibu swali kwa uzuri kabisa, pokea maua yako mkuu
 
Back
Top Bottom