Mimi nilisema juzi kwenye mechi ya Yanga na Azam nikaonekana sina hoja. Kama pesa ipo, kwa nini uwanja usifungwe kabisa ili focus iwe kwenye kufanya huo ukarabati na kuumaliza mapema. Hivi vimechi vidogo sijui Yanga vs Azam, Yanga vs.
Singida vingeendelea kuchezewa huko huko Chamazi. Hii itawawezesha kuwahisha hatua kadhaa za ukarabati ili mechi za kimataifa zikianza, at least uweze kutumika wakati ukarabati maeneo mengine ukiendelea.
Yaani tunashindwa kufanya maamuzi madogo kama haya kweli, kila kitu tunataka kufurahisha watu? Hakuna ukarabati wa maana unaweza kufanyika wakati uwanja unatumia kila baada ya siku mbili, tuache kudanganyana.