JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 685
- 1,124
Kadiri janga la Virusi vya Corona (COVID-19) linavyoendelea, ndivyo pia wingi wa habari zinazohusiana na kusababisha kile kinachoitwa "infodemic'’ unavyoongezeka.
Taarifa potofu na za uongo kuhusu COVID-19 zinasambazwa kwa haraka sana mtandaoni na zinaweza kuathiri watu wengi. Hakuna chanzo kimoja, na watu tofauti wanasambaza taarifa kwa nia tofauti ili kutimiza malengo na ajenda zao wenyewe. Kwa mfano, baadhi ya watu wanatumia majukwaa ya mtandaoni kueneza nadharia za kupotosha wakidai kuwa COVID-19 ni silaha ya kibaolojia, kwamba COVID-19 haipo, huku wengine wakidai kuwa COVID-19 ni sehemu ya mpango wa kudhibiti idadi ya watu duniani n.k
Wengine wanaeneza uvumi wa matibabu ambayo hayajathibitishwa kisayansi kama vile kula malimau na tangawizi nyingi, kujifukiza (nyungu) n.k. Wengine wanatumia janga la COVID-19 kwa manufaa ya kifedha kama vile kuuza mitishamba ambayo wanadai inatibu COVID-19 n.k.
Kwa kuzingatia kuibuka kwa yote haya, Shirika la Afya Duniani (WHO), wataalamu wa Afya pamoja na mashirika ya yanayoshughulika na afya yamefafanua mambo yote ambayo yanaweza kuleta nkanganyiko kwa jamii.
Hapa chini ni mjumuiko wa ufafanuzi kuhusu masuala anuai yahusuyo COVID-19 yaliyotolewa ufafanuzi na vyanzo vya kuaminika.
1. #COVID19 - Chanjo ya COVID-19 haisababishi usumaku mwilini
2. #COVID19 - CDC: Hakuna madhara kupata chanjo za maradhi mengine kabla au baada ya chanjo ya COVID-19
3. #COVID19 - CDC: Chanjo za COVID-19 hazitumiki kufuatilia mienendo ya watu
4. #COVID19 - CDC: Pata chanjo ya COVID-19 iliyoidhinishwa katika eneo unaloishi
5. #COVID19 - Chanjo za COVID-19 hazisababishi mimba kuharibika
6. #COVID19 - Chanjo za COVID-19 zenye virusi hai (viral vector vaccines) hazisababishi mtu kupata CoronaVirus
7. #COVID19 - Chanjo za COVID-19 hazisababishi kuibuka kwa aina (variants) mpya za Coronavirus
8. #COVID19 - CDC: Hakuna madhara kupata chanjo za maradhi mengine kabla au baada ya chanjo ya COVID-19
9. #COVID19 - Chanjo za COVID-19 zimepitia hatua muhimu za kiusalama
10. #COVID19 - Chanjo ya COVID-19 haiondoi uwezo wa kupata watoto
11. #COVID19 - CDC: Hakuna madhara kupata chanjo za maradhi mengine kabla au baada ya chanjo ya COVID-19
12. #COVID19 - Chanjo za COVID-19 haziathiri DNA kwa namna yoyote
13. #COVID19 - Chanjo ya COVID-19 ni salama kwa wagonjwa wa Saratani
14. #COVID19 - Pata chanjo hata baada ya kuugua na kupona COVID-19
15. #COVID19 - Chanjo za COVID-19 hazina madhara kwa mama anayenyonyesha
16. #COVID19 - Chanjo ya Covid-19 haiathiri nguvu za kiume