Ufahamu kuhusu kulangua mpunga.

Ufahamu kuhusu kulangua mpunga.

Mambo ni moto, msimu huu lazima nikisanue kwenye mpunga, nalima mwenyewe, tena kando kando ya ziwa mvua ikizingua napiga irrigation
Hiyo safi sana nyand'one! Hongera sana Kiongozi mwenzangu!
 
Mkuu Morogoro mavuno yanaanza mwezi wangapi kama una taarifa .??
Na hiyo ndoo ya laki mbili ikoje.??
Na kingine bei za kuhifadhi zinakuwaje kwa gunia moja.?
Msimu umeshaanza mwezi huu wa sita.

Ndoo hii ni kubwa ukilinganisha na ndoo za kawaida za lita 20 hivyo ukiitumia kupimia mpunga wakati wa kununua inatoa kilo nyingi zaidi za mchele baada ya kukoboresha.

Kuna sehemu zingine kuhifadhi ni bure, ili mradi tu ukitaka kukoboa utumie mashine ya mwenye ghara lakini pia hata ukitozwa hela haizidi 1500 kwa gunia! Experience yangu mie nimekuwa nikiweka bure!
 
Mdanganye,, siku hizi Wasukuma wanatumia ndoo zao kama hutaki tembea! Pia chunga sana siku hizi wanadaiwa kuonesha mashamba, ama sivyo unanyang'anywa mpunga wote! Hawa Usukumani wanaitwa "Bagalagaja"
Mkuu labda kama hawana shida na pesa! Wakulima wamekuwa wakiendelea na wataendelea kuuza tu. Labda cha kuwasaidia wawe wanauza kwa kilo badala ya kuuza kwa kupima kwenye vyombo hivyo. Lakini kutokana na kukosa elimu juu ya hilo wachache watakaoelewa au kuitikia hilo hasa kwa upande wa mpunga.

Mfanyabiashara wa mazao huwa anatembea na ndoo yake ya kupimia au kama ni mzani kwa wale wachache wanaonunua kwa kupima kilo anakuwa na mzani wake.

Na hii ya kuonesha mashamba haipo kwa mazao ya chakula na inawezekana kwa mazao ya biashara tu ambayo ni ya msimu kiasi kwamba msimu wa kuuza ukipita basi unabaki nayo ndani huna wa kumuuzia tena hadi msimu ujao..
Mazao ya chakula ni ngumu maana ni biashara huria kwa kila mtu hasa ambako serikali huwa hainunui mazao hayo na ukizingatia ni mikoa michache sana ambako serikali ina maghara ya chakula kuweza kununua na hivyo kucontrol bei ya soko, sehemu kubwa mavuno ya mwaka huo ndiyo yanadetermine bei iweje na wala hakuna bei elekezi! Na ukitaka mazao yauzwe kwa bei ya juu kwa wanunuzi, unawaumiza wananchi hao hao wa sehemu zingine hasa sehemu ambazo zina upungufu wa chakula maana nao wataenda wauziwe kwa bei kubwa kucompasate gharama zingine.
Na ukumbuke hakuna msimu wa kuuza mazao ya chakula zaidi ya kuwepo kwa msimu wa kuvuna tu!

Na ukitaka serikali igombanishwe na wananchi basi waweke utaratibu wa kuwa hakuna kununua mazao ya chakula hadi msimu wa serikali ufunguliwe hapo watatafuta lawama za bure maana misimu huwa inachelewa kufunguliwa wakati shida kwa watu zipo kila siku na wanahitaji pesa immediately tu wanapoona mazao yao yamekuwa tayari kuvunwa.

Mfano angalia msimu wa pamba kanda ya ziwa hadi sasa haujafunguliwa kutokana na kuchelewa huko baadhi ya wakulima wameamua kuuza pamba yao kwa walanguzi ili angalau wajipatie fedha kukidhi mahitaji yao japokuwa wanaibiwa lakini hawana namna inabidi wauze tu.

Kwa hiyo shida ndiyo zinawafanya wakulima wauze mazao mapema wakati mwingine hata kwa bei ya chini hasa mazao yasiyokuwa na bei elekezi na hata yenye bei elekezi msimu ukichelewa kufunguliwa wananchi wanalazimika kuuza kwa bei ya chini ili wakidhi mahitaji yao.
 
Morogoro kubwa chief, saivi wanauzaje mpunga kwa hiyo ndoo.?
Na je mpunga upon mwingi?
Ifakara vijijini maeneo ya Mchombe, Ikule, Ilungusha, Chita.

Debe kati ya Sh 6500 hadi 7500
Mpunga unapatikana kwa wingi wewe tu na hela yako tena saivi wakulima wengi ndio wanavuna ila kwa hali ilivyo utapanda bei mda si mrefu maana mwanzoni mwa mwezi wa 6 debe lilikuwa 6000 lakini saivi imefikia bei niliyoitaja na wakati ilikuwa inategemewa kushuka kutokana na wakulima wengi saivi kuwa wanavuna lakini haijashuka imeongezeka.

Sababu ya kuongezeka kwa bei ni kuwa baadhi ya mikoa mfano Shinyanga na Tabora hawajapata mpunga vizuri kutokana na mvua kuwa za shida hivyo kuna wafanyabiashara wengi wanakuja kukusanya mpunga na kusafirisha kupeleka mikoa ambayo haijapata mavuno ya kutosha japo wafanyabiashara wengi wa mikoa niliyoitaja huwa wanaenda kununulia Mpanda inapotokea upungufu katika mikoa yao ila scrambling ya mpunga kwa Ifakara ipo kutokana na sababu nilizozitaja za mavuno haba baadhi ya sehemu nchini.

Kwa mwaka huu Ifakara wamepata vizuri kuliko mwaka jana. Mwaka jana debe tulinunua kwa 6000 pamoja na kwamba walivuna kidogo kwa sababu maeneo mengine pia ya nchi yalikuwa yamepata mavuno vizuri. Mwaka huu pamoja na kuwa wamevuna vizuri lakini bei imepanda kutokana na baadhi ya sehemu nchini kutopata mavuno ya kutosha!
 
Poa poa kiongozi kwa ufafanuzi mzuri
 
Biashara ya nafaka hususani mpunga ni nzuri ikiwa tu utafanya mambo yafuatayo;

1.Uvumilivu (kuweka stoo mpunga then uje kuuza mchele baadae au hata mpunga huohuo)

2.Uchaguzi mzuri wa mpunga (Kuna mbegu nyingine sio nzuri au mpunga kulowa maji wakati wa kuvuna baadae huwa unakatika sana ukiukoboa)

3.Ghala (Hakikisha una sehemu nzuri ya kuhifadhi mpunga ila usiharibiwe panya maana huwa wanaweza kula hata gunia moja likaisha)

Mwaka jana nilikuwa na gunia 30 za mpunga 15 nilipata hela nzuri kwakuwa mpunga ulikuwa fresh ila 15 nyingine niliuza kwa bei ndogo japokuwa sikupata hasara.

N.b; Ukizingatia hivyo vitu 3, ukauza bei nzuri sokoni utapiga sana hela mkuu, nataka nisifanye makosa tena najiandaa niingie porini.
Kwa nnavyoijua biashara ya mpunga wewe ujaifanya bado[emoji28] haipo rahisi hivyo
 
Duuh aisee nilikuwa nafikir hii biashara ni rahisi tu kwamba nanunua naweka stoo halaf naondoka kufanya shughuli zangu zingine miezi 3 mbele naenda kupiga faida tu.
Unaweza ukanunua makapi ukadhani umenunua mpunga
 
Tupe na wewe uzoefu wako/ Hoja zako kuhusu hii biashara, maan naona umempinga yule jamaa amabaye mi naona kaeleza fresh.
NB, Tafiti hupingwa na tafiti.
Manunuzi ya mpunga hayahitaji Elimu flani hasa kama ni mgeni,Unapokuwa mgeni kwenye swala la mpunga
1.Hakikisha unaenda kununua Mpunga na wanaofahamu namna ya ununuzi,(wanajua aina ya mpunga
2.Hili swala litakuepuka wewe kununua mpunga ulio na Biriani ama ulio na Mbigili,wazoefu huwa wanajua Mkulima gani ndio hulima mbegu nzuri na yupi hulima ya kawaida.
3.Utajigunza pia namna ya kununua mpunga..hapo juu wengi wameonglea sijui ndoo kuweka Mafuta ili ipanuke na janja nyengine...ila naomba niseme tu hizo ni mbinu za kizamani sana..wakulima sikuizi wana aina mbili za kukuuzia, wakati wa mpunga bei Rahisi
huwa wanauza kwa kupimiana kwenye Ndoo zao,na pindi mpunga umehadimika anaweza kukuuzia kwa Gunia moja kwa moja ujazo wa (Uzazi wa Mpango)
4.Na sio kweli kuwa mpunga utapata hasara kwa kuliwa na Panya..panya anaweza kula mpunga hta pishi moja asimalize sababu mpunga unawasha na kukata.
5.Kama utapata Muda nunua mpunga kule kule mitoni kipindi wanavyovuna inakuwa vizuri zaidi

MWISHO: Kama unataka anza biashara hii nenda kwanza kashinde Mashine ai
u iza Mchele maeneo ya mashine upate uzoefu kwanza. na si kwenda kichwa kichwa.
 
Kuna uwezekano ukanunua mpunga ambao haukuvunwa vzr au uliozama kwenye tope n.k hii n hasara kubwa mnoo utakapoukoboa utatoka vby na hivyo utauza kwa bei ya hasara so hyo inakata mtaj fastaa.
Changamoto ya pili, n kwamba kuna mpunga mwingne unakuwa n mwepesi sana ukiukoboa unatoa kg chache sn hivyo inapelekea kuporomosha matazamio yako ya faida na hadi kupelekea hasara.
Kwa ufupi n biashara ya leo unapata, kesho unakosa so unapofanya jiandae kwa hali hizo.
Biashara inayokupa uhakika wa pesa yako n ya kununua mchele moja kwa moja maana utaona ubora wake pia utakuwa na uhakika wa kg unazoingiza kwenye mzunguko hivyo kuifahamu faida halisi.

Ata mm hapo nimekuelewa ndugu
 
Usijalibu kununua mpunga hata siku moja, maana kwenye kukoboa unaweza ukazingua sana, nunua mchele ndugu
 
Usijalibu kununua mpunga hata siku moja, maana kwenye kukoboa unaweza ukazingua sana, nunua mchele ndugu
Siyo kweli. Maana Mchele unatokana na Mpunga wakulima hawauzagi Mchele.

Mchele hautunziki sana, issue ni umakini wakati wa kulangua.

People have been doing this business over decades.
 
Uzoefu ndio muhimu. Kama vp nunua kiwango kdg kwa mwaka huu ili kujifunzia changamoto za soko. Ukishakuwa comfortable msimu ujao unaongeza kiwango.

Ila usiweke mtaji wako wote kwenye huu msimu huu wa kwanza.
 
wafanya biashara wa mpunga wapo shamba humu ndani tunadanganya tu, nina experience 90% ya wakulima wa mpunga hata wanunuzi hawijui JF.
Ukitaka data za mpunga nenda shamba na mashineni na ukitaka kupata data za mchele nenda mashineni TU,
 
Safi sana. .mawazo mujarabu
Kuna uwezekano ukanunua mpunga ambao haukuvunwa vzr au uliozama kwenye tope n.k hii n hasara kubwa mnoo utakapoukoboa utatoka vby na hivyo utauza kwa bei ya hasara so hyo inakata mtaj fastaa.
Changamoto ya pili, n kwamba kuna mpunga mwingne unakuwa n mwepesi sana ukiukoboa unatoa kg chache sn hivyo inapelekea kuporomosha matazamio yako ya faida na hadi kupelekea hasara.
Kwa ufupi n biashara ya leo unapata, kesho unakosa so unapofanya jiandae kwa hali hizo.
Biashara inayokupa uhakika wa pesa yako n ya kununua mchele moja kwa moja maana utaona ubora wake pia utakuwa na uhakika wa kg unazoingiza kwenye mzunguko hivyo kuifahamu faida halisi.
 
Mhh mimi mbona sijaelewa hiyo ndoo ukiifanya hivyo ndio inakuwa ina saidia mechanism gani
mkuu siku hizi kuna ndoo za kupimia huo mpunga huko polini zimeshafanyiwa utundu kitaalamu ndoo moja inauzwa laki 2!!sio mchezo hata mkulima kuishitukia ni shida ila hizo nyingine za kutengeneza mwenyewe local wanazishitukia sana na utapelekwa hadi kwa mwenyekiti wa kijiji kwa uhujumu uchumi !!!tatizo la biashara ya kununua mpunga ni kwenye kuukagua ubora wake kwani huuoni unakuja kuukoboa baba ni chenga/biliani(rangi ya uvundo)tayari hasara tofauti na biashara ya. mchele unanunua kitu unachokiona.
 
Mkuu hiyo ni mkoa gani?

Back
Top Bottom