Ufahamu kuhusu nyota za angani

Ufahamu kuhusu nyota za angani

Napenda kujua kuwa, jua ni nyota inayotuwezesha dunia kuwa na uhai (najua Mungu ndiye anatoa uhai ila naamini nimeeleweka) Je hizo nyota nyingine kuna utafiti uliofanywa ukaonyesha kuwepo uhai kama kwenye nyota jua?
Swali zuri.

Sasa hivi wanasayansi za anga wote wamejikita kutafuta sayari katika majua (nyota) mengine kuona kama yanaweza kuwa na uhai. Tatizo ni kuwa wengi wao wanatafuta hali kama ya hapa duniani kwetu. Sio lazima uhai uwe kwenye vigezo vyetu (joto, maji, hewa, nk.)

Kunaweza kuwa na uhai mwengine ambao haufanani na wa kwetu (carbon-based). Inawezekana kabisa kuwa kuna viumbe ambao ni silicon-based na wanaweza kuishi kwenye hali ambayo sisi hatuwezi kuishi.
 
Sirius ni nyota ilioko kwenye Constellation Canis Major (Big Dog). Iko kwenye pua ya huyu mbwa.

Kama unasoma hili jibu sasa nimeweka picha ya Sirius ilipo sasa hivi Tanzania (DSM). Simama nje mwili wako ukiangalia kaskazini. Angalia juu (utosini) na utauona mwezi. Teremsha macho yako kidogo kuelekea kaskazini-magharibi na utaiona nyota moja yenye muanga mkubwa zaidi ya nyingine karibu. Hiyo ndio Sirius.

Kama hukuupata huu ujumbe muda muafaka, nipe siku na muda (usiku) utakapokuwa tayari kutoka nje na kuangalia angani (kusiwe na mawingu) na nitakutumia chart kukuelekeza uangalie wapi. Ukinipa mji itasaidia zaidi.
Asante kwa hii elimu Mkuu.
 
Nashukuru mkuu kwa jibu zuri
 
Elimu
Hii
Imenifanya
Niwaze
Zaidi
Kuhusu
Mwisho
Wa
Dunia
,jua
Ndio
Jehanam
Inayotajwa
,nafananisha
Matukio
Ya
Urushwaji
Wa
Maroketi
Ya
Anga
Mbali
,na
Safari
Ya
Watukufu
Ya
Kwenda
Mbinguni
Iliyotajwa
,huo
Unaitwa
Mhamo
Wa
Wanadamu
Wa
Jamii
Fulani
Kwenda
Sayari
Nyingine
.na
Hii
Itaja
Fanyika
Miaka
Mingiiii
Ijayo
,imean
Israel+
Itakapotwaaliwa
 
Sirius ni nyota ilioko kwenye Constellation Canis Major (Big Dog). Iko kwenye pua ya huyu mbwa.

Kama unasoma hili jibu sasa nimeweka picha ya Sirius ilipo sasa hivi Tanzania (DSM). Simama nje mwili wako ukiangalia kaskazini. Angalia juu (utosini) na utauona mwezi. Teremsha macho yako kidogo kuelekea kaskazini-magharibi na utaiona nyota moja yenye muanga mkubwa zaidi ya nyingine karibu. Hiyo ndio Sirius.

Kama hukuupata huu ujumbe muda muafaka, nipe siku na muda (usiku) utakapokuwa tayari kutoka nje na kuangalia angani (kusiwe na mawingu) na nitakutumia chart kukuelekeza uangalie wapi. Ukinipa mji itasaidia zaidi.
Pua
Ya
Huyu
Mbwa
Maana
Yake
 
ImageUploadedByJamiiForums1458505226.116296.jpg
ImageUploadedByJamiiForums1458505390.864576.jpg

Nimejaribu kupiga picha hapo ilikua sa 2323hrs DSM. Nadhani ndo hiyo ipo karibu na mwezi na hio compass inaendana na nlipokua naipiga hio picha
 
View attachment 331337View attachment 331338

Nimejaribu kupiga picha hapo ilikua sa 2323hrs DSM. Nadhani ndo hiyo ipo karibu na mwezi na hio compass inaendana na nlipokua naipiga hio picha

Nimeiangalia tena picha yako pamoja na telemetry na nadhani ulioipiga picha ni "Procyon" na sio Sirius. Nimetuma chart mbili. Moja inaionesha Procyon karibu na mwezi na nyingine inainosha Sirius north-west ya Procyon.

Jaribu kuangalia tena kama utaona tofauti. Sirius inawaka zaidi kuliko Procyon.
Sirius (not Procyon).png

Procyon (Not Sirius).png
 
Nimeiangalia tena picha yako pamoja na telemetry na nadhani ulioipiga picha ni "Procyon" na sio Sirius. Nimetuma chart mbili. Moja inaionesha Procyon karibu na mwezi na nyingine inainosha Sirius north-west ya Procyon.

Jaribu kuangalia tena kama utaona tofauti. Sirius inawaka zaidi kuliko Procyon.

Mkuu upo macho?
 
Haya, BISMILLAH.

Nyota ni nini?
Nyota ni kama jua letu, lakini ziko mbali sana.

Nyota ziko mbali kiasi gani?
Mwanga unasafiri kwa kasi (speed) ya 299,793 km/sekunde au 1,079 milioni km/saa. Mara nyingi umbali wa nyota hupimwa kwa muda utakaotumiwa na mwanga kusafiri mpaka kutufikia sisi. Kwa mfano, mwanga kutoka jua letu unasafiri kwa takriban dakika 8 hivi kutufikia sisi (au, jua liko umbali wa 8 light-minutes kutoka hapa duniani). Nyota iliyo karibu sana na sisi ni ile iitwayo alpha-Centauri (kwenye constellation ya Centaurus) ambayo iko umbali wa 4.4 light-years kutoka hapa (mwanga kutoka alpha-centauri huchukua miaka 4.4 kutufikia) ndio maana nyota zinaonekana ndogo sana ukifananisha na nyota yetu (jua) hapa duniani. Jua letu ni moja ya nyota ndogo sana. Kuna mizinga ya nyota kama Betelgeuse (kwenye Constellation ya Orion) ambayo ina ukubwa wa majua yetu 1,000 na iko umbali wa 643 light-years kutoka hapa.

Chanzo cha mwanga wa nyota.
Nyota zote (pamoja na jua letu) zinatoa mwanga, joto, na nishati nyingine kutokana na nguvu za nyuklia aina ya fusion. Fusion inachukua atom mbili za hewa ya hydrogen na kuziunganisha ili kutengeneza atom moja ya hewa ya Helium. Uzito wa zile atom mbili za hydrogen ni mkubwa kuliko uzito wa atom ya helium iliyotengenezwa. Hii tofauti ya uzito "m" haipotei bali hubadilika kuwa nishati (E) kufuatia kanuni ya mkulu Albert Einstein kuwa E=mC2. Hii C ni ile kasi (speed) ya mwanga tuliyozungumzia hapo juu.

(Nguvu za nyuklia pia zinaweza kupatikana kwa kupasua (Fission) atom nzito kama za Urani (Uranium). Njia hii inatumika kwenye mitambo ya nyuklia inayozalisha umeme, mabomu, nk. Njia hii ya fission ni less efficient kuliko ile inayotokea kwenye jua kupitia fusion.)

Kwa kuwa nyota zote zina ujazo mkubwa sana wa hewa ya hydrogen, inachukua mabilioni ya miaka kuimaliza hii hydrogen. Kwa hiyo usiwe na wasiwasi, jua letu litaendelea kuwaka kwa mabilioni mengine ya miaka.

Rangi ya nyota nyingine kubadilika badilika (Nyekundu/bluu)
Nyota nyingi ziko moja moja, kama jua letu. Lakini kuna nyota nyingine zinakuwa pacha (mbili karibu karibu au Binary-stars). Zikiwa hivi basi zina-spin. Sisi hapa duniani tukiziangalia tunachoona ni matokeo ya hii spin (naomba mtu anisaidie maana ya spin).

Wakati moja ya hizi nyota ikiwa inakuja kwetu mwanga wake unaonekana kama una wave-length fupi (wave-length ya rangi ya bluu.) Ile nyota inayo tukimbia mwanga wake unaonekana kama una wave-length ndefu (wave-length ya rangi nyekundu). Hali hii inafanya tuone nyota ina-twinkle na rangi mbili, nyekundu na bluu. Hii inajulikana kama Doppler-effect iliyogunduliwa na mwanasayansi Christian Doppler mwaka 1842 alipowasilisha mada yake kwenye kongamano huko Prague kuhusu hizi binary-stars na rangi zake (alikuwa ni Astro-Physicist Kutoka Austria).

Nawasilisha.

I am sorry if this is an overkill.

Mkuu hapa umetoboa penyewe. Asante kwa elimu mujarabu. Ila hiyo kitu Doppler effect umenikumbusha Physics advance.
 
Mkuu here i am...vipi kwema

Mkuu jana nilikusubiri kwa masaa mawili sikukuona.

Kwa sasa ngoja nikupe maelekezo ya haraka haraka kwa kuwa nitatoka hivi karibuni.

Toka nje, angalia Magharibi (tumia dira yako). Halafu geukia kusini kwa nyuzi 10 (degrees). Halafu inua macho yako (from horizon) nyuzi 33 (degrees of altitude). Hapo ndipo ilipo Sirius kwa sasa (11:31 pm). Katika mitaa hiyo Sirius ni hiyo nyota inayowaka zaidi ya nyingine hapo.
 
Back
Top Bottom