Matikuu Kifyatu naomba unieleweshe ni nishati gani inayowezesha satelite kuwa kwenye motion.
Nishati ya kuiongoza:
Satellite ikishaingia kwenye orbit na kupata spidi stahiki basi haihitaji kusukumwa tena. Itaendelea tu kama ulivyo mwezi wetu (mwezi ni satellite ya dunia yetu). Isipokuwa satellite zote zinakuwa na mitungi ya hewa ya hydrogen na Oxygen ambazo zikichanganywa zinalipuka na kutoa msukumo (thrust) kama unataka kuirekebisha au kuipunguzia mwendo ili uidondoshe.
Nishati ya matumizi ya kila siku:
Satellite zote zinatumia nishati kubwa sana kuendeshea mitambo yake ya mawasiliano na dunia, kupiga picha, kompyuta na electronics zote. Kupata nishati hii Satellite nyingi hutumia solar panels kutengeneza umeme. Pia ndani ya hizi satellite kuna rechargeable batteries ambazo zinachajiwa na hizi solar panels ili kuhifadhi nishati kwa matumizi ya baadae.
Vyombo vinavyokwenda mbali sana ambako muanga wa jua ni hafifu sana wanatunia nishati ya nyuklia kutengeneza umeme wa matumizi ya kila siku.