Ufahamu kuhusu nyota za angani

11:59 pm. Elevation ya Sirius ni 16 degrees. Kama hujapata message zangu mpaka sasa basi ni mpaka kesho tena. Sirius inaelekea kuzama sasa.
 
Naomba pia mwenye uelewa na haya masuala ya nnyota (zodiacal light) namaanisha makundi kumi na mbili ya nyota mfano ndoo, mashuke,samaki mapacha ,simba ,nge, n.k
 
Naomba pia mwenye uelewa na haya masuala ya nnyota (zodiacal light) namaanisha makundi kumi na mbili ya nyota mfano ndoo, mashuke,samaki mapacha ,simba ,nge, n.k
Zodiac signs ni makundi ya nyota yaliopo kwenye njia ya jua (Ecliptic). Chukulia kuwa dunia imesimama na jua ndio linalotuzunguuka (ambavyo ndio tunavyojihisi hapa duniani), basi ukiliangalia jua angani litakuwa katika mkusanyiko wa nyota mmoja baada ya mwengine takriban kila mwezi. Hii mikusanyiko ya nyota ndio hiyo unayoitaja hapo juu.

Zamani wataalamu wa anga walifananisha makundi ya nyota angani na vitu fulani (mbwa, samaki, Orion, n.k.) ili waweze kuikumbuka kila inapojirudia. Kuna makudi ya nyota kama 99 hivi (ninayoyafahamu).

Unataka kujua nini kuhusu haya makundi ya Zodiac?
 
Ninachohitaji kujua ni jinsi gani makundi kumi na mbili ya nyota yanavyohusianishwa na maisha ya kila siku (Utabiri wa nyota).

Pia mpangilio wake katika tarehe hasa samaki na ndoo kumekuwa na mabadiliko kati ya tarehe 19 na 20 mwezi wa pili.
 
Ninachohitaji kujua ni jinsi gani makundi kumi na mbili ya nyota yanavyohusianishwa na maisha ya kila siku (Utabiri wa nyota).
Pia mpangilio wake katika tarehe hasa samaki na kumekuwa na mabadiliko kati ya tarehe 19 na 20 mwezi wa pili.

Taaluma ya utabiri wa nyota hujulikana kama ASTROLOGY. Dhana hapa ni kuwa mpangilio wa jua, nyota, sayari na mwezi angani wakati unazaliwa vinakupa muelekeo fulani katika maisha yako. Halafu, kadri hizi nyota, sayari, mwezi na jua zinavyobadilika angani huwa vinaathiri (vibaya au vyema) maisha yako ya kila siku.

Jua na mwezi vinadhaniwa ndivyo vinavyochangia kwa hali ya juu sana maisha yako. Ndio maana jua lilipo (Zodiac sign) wakati wa kuzaliwa kwako ni muhimu sana

Mimi sio mtaalamu wa Astrology (ni hobby yangu nyingine ya juu juu tu) kwa hiyo ngoja tusubiri wenye fani yao waje wakubwagie nondo.
 
Asante sana mkuu, labda tumsubirie M.M ezekiel au huyu mtoto wa sheikh yahya husein. Au mwingine yoyote yule mwenye ufahamu na somo hilo
 
Kifyatu Mkuu niambie zaidi kuhusu voyages zilipo fika na taarifa ambazo zimeleta. hapa dunian....je zinaleta taarifa kwa wakati au taarifa zinachelewa Ikifika kutokana na umbali???

2.ikitokea zikakamatwa na another being kwenye universe je tuna namna ya kufahamu!!,

Nin nature ya mission yao!!
Neo
 
hii light years maana yake nini?
hii ni umbali ambao mwanga unaweza kusafiri kutoka sehemu moja hadi nyingine kwa mwaka, watu waastronomy wanatumia light years kwa sababu umbali kwenye maswali ya anga mfano kutoka labda hapa duniani hadi kwenye galaxy zingine zinachukuwa number nyingi sana, mfano 1 light year=6 trillions miles, ukizangatia mwanga ndo kitu chenye spidi kubwa kuliko chochote hivyo wanaanga hutumia hiyo unit ya lightyear.
 
Mkuu hivi dunia inagravity yake? Jua lina gravity yake? Na mwezi pia unagravity yake? If yex kwanini gravity ya jua haiathiri kujaa na kukupwa kwa maji?
 
Nashukuru sana wakuu kwa kufatilia uzi huu mengi nimelimika, awali niliona maelezo kuwa nyoto hutoa rangi tofauti kama blue, green, red hicho nimefanikiwa kukiona pia nimejifunza kuhusu binary stars (nyoto pacha) zina spiin light na kutoa wave length zenye kutembea kwa speed, naomba kupata elimu huwaga siku za mawingu au mvua ndogo ndogo naona kitu ambacho tumezoe kukiita upinde (Rambow) ikiwa inajitokeza ktk blue sky(mawingu) naomba kufahamu inafanyikaje?

Na Je inahusiana na zile nyota kuspiin light
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…