Mkuu here i am...vipi kwema
Samahani. Elevation ya Sirius ni 21 degrees sasa hivi at 11:40pm
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu here i am...vipi kwema
Mkuu uko deep sana na hayo mambo ya Astronomy nadhani ndo fani yako,asante sana nimejifunza mengi sana!!! Namkumbuka Monstgala kama sijakosea kuhusu haya mambo!!!11:59 pm. Elevation ya Sirius ni 16 degrees. Kama hujapata message zangu mpaka sasa basi ni mpaka kesho tena. Sirius inaelekea kuzama sasa.
Asante mkuu. Astronomy ni moja ya hobby zangu tu.Mkuu uko deep sana na hayo mambo ya Astronomy nadhani ndo fani yako,asante sana nimejifunza mengi sana!!! Namkumbuka Monstgala kama sijakosea kuhusu haya mambo!!!
11:59 pm. Elevation ya Sirius ni 16 degrees. Kama hujapata message zangu mpaka sasa basi ni mpaka kesho tena. Sirius inaelekea kuzama sasa.
Safi sana mkuu. Wewe sio Monstgala? nakufananisha sana na huyo jamaa!!Asante mkuu. Astronomy ni moja ya hobby zangu tu.
Zodiac signs ni makundi ya nyota yaliopo kwenye njia ya jua (Ecliptic). Chukulia kuwa dunia imesimama na jua ndio linalotuzunguuka (ambavyo ndio tunavyojihisi hapa duniani), basi ukiliangalia jua angani litakuwa katika mkusanyiko wa nyota mmoja baada ya mwengine takriban kila mwezi. Hii mikusanyiko ya nyota ndio hiyo unayoitaja hapo juu.Naomba pia mwenye uelewa na haya masuala ya nnyota (zodiacal light) namaanisha makundi kumi na mbili ya nyota mfano ndoo, mashuke,samaki mapacha ,simba ,nge, n.k
Ninachohitaji kujua ni jinsi gani makundi kumi na mbili ya nyota yanavyohusianishwa na maisha ya kila siku (Utabiri wa nyota).Zodiac signs ni makundi ya nyota yaliopo kwenye njia ya jua (Ecliptic). Chukulia kuwa dunia imesimama na jua ndio linalotuzunguuka (ambavyo ndio tunavyojihisi hapa duniani), basi ukiliangalia jua angani litakuwa katika mkusanyiko wa nyota mmoja baada ya mwengine takriban kila mwezi. Hii mikusanyiko ya nyota ndio hiyo unayoitaja hapo juu.
Zamani wataalamu wa anga walifananisha makundi ya nyota angani na vitu fulani (mbwa, samaki, Orion, n.k.) ili waweze kuikumbuka kila inapojirudia. Kuna makudi ya nyota kama 99 hivi (ninayoyafahamu).
Unataka kujua nini kuhusu haya makundi ya Zodiac?
Ninachohitaji kujua ni jinsi gani makundi kumi na mbili ya nyota yanavyohusianishwa na maisha ya kila siku (Utabiri wa nyota).
Pia mpangilio wake katika tarehe hasa samaki na kumekuwa na mabadiliko kati ya tarehe 19 na 20 mwezi wa pili.
Asante sana mkuu, labda tumsubirie M.M ezekiel au huyu mtoto wa sheikh yahya husein. Au mwingine yoyote yule mwenye ufahamu na somo hiloTaaluma ya utabiri wa nyota hujulikana kama ASTROLOGY. Dhana hapa ni kuwa mpangilio wa jua, nyota, sayari na mwezi angani wakati unazaliwa vinakupa muelekeo fulani katika maisha yako. Halafu, kadri hizi nyota, sayari, mwezi na jua zinavyobadilika angani huwa vinaathiri (vibaya au vyema) maisha yako ya kila siku.
Jua na mwezi vinadhaniwa ndivyo vinavyochangia kwa hali ya juu sana maisha yako. Ndio maana jua lilipo (Zodiac sign) wakati wa kuzaliwa kwako ni muhimu sana
Mimi sio mtaalamu wa Astrology (ni hobby yangu nyingine ya juu juu tu) kwa hiyo ngoja tusubiri wenye fani yao waje wakubwagie nondo.
Nyota hazina umbo maalumu .
hii light years maana yake nini?sio kweli, jua ni kati ya nyota ndogo sana kuonekana kwamba ni kubwa ni kwamba iko karibu sana na sisi wakati nyota nyingine ziko millions of light years away.
hii ni umbali ambao mwanga unaweza kusafiri kutoka sehemu moja hadi nyingine kwa mwaka, watu waastronomy wanatumia light years kwa sababu umbali kwenye maswali ya anga mfano kutoka labda hapa duniani hadi kwenye galaxy zingine zinachukuwa number nyingi sana, mfano 1 light year=6 trillions miles, ukizangatia mwanga ndo kitu chenye spidi kubwa kuliko chochote hivyo wanaanga hutumia hiyo unit ya lightyear.hii light years maana yake nini?
Mkuu hivi dunia inagravity yake? Jua lina gravity yake? Na mwezi pia unagravity yake? If yex kwanini gravity ya jua haiathiri kujaa na kukupwa kwa maji?1. sasa mkuu hii dhana ya dunia kuwa duara inakuwaje?
Dunia ni duara. Sayari inapoanza kuumbika inaweza kuwa ndogo na sio duara. Lakini kadri vitu vingine (meteorites, commets, sayari nyingine) vinapojiunga (zinavutwa na gravity ya hii sayari inayoumbika) huu mgongano hufanya miamba inawaka na kuyeyuka kama uji. Katika hali hii gravity na mzunguuko wa hii sayari huifanya iwe duara. Baada ya miaka mingi kupita sehemu ya nje ya hii sayari hupoa na kuwa kama ardhi yetu lakini ndani bado miamba inakuwa kama uji. Mara kwa mara huu uji hujitokeza nje kama volkano. Mlima kilimanjaro ndivyo ulivyotengenezwa.
Maji kupwa na kujaa kama dunia ingekuwa duara si maji yangekuwa yanapotea? hii ndio imekaaje?
Kumbuka dunia ina mdogo wake aitwae mwezi. Huu mwezi una gravity yake. Maji baharini huvutwa na hii gravity ya mwezi. Upande mwezi ulipo ndiko maji yanapoelekea na maji kujaa wakati ule upande mwengine (ambako mwezi haupo) maji hupwa.
2. ni kweli kuna jua lingine?
Jua letu ni hili hili moja. Lakini kila nyota angani ni jua lengine bali majua hayo yako mbali sana.
3. pamoja na idadi ya mito inayomwaga maji baharini kwa nini bahari haijai?
Bahari haijai kwa sababu jua linafyonza (evaporation) maji na kuwa mawingu. Upepo unapeperusha haya mawingu kuelekea sehemu zenye misitu na milima. Huko yale maji katika mawingu yanageuka kuwa mvua. Mvua inajaza mito na kupeleka maji baharini na huu mzunguuko unajirudia. Hii ndio maana watu wanaambiwa wapande miti ili kuleta mvua.
Nashukuru sana wakuu kwa kufatilia uzi huu mengi nimelimika, awali niliona maelezo kuwa nyoto hutoa rangi tofauti kama blue, green, red hicho nimefanikiwa kukiona pia nimejifunza kuhusu binary stars (nyoto pacha) zina spiin light na kutoa wave length zenye kutembea kwa speed, naomba kupata elimu huwaga siku za mawingu au mvua ndogo ndogo naona kitu ambacho tumezoe kukiita upinde (Rambow) ikiwa inajitokeza ktk blue sky(mawingu) naomba kufahamu inafanyikaje?
Kifyatu; tafadhali naomba unieleweshe khs hizi satellite zetu zinazorushwa angani je zipo umbali gani?
Kuna zilizoko umbali wa 36,000 km (geosynchronous satellite za TV, Radio, na huduma za simu) na,
kuna zilizoko karibu sana kama 400 km (International Space Station) au chini ya hapo (spy satelites).
Zinavuka hili tabaka la ozon layer?
Ozone layer yetu iko umbali wa kati ya 10km mpaka 17km (asilimia 90) na inaendelea mpaka 50km. Satelite zote ziko juu ya hii layer. Orbit ya chini kabisa ya satellites ni kama 160 km hivi.
Swali lako la mwisho:
Ili satelite ikae kwenye orbit (umbali) fulani lazima itembee katika kasi itakayoipa uwiano kati ya gravity (uzito wake) na centripetal force. Orbit za chini zinahitaji spidi kubwa na zile zilizo mbali zinatembea kwa kasi ndogo. Ili kuirudisha satelite duniani cha kufanya ni kupunguza tu spidi yake na itadondoka tu.