Kila kitu chenye mass (hata wewe na mimi) kina gravity yake. Kwa hiyo jua, mwezi, nyota, sayari vyote vina gravity zao.Mkuu hivi dunia inagravity yake? Jua lina gravity yake? Na mwezi pia unagravity yake? If yex kwanini gravity ya jua haiathiri kujaa na kukupwa kwa maji?
Nashukuru sana wakuu kwa kufatilia uzi huu mengi nimelimika, awali niliona maelezo kuwa nyoto hutoa rangi tofauti kama blue, green, red hicho nimefanikiwa kukiona pia nimejifunza kuhusu binary stars (nyoto pacha) zina spiin light na kutoa wave length zenye kutembea kwa speed, naomba kupata elimu huwaga siku za mawingu au mvua ndogo ndogo naona kitu ambacho tumezoe kukiita upinde (Rambow) ikiwa inajitokeza ktk blue sky(mawingu) naomba kufahamu inafanyikaje? Na Je inahusiana na zile nyota kuspiin light
Kupitia mchoro huu hivi kwanini hatutafautiani siku na tarehe, ikiwa sayari inajingusha yenyewe kulinguka jua na ndio matokeo ya usiku na mchana, kama vile tunavyotafautiana masaa? Je hii internationa date line zigzag yake ipoje?View attachment 318903Tazama hii sketch apa hizo ni sayari ambazo kila moja ina mzunguko wake binafsi na kila moja inazunguka jua kwa muda wake tofauti, Mchana na usiku ni matokeo ya dunia kuzunguka katika muhimili wake na mwaka ni dunia kuzunguka jua
Majibu:
- Uzito mdogo kwenye Mars sio tatizo bali viumbe vitakavyoishi huko vitakuwa na mifupa na musuli hafifu (density).
- Uzito sio tatizo bali hakuna hewa ya Oxygen wala maji yanayotiririka kama hapa.
- Mwaka wa dunia ni siku zetu 365, mwaka wa Mars ni siku zetu 687. Siku ya dunia yetu ni masaa 24, siku ya Mars ni masaa 24 na dakika 40.
- Mars haina pete kama ilivyo Saturn isipokuwa ina miezi miwili Phobos na Deimos. Inatabiriwa kuwa siku za usoni hii miezi inaweza kupigwa dhoruba na vimondo na kuwa vumbi ambalo linaweza kutengeneza pete kama ilivyo Saturn. Kitu hicho kinaweza kutokea hapa kwetu pia kama mwezi wetu utapigwa na dhorubwa kubwa hivyo.
Mkuu Kifyatu umenisahauKifyatu Mkuu niambie zaidi kuhusu voyages zilipo fika na taarifa ambazo zimeleta. hapa dunian....je zinaleta taarifa kwa wakati au taarifa zinachelewa Ikifika kutokana na umbali???
2.ikitokea zikakamatwa na another being kwenye universe je tuna namna ya kufahamu!!,
Nin nature ya mission yao!!
Neo
Mkuu samahani. Naona nilipitiwa. Nilidhani nimekujibu.Mkuu Kifyatu umenisahau.
Kifyatu Mkuu niambie zaidi kuhusu voyages zilipo fika na taarifa ambazo zimeleta. hapa dunian....je zinaleta taarifa kwa wakati au taarifa zinachelewa Ikifika kutokana na umbali???
2.ikitokea zikakamatwa na another being kwenye universe je tuna namna ya kufahamu!!,
Nin nature ya mission yao!!
Neo
Albert Einstein alifanya mahesabu yake na kugundua kuwa nguvu ya gravity ni sawa na mkunjo (curvature) katika mkeka wa space-time (space-time fabric). Pia hesabu zake zilitabiri kuwa kukitokea msituko kwenye mkeka huu basi mawimbi yake yatasambaa kwenye mkeka kama ambavyo mawimbi ya maji yanavyosambaa kutoka pale unapotupia jiwe au kitu kizito.Sante mkuu Kifyatu ,
Niambie kuhusu hii vibtation of black hole ambazo zimekuwa detected!, izo vibration ni nini na tunategemea nini kujifunza au kutengeneza kutokana huo ugunduzi!
Ahsante Kifyatu nini mategemeo kwenye huu ugunduzi???.Albert Einstein alifanya mahesabu yake na kugundua kuwa nguvu ya gravity ni sawa na mkunjo (curvature) katika mkeka wa space-time (space-time fabric). Pia hesabu zake zilitabiri kuwa kukitokea msituko kwenye mkeka huu basi mawimbi yake yatasambaa kwenye mkeka kama ambavyo mawimbi ya maji yanavyosambaa kutoka pale unapotupia jiwe au kitu kizito.
Blackhole ni sawa na mkunjo mkubwa sana katika huu mkeka. Sasa black-holes mbili zikigongana basi zinaufanya huu mkeka utetemeke sawasawa na bahari itakavyo tengeneza mawimbi (kama sunami) endapo mwamba mkuwa utatumbukizwa majini. Haya mawimbi yatasambaa kwenye mkeka wote. Ni haya mawimbi ndiyo yaliyokuwa detected kama vibrations.
Hizi vibrations zenyewe sidhani kama zitatusaidia sana kwa sasa.Ahsante Kifyatu nini mategemeo kwenye huu ugunduzi???.
Maana habari za mtaan zinasema we can know universe zaidi coz we can traval through izo vibrations ambazo zina speed kubwa kuliko mwanga!!!...
Tell me more kikombe changu nimemwaga maji nipe nijifunze zaid
Nitajaribu.Sante mkuu Kifyatu
Niambie kuhusu space time.
Wanasema time haiend mbele its constant.
Past, present and future zipo kwenye same line.
Nifunze zaid kuhusu space time na maelezo yake
Ngoja nikupe mfano mmoja. Nyota ya karibu na sisi (Alpha Centauri) iko 4.4 light years kutoka hapa. Ina maana tunapoiangalia tunaona vitu vilivyotokea zamani (miaka 4.4 iliopita).Kifyatu Napata idea ila bado saana!!. Kwa maana iyo unaweza kwenda future au past bila ku afect present? Maana inaonekana vyote vipo kwenye pallale line..haviwez kukutana iLa vinaongozana??
Ilivyo ni kuwa kadri unavyokaribia kasi ya mwanga ndio ukuaji wako unavyozorota kutokana na contraction of space. Sasa kama ulimuacha pacha wako hapa duniani na kusafiri kwenye space kwa kasi ya mwanga, ukirudi hapa pacha wako atakuwa amezeeka kuliko wewe. Ukisafiri katika kasi ya mwanga basi kwako wewe muda (time) unasimama.Mkuu Kifyatu mfano tukipata kitu chenye speed kubwa kuliko mwanga wa jua how is it possible mfn km mwanga wa jua unafika kwa dunia baada ya dakika 8, ikiwa inaweza kufika ndani ya dakika 2 ivyo sawa na kuwa na chombo cha speed ya 2min from sun to earth what will it change??
Tuanze hapa: Muda (time) ni relative na speed yako. Kadri speed inavyoongezeka ndio muda (Time) wako unavyozorota (slow-down). Dhana ni kuwa ukisafiri katika speed ya mwanga basi muda (au umri) wako unasimama ukilinganisha na uliowaacha duniani. Kwa hiyo ukirudi duniani wewe utakuwa kama ulivyoondoka (ki-umri) lakini dunia na watu wake watakuwa wamezeeka. Kwa hiyo wewe utakuwa unaona mambo ya siku za mbele ukilinganisha na umri wako (travel to the future). Hii ya kuwa ukisafiri kwa kasi umri wako unazorota imekwisha thibitishwa kisayansi kwa kuwatumia astronauts.Ahsante mkuu Kifyatu
Nlitaka kujua hii paradox ya ukiwa kwenye kax zaid ya mwanga unawexa kwenda kwenye future au kurud past..hii mechanism imekaaje maana inanichanga saana.