Mkuu
Kifyatu umenisahau.
Kifyatu Mkuu niambie zaidi kuhusu voyages zilipo fika na taarifa ambazo zimeleta. hapa dunian....je zinaleta taarifa kwa wakati au taarifa zinachelewa Ikifika kutokana na umbali???
2.ikitokea zikakamatwa na another being kwenye universe je tuna namna ya kufahamu!!,
Nin nature ya mission yao!!
Neo
Mkuu samahani. Naona nilipitiwa. Nilidhani nimekujibu.
Voyager1 na Voyager2 zilirushwa mwaka 1977 (September 5, na August 20) zikiwa na majukumu mawili kila chombo.
Voyager 1
Jukumu la kwanza:
Kutembelea na kuzichunguza sayari za Jupiter, Saturn (na mwezi wa Saturn uitwao Titan).
Jukumu la pili:
Kuendelea na safari mpaka kutoka nje ya solar system yetu (Heliosphere) na kutuma taarifa za anga la huko.
Iko wapi kwa sasa (May 2016):
Iko kwenye Interstellar space zaidi ya km 21,000,000,000 kutoka hapa. (Ni sawa na umbali wa duniani mpaka kwenye jua mara 136).
Bado inawasiliana nasi?
Ndio. Huchukua takriban masaa 20 hivi kwa ujumbe kutoka Voyager1 kutufikia kupitia mtandao wa
Deep-Space-Network.
Lini mwisho wa hii mission?
Nishati ya hiki chombo inapatikana kwa jenerata la nuclear. Inakadiriwa ifikapo mwaka 2025 hili jenerata litaishiwa nguvu na hapo ndio itakuwa mwisho wa mission hii.
Je kikikamatwa na aliens?
Kama watakikamata kabla ya 2025 basi kitatufahamisha. Wakikikamata baada ya 2025 basi tena ndio tutakuwa tumeula.
*******************************************************
Voyager 2
Jukumu la kwanza:
Kutembelea na kuzichunguza sayari za Jupiter, Saturn (na mwezi wa Saturn uitwao Titan), Uranus na Neptune.
Jukumu la pili:
Kama la Voyager1
Iko wapi kwa sasa (April 2016):
Iko kwenye ukingo wa heliosphere zaidi ya km 17,000,000,000 kutoka hapa. (Ni sawa na umbali wa duniani mpaka kwenye jua mara 110).
Bado inawasiliana nasi?
Ndio. Huchukua takriban masaa 17 hivi kwa ujumbe kutoka Voyager2 kutufikia kupitia mtandao wa
Deep-Space-Network.