Nia ya mada hii ni kuuweka muda na matukio kwa ufupi sana kama wataalamu wanavyouona ili tujifunze na kutafakari kwa akili zetu tunapochanganya na ufahamu kutoka vyanzo tofauti. Binafsi huu si msimamo wangu bali uchunguzi katika vyanzo ambavyo vipo siku zote kwenye vitabu, machapisho, digital information sources, habari za kuambiwa au kusikia, kujifunza na kadhalika. Kama tulitokea kwa bahati basi tuione bahati hii kwa upana wake na kama tulikusudiwa tutokeaa basi tuone kusudio hilo lilivyo na nguvu za kipekee kwa kuangalia matukio yanayoelezewa na wataalam wa fani husika.

Pia katika kuupitia muda na matukio tunayoambiwa yalitokea na yatatokea, tunaweza kuona jinsi tulivyo muhimu au tusivyo muhimu katika muda huu mrefu wenye mambo makubwa yaliyotokea na yatakayotokea na hivyo kuufanya wakati huu kuwa wa kipekee sana.

Muda ni nini?

Ni swali zito na la zamani sana kabla sisi wote hatujazaliwa tayari wataalam wa fani mbali mbali wamejaribu kulijibu kwa upeo wa juu sana. Bado swali hili lipo tu kwa kuwa bado tunaendelea kujifunza jinsi ulimwegu ulivyo na unavyofanya kazi. Na hasa ukitaka kufafanua muda ni nini ugumu unakuja lakini kila mtu hata mtoto mdogo anauona muda kwa namna yake mwenyewe. Hivyo kila mtu kwa nafasi yake anaweza kuu-define muda kwa maana kila mtu anau-experience na analo jambo fulani linalomfanya auone muda kwa namna yake. Sitajikita katika kutafuta maana ya muda inayokubaliwa na wengi kwa kuwa kuna majibu mengi sana kutoka kwenye dhana tofauti na hiyo si mada hii ila nitajikita katika kuangalia matukio na tofauti ya muda wake kwa kuwa ndio yanatupa ule mstari wa kufikirika wa muda wenye past, present and future.

Kumbuka muda tumeamua wenyewe (binadamu) kuuweka katika vipimo (sekunde, dakika, mwaka etc) hivyo kuujengea kitu kama mstari ulionyooka katika fikra zetu. Kwamba mstari huu una uelekeo mmoja na sasa tuko katikati yake (tulipo) na yale yaliyopita yanajipanga upande mmoja wa tulikotoka na yajayo ambayo hatujayafikia yanajipanga katika upande mwingine wa mstari wa tunakoelekea.

Matukio yanayo/yatakayo na yaliyotokea yanatupa uelewa wa muda uliopita, wa sasa na ujao. Kitu cha kukumbuka na cha ajabu ni kwamba mstari huu wa muda (arrow of time) wala haupo katika zile sheria za msingi za physics na wala hauna muunganiko wowote na sheria hizi. Hivyo mstari huu wa muda ni katika ufahamu wetu na uwezo wa kuuona au kuufikiri kwa kuangalia matukio hivyo ni wa kufikirika au psychological arrow. Tusiuchanganye na thermodynamic arrow na cosmological arrow hizi zinasimama kama dhana tofauti na sio mada yetu kwa sasa.

Muda kwa kuangalia tangu kutokea kwa ulimwengu (universe)

NOTE. Kumbuka hapa baadhi ya maeneo theories, hypothesis na phenomena zenye ushawishi zinatumika. Wataalam wa theoretical phyisics, na Astrophicists wanashika hatamu hapa.

Umri wa sayari ya Dunia na Jua

Wataalam hawa wanatuambia umri wa jua na dunia umekaribiana wakiwa na maana kuna tofauti ya miaka milioni 60. Lakini muda huu si kidogo kwetu sisi binadamu ambao dakika zinatumika hata kwenye misemo ya kila siku. Kama unakumbuka ule wa "Nipe dakika mbili tu ntakua hapo"

Jua lilitokea katika wingu kubwa la gesi mbali mbali miaka bilioni 4.6 iliyopita (4.6 Ga). Baada ya hapo dunia ikatokea/tengenezwa kutoka kwenye mabaki ya milipuko ile ya gesi iliyokuwa iliyotengeneza jua. Baada ya hapa kikafuata kipindi kigumu sana ambacho dunia imewahi kupitia (Hadean Eon). Joto kali na lava katika uso wote wa dunia pamoja na milipuko mingi sana na kugongwa na mamilioni ya vimwondo, miale na mawe makubwa. Na hypothesis moja inasema katika kipindi hiki cha Hadean Eon ndipo mwezi ulipotokea baada ya dunia kugongwa na kitu kizito sana ambacho kinadhaniwa kuwa sayari ndogo au dwarf planet. Mkusanyiko wa mapande ya mawe, vumbi na madini yaliyosababishwa na mgongano huu wa dunia na aina fulani ya sayari ndogo ndio ulioutengeneza mwezi. Kumbuka ni process za muda mrefu sana hizi mamilioni ya miaka. Kipindi hiki cha Hadean Eon kinakadiriwa kuchukua takribani miaka bilioni moja(1 Billion) mpaka pale hali ya hewa ilipoanza kutulia taratibu na dunia kupoa.

Umri wa Ulimwengu (Universe)

Umri wa ulimwengu au universe unakadiriwa kutokana na ile theory ya Big Bang kuwa ni miaka bilioni 13.8 toka mlipuko huo mpaka sasa. Hivyo toka jua li-form kutoka kwenye mawingu fulani ya gesi na baadae dunia mpaka sasa.

Mwisho wa Jua

Na kama ulidhani muda unavyoenda mbele ndio mambo yanakuwa mazuri basi kaa vizuri uone muda ukiangaliwa huko mbeleni predictions za future zikoje. Baada ya miaka bilioni nane jua litapanuka mara 250 ya sasa na hivyo kumeza dunia na sayari zote. Lakini kabla ya hapo ndani ya miaka milioni mia nane (800yrs) kiwango cha carbondioxide kitashuka chini kabisa na kuisha na hii ina maana hakutakuwa na photosythesis na hivyo kukosekana kwa oygen ambayo ndio chanzo muhimu cha uhai. Baada ya miaka bilioni moja miale ya jua itakuwa mikali sana na kufanya maji yote katika dunia ya-evaporate na kupotelea anga za mbali.

Kabla ya universe

Wataalam wanatuambia hata muda ulizaliwa hapo hivyo kabla ya Big bang hakukuwa na muda. Mvurugano na mraruano uliopo ni kwamba hakuna theory yoyote nzuri inayoendana na uwezo wa akili ya mwanadamu kwa hili. Lakini si kwamba hazipo theory zinazojaribu kueleza nini hii kitu inayoitwa "kabla ya Big Bang".

Albert Eisten katika "theory of relativity" yeye anafafanua wazi jinsi muda ulivyozaliwa na kabla ya hapo muda ulikuwa umesimama au kwa lugha nyingine hauendi mbele wala nyuma. Na katika kipindi hiki ulimwengu mzima (universe) ulikuwa kitu kimoja kidogo sana zaidi ya sub-atomic particle yani huwezi kukiona hata kwa microscope.

Inflation theory inasuggest kuwepo kwa universe nyingine iliosababisha hii tuliyomo wakati ile ya multiverse au chaotic inflationary ikipendekeza kuwepo kwa universes nyingi kama bubbles zisizohesabika na hii ya kwetu ni mojawapo. Kuna ile ya "Extra dimensional membranes" (branes), White holes, Our universe being inside a big black hole na models nyinginezo katika kujaribu kutafuta jibu lenye ushawishi.

Wakati ujao wa ulimwengu (universe)

Baada ya jua kulipuka na kutoweka ama kuwa kitu kingine tofauti muda unaoendelea mbele ni wa kutisha na kusikitisha sana. Hapa sasa tunauangalia muda kwa kipindi kirefu sana kiasi kwamba namba zinazotumika kwa makadirio ili tuuone mwisho wa universe ni trillions za miaka (T).

Baada ya muda wa kati ya miaka trilioni moja na trillioni mia (1-100T) nyota zitaacha kuumbika au ku-form katika pande zote za ulimwengu mzima. Kumbuka nyota zinakufa na kuzaliwa kila siku kwa sasa. Baada ya kati ya miaka trilioni 110 na 120 (110-120T), nyota ya mwisho kabisa kuwepo inaishiwa nishati yake na kuzima/kufa. Baada ya miaka 10^10 [SUP]76 [/SUP], matter katika ulimwengu au universe sasa imeliwa yote na black holes na ndiyo yamebakia yakiranda-randa na kumezana/kuungana.

Baada ya miaka 10^10[SUP]120[/SUP] nishati yote katika ulimwengu(universe) imeisha hivyo hamna chochote kinachofanyika tena popote pale na inaitwa "Heat Death" wala haieleweki vizuri au mimi siielewi vizuri lakini ni model mojawapo yenye ushawishi kwa sasa.

Hitimisho:

Kutokana na information hizi za hawa wataalam, binadamu wa kawaida mwenye lugha na utamaduni (modern human) amekuwepo miaka 62,014 tu katika ulimwengu wenye miaka bilioni 13.8. Hii ni asilimia 0.000449% tu ya muda wote tangu kuanza kwa universe.

Na wataalam hawa wanamaanisha kwa lugha nyepesi - katika muda huu mrefu na matukio yake chini ya sheria za kifizikia zilizojiweka zenyewe au zilizowekwa umefanya baadhi ya zile gas zijiangalie, zijitambue na kuanza kuulizana na kubishana zilitoka wapi na muda uendavyo mbele(kama unaenda mbele) imagine gas hizi zitafanya nin??.
Mada yake inajitegemea toka kwa @monstagala
Tafadhali kifyatu mchango wako