Ufahamu kuhusu nyota za angani

Ufahamu kuhusu nyota za angani

Asaante mkuu kwa kunitoa hofu

swal lingine iv radi nkimaanisha ule mwanga ambao unaweza kuunguza miti mikubwa na had kuua mtu pamoja na zile nguromo uwa zinatokana na nn uko juu?
Radi ni chaji ya umeme inayojijenga kwenye mawingu na ikiwa kubwa inateremka (discharge) aridhini. Sasa ikipitia mti, mtu au chochote kile inakipasua.

Sijui kama ulikwishawahi kuteremka kwenye gari na ukapata ka-electric shock kadogo? Gari linapotembea, upepo unasuguana na hilo gari na kulichaji (static charge). Sasa ukiteremka na kuweka mguu aridhini hiyo chaji inapitia mwili wako kwenda aridhini. Mfumo huohuo ndio unaotokea kwenye mawingu na kupata radi.

Radi ni muhumu sana katika maisha yetu. Homework yako ya leo ni kwenda kwenye mtandao wa internet ufanye utafiti wa faida za radi hapa duniani halafu utuletee hiyo mada hapa na sisi tunufaike.
 
sawa mkuu had kufika saa 4 usiku ntaleta mrejesho hapa juu ya faida za radi
 
Mkuu Kifyatu Siku hizi kwenye type of matter zimekuwa 4,liquid,solid gas na plasma!,
Sasa iyo plasma ni kitu gan???
 
Mkuu Kifyatu Siku hizi kwenye type of matter zimekuwa 4,liquid,solid gas na plasma!,
Sasa iyo plasma ni kitu gan???
Plasma ni gas tu yenye properties fulani. Katika Gas ya kawaida atoms zake zinakuwa stable (balanced in electrons na protons) na ni vigumu sana kupitisha umeme. Sasa kama gas ikipashwa moto mkali (au ikiwa subjected to strong electric fields) hii gas inaweza kupoteza electrons au electrons zake zinakuwa so excited kwamba zinaweza kuruka freely kutoka atom moja hadi nyingine. State hii ya gas inaitwa ionized gas. Sasa gas ambayo ni super-ionized ndio plasma. Umeme unaweza kuwa conducted vizuri na hii plasma.

Kwa hiyo matter inaweza kuwa solid, liquid, gas (neutral) au plasma (super-ionized gas)
 
Kifyatu za join!!!,tuendeleze mjadala wetu!,sasa mfano was hzo plasma ni nini!!?,inatusaidiaje??..na unaweza kupima vp kiwango chake
Je radi ina plasma ???
 
Mkuu Kifyatu kwanza nikushukuru kwa namna ambavyo umeutendea haki huu uzi.Nakiri kwamba mimi ni mmoja kati ya waliolemika vya kutosha kupitia michango yako tangu uzi huu ulipoanza.

Ila kuna suala ambalo sijakuelewa vizuri hivyo kama utapata muda naomba unisaidie kunielewesha.

Kuna bandiko humu uliliweka pamoja na picha ukiwa unajaribu kumuonyesha mmoja kati ya wachangiaji wa mada juu ya ilipo galaxy yetu ya milkway. Sasa suala langu ni vipi hiyo ndio iwe galaxy yetu ikiwa sisi wenyewe (ambao tupo kwenye hiyo galaxy) twaiona kwa umbali huo?.Kwa maana ya kwamba tunakuwaje ndani ya chombo ambacho twakiona kwa umbali kiasi hicho?

Natumaini utakuwa umenielewa nachojaribu kumaanisha hapa.
Ahsante na nasubiria jawabu lako In Sha Allah.
 
Kifyatu za join!!!,tuendeleze mjadala wetu!,sasa mfano was hzo plasma ni nini!!?,inatusaidiaje??..na unaweza kupima vp kiwango chake
Je radi ina plasma ???
Radi:
Gas inapokuwa ionized inakuwa plasma. Kwa hiyo radi inapopiga basi hewa angani inakuwa ionized na inakuwa plasma (pale radi inapopita tu). Ni hii plasma inayotengenezwa na radi ndiyo yenye manufaa makubwa kwetu sisi (binadamu, mimea, wanyama) hapa duniani. Pasinge kuwepo na radi basi sisi viumbe tusingekuwepo kabisa. Tumsubiri mkuu baraka bb aje na maelezo yake. Nilimpa homework hii jana bado tunasubiri mrejesho wake.

Faida nyingine za plasma:
Zaidi ya kutupa uhai wetu kupitia radi, plasma pia inatumika kwenye
  • TV (plasma TV - kuna ionized gas cells ndio zinazotoa mwanga wa rangi nzuri),
  • Neon signs/displays (nadhani umeona mabango ya matangazo usiku yenye rangi nzuri sana),
  • Auroras (borealis na australis) ambao ni muanga unaotokea usiku north au south poles.
  • Mara nyingi mahali popote pale penye moto mkali basi plasma nayo ipo.
Natumaini hii imesaidia.
 
Mkuu Kifyatu kwanza nikushukuru kwa namna ambavyo umeutendea haki huu uzi.Nakiri kwamba mimi ni mmoja kati ya waliolemika vya kutosha kupitia michango yako tangu uzi huu ulipoanza.
Ila kuna suala ambalo sijakuelewa vizuri hivyo kama utapata muda naomba unisaidie kunielewesha.
Kuna bandiko humu uliliweka pamoja na picha ukiwa unajaribu kumuonyesha mmoja kati ya wachangiaji wa mada juu ya ilipo galaxy yetu ya milkway.
Sasa suala langu ni vipi hiyo ndio iwe galaxy yetu ikiwa sisi wenyewe (ambao tupo kwenye hiyo galaxy) twaiona kwa umbali huo?.Kwa maana ya kwamba tunakuwaje ndani ya chombo ambacho twakiona kwa umbali kiasi hicho?.
Natumaini utakuwa umenielewa nachojaribu kumaanisha hapa.
Ahsante na nasubiria jawabu lako In Sha Allah.
Asante mkuu kwa kushukuru.

Galaxy yetu (milkway nilioiweka hapo chini) ni spiral galaxy (ina mikia). Katikati ya hii galaxy ndipo lilipo hilo blackhole letu. Sisi (jua na solar system yetu) tuko kwenye moja ya mikia ya hii galaxy mbali kabisa na center. Kwa hiyo kama jua halituzibii tunaweza kuiona karibuni galaxy yetu yote usiku.
images
 
Mkuu Kifyatu nini kinasababisha Maisha kuwepo Dunian je ni miti ambayo inafanya photosynthesis inatoa oxygen na kuchukua borbondioxide au ni maji yanayofanya evaporation.....
Je mfn Mars kipi cha kuweka....dams au kupanda miti ili kusuport life???
 
Ahsante sana mkuu,hapo nimekuelewa.
 
Mkuu Kifyatu nini kinasababisha Maisha kuwepo Dunian je ni miti ambayo inafanya photosynthesis inatoa oxygen na kuchukua borbondioxide au ni maji yanayofanya evaporation.....
Je mfn Mars kipi cha kuweka....dams au kupanda miti ili kusuport life???
Mars hewa yake karibuni yote ni carbon dioxide (95%) na 3% Nitrogen. Ili maisha yawepo Mars tunahitaji kuzalisha Oxygen na mimea ndio kazi yake hiyo. Kwa hiyo unaweza kusema tupande miti kwa wingi inayotumia carbon dioxide na kuzalisha oxygen. Wasiwasi wangu ni kuwa huu uhaba wa Nitrogen unaweza kutukwaza.

Nitalielezea hili kwa kirefu, pamoja na swali lako la kwanza (Maisha kuwepo duniani) baada ya mrejesho wa mkuu baraka bb . Sitaki kumjibia assignment yake.

Tukumbushane lakini mkuu.
 
Swali jingine Kifyatu wakati tunamsubiri baraka bb ,je iwapo dunia ikagongwa na kitu kizito bila kuangalia athari na tukahama kwenye muhimili wa wake na solar system yetu hi!!..je Maisha yanaweza kuendelea kuwepo???
 
Mkuu swali zuri sana hili.

Yaani sisi hapa duniani tushukuru bahati tuliokuwa nayo kuwepo hapa. Ni sehemu ambayo is just right au perfect. Tukihama tu hii orbit yetu, basi bila kuangalia tutagongana na nani au nini ni kwamba hali ya hewa itabadilika vibaya sana (joto kali au baridi kali) kiasi kwamba pengine uhai duniani ukatoweka kabisa. Mpaka sasa kwenye solar-system yetu hatujathibitisha kuwa kuna uhai mahali popote pengine isipokuwa hapa (pengine sio kweli). Hii ni kwa sababu ya nafasi maridhawa tuliokuwa nayo sisi hapa duniani.

Lakini pengine cha maana zaidi ni kuwa hicho kitu kitakachotugonga mpaka tukasesereka sidhani kama kitaacha uhai hapa duniani.
 
Mkuu Kifyatu katika soma yangu nimeona kuhusu mwezi na ambavyo inasuport maji kupwa na kujaa...tena ikasema ina athari kwenye akili za mwanadam!!,je ina athari gan??..ukiachana kupwa na kujaa mwezi una msaada gan mwingine kusuport Maisha kwenye dunia yetu hi??
 
Mwezi ni muhimu sana kwetu hapa duniani kwa sababu unaufanya mzunguuko wa dunia kwenye mhimili wake (23.4 degrees) usibadilike (uwe stable). Bila ya mwezi basi dunia ingeyumba sana (mwaka huu DSM inakuwa ikweta, mwaka ujao inakuwa north pole, n.k.). Mwezi unaipa dunia the gyroscopic stability na ni muhimu sana kwa majira yetu na ukulima wetu. Kwa mantiki hii, mwezi ni muhimu kwa maisha (ukulima) yetu.

Ndio, mwezi husababisha maji ya bahari kupwa na kujaa. Hii ni kwa sababu ya gravity yake. Hii gravity ya mwezi inadhihirika zaidi kwenye maji lakini pia huathiri kila kitu kingine hapa duniani. Sisi binadamu/wanyama asilimia 80 yetu ni maji. Kwa hiyo kama bahari zinaathiriwa kwa nini sisi tusiathirike? Utasikia mara nyingi kuwa wagonjwa wa akili wanacharuka katika vipindi fulani vya mwezi.

Wanajimu (Astrologers) wanaupa kipaumbele kikubwa sana mwezi (saa nyingine hata zaidi ya jua) katika kutabiri nyota ya mtu. Pamoja na kuwa Astrology ni moja ya hobby zangu kama ilivyo Astronomy (tunayoijadili hapa), nisingependa kujibu swali lolote hapa kuhusu unajimu.
 
Mkuu Kifyatu ahsante Kwa maarifa yako ku-share na sisi....japo umesema usingependa kujibu kuhusu unajimu...Ila Nina ombi can you compare and contrast on astrology and astronomy??..

Je at some point vinakutana kwenye mada zao??
Japo astrology ni ya zaman kuliko astronomy imeisaidia astronomy kugundua Singapore huko kwenye deep space??!
 
Wewe mtu unatupa vitu vizito sana... Vinavyonifanya nije na hoja, daaaa.
 
Mkuu Kifyatu ahsante Kwa maarifa yako ku-share na sisi....japo umesema usingependa kujibu kuhusu unajimu...Ila Nina ombi can you compare and contrast on astrology and astronomy??..

Je at some point vinakutana kwenye mada zao??
Japo astrology ni ya zaman kuliko astronomy imeisaidia astronomy kugundua Singapore huko kwenye deep space??!
Astronomy inaangalia vitu angani (heavenly bodies) na kujaribu kuelewa laws of physics zinazovielezea tabia zake.

Astrology inaangalia uhusiano wa hizi heavenly bodies zilipo na zinavyomuathiri binadamu anapozaliwa, atakavyokuwa maishani, na pengine hata mauti yake yatakujaje. Huu utabiri sio kwa watu tu bali hata kwa systems hapa duniani.

Astrology is fascinating hasa unapoisoma na kuifanyia utafiti. Kwa mfano, tukichukua watu wote waliozaliwa katika mazingira sawa ya nyota na sayari zilipo, je tunaweza kuona ni vitu (traits) gani vinazojirudia?

Astrological Inference: Kama tangu zama hizo tumeona watu wenye nyota fulani wana character fulani, je tunaweza kutabiri kama mtoto anaezaliwa leo chini ya nyota kama hiyo atakuwa na traits hizo hizo? Mimi hicho ndio kinachonikuna sana. Kutafiti (kuanzia zama hizo) uhusiano wa mpangilio wa nyota na characteristics za watu wa nyota hiyo. Kupiga ramli na kumtabiria mtu nyota yake siku za usoni havini-interest sana.
 
Back
Top Bottom