Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tuanze hapa: Muda (time) ni relative na speed yako. Kadri speed inavyoongezeka ndio muda (Time) wako unavyozorota (slow-down). Dhana ni kuwa ukisafiri katika speed ya mwanga basi muda (au umri) wako unasimama ukilinganisha na uliowaacha duniani. Kwa hiyo ukirudi duniani wewe utakuwa kama ulivyoondoka (ki-umri) lakini dunia na watu wake watakuwa wamezeeka. Kwa hiyo wewe utakuwa unaona mambo ya siku za mbele ukilinganisha na umri wako (travel to the future). Hii ya kuwa ukisafiri kwa kasi umri wako unazorota imekwisha thibitishwa kisayansi kwa kuwatumia astronauts.
Sasa mkwara unakuja hapa. Kinadharia, kama utaweza kusafiri kwa kasi zaidi ya speed ya mwanga, basi muda (time) wako sio tu kuwa unasimama bali utakuwa unarudi nyuma (travel back in time). Tatizo hapa ni kuwa ukiweza kufanya hivyo na kukutana na wazazi wako walipokuwa watoto na ukaweza kuwaua, je wewe umepatikanaje. Hii ndio paradox ya kusafiri into the past.
Kwa maoni yangu ni kuwa kusafiri into the past haitawezekana. Sababu ya kwanza ni kuweza kusafiri kwa kasi kubwa zaidi ya kasi ya mwanga. Sababu ya pili ni hicho kiini-macho cha kuweza kubadilisha historia (mfano, umuue Hitler alipokuwa kichanga).
Imethibitika kisayansi kuwa ukisafiri kwa kasi kubwa basi aging process yako inazoroto. Na ukisafiri kwa kasi ya mwanga basi ukuaji wako unasimama kabisa .Mkuu travelin in to the future ina athiri vip umri wako wakati utakuwa umesafiri umbali mrefu kwa muda mfupi na kurudi? Kwa mfano Sehemu uliyokuwa usafiri kwa miaka 30 unasafiri kwa dakika tano kwenda na kurudi ita athiri vipi umri wako?
Imethibitika kisayansi kuwa ukisafiri kwa kasi kubwa basi aging process yako inazoroto. Na ukisafiri kwa kasi ya mwanga basi ukuaji wako unasimama kabisa .
Kwa hiyo ukisafiri masafa marefu ambayo yangekuchukua miaka 30 kwa kutumia dakika 5, wewe ndie utakaeona umetumia dakika 5 lakini sisi uliotuacha hapa tutaona umekwenda kwa miaka 30. Ukirudi, umri wako utakuwa umeongezeka kwa dakika 5 wakati sisi hapa duniani umri wetu utakuwa umeongezeka kwa miaka 30. Hii ndio maana ya traveling into the future.
Mkuu, dhana ya kusafiri into the past ni ya kusadikika lakini kusafiri into the future inawezekana.Mmhh hii bado ngumu kumeza mkuu..japo nimekuelewa vizuri..bado nahisi ni kuaminika zaidi ya uhalisia
Mkuu, dhana ya kusafiri into the past ni ya kusadikika lakini kusafiri into the future inawezekana.
Fikiria hivi: Kama leo tukikugandisha (cryogenically) na kukuweka kwenye freezer kwa miaka 30. Tukikugandua (na ukiwa mzima) basi umri wako utakuwa uleule uliokuwa nao wakati ulipogandishwa (miaka 30 iliopita) wakati sisi tutakuwa tumezeeka kwa miaka 30. Sasa kasi ya mwanga ina effect kama ya cryogenics. Sio kwa kugandisha bali kwa kuzorotesha au kusimamisha muda.
Kugandishwa kwa cryogenics hutumika kila siku kuhifadhia mayai na megu za kiume za binadamu, au vimelea hai vinginevyo (bacteria, viruses). Kwa hiyo hii sio nadharia tena.
Nafikiri itawezekana. Lakini hata kama ukisafiri kwa kasi ya nusu ya speed ya mwanga umri wako utazorota, ikimaanisha utasafiri into the future japokuwa ni kidogo.Duuh...mkuu unadhan teknolojia inaweza kuja kutengeneza chombo kinachokaribia light speed?
nyota ni ndogo sana kuliko dunia, ni kama mwezi. zinategemea mwanga wa jua. na nyota ulizoona zinazobadilika kutoka rangi kutokea ya blue kwenda ya kijani ni kutokana na kuzibwa na miti na bahari .na ukiona nyekundu ujue hapo kuna radi na mvua inanyesha.
Mkuu sasa ndio umefikia ukingoni walipo wanasayansi. Maswali kama, Je:mkuu Kifyatu samahan naomba kufunzwa kuhusu hili
hivi kama mambo yoooooote kama nyota,sayari,galaxies etc vipo ndani ya universe,sasa je hiyo universe imo ndani ya nn? je nje ya universe kuna nini? nawaza mpaka nahisi kuwehuka
mkuu Kifyatu samahan naomba kufunzwa kuhusu hili
hivi kama mambo yoooooote kama nyota,sayari,galaxies etc vipo ndani ya universe,sasa je hiyo universe imo ndani ya nn? je nje ya universe kuna nini? nawaza mpaka nahisi kuwehuka
Universe yetu (pamoja na galaxies) inatanuka kwa kasi kubwa sana. Sasa sijui tunakwenda wapi.Mkuu Kifyatu nlisoma sehem kwamba galaxy zinaendelea kupanuka kwa speed kubwa kuliko speed ya risasi...je kuna phenomenon yoyote kwamba kuna possibility galaxy zikaja collide??...je ikitokea nini kitatokea maana kila galaxy ina black hole
Ngoja nikupe mfano mmoja. Nyota ya karibu na sisi (Alpha Centauri) iko 4.4 light years kutoka hapa. Ina maana tunapoiangalia tunaona vitu vilivyotokea zamani (miaka 4.4 iliopita).
Sasa kama tungeweza kwenda kwa kasi ya ajabu na kufika kwenye hii nyota na kurudi mara moja, ina maana tungeona vitu ambavyo vitakujaonekana hapa duniani miaka 4.4 ijayo. Ina maana tutaweza kwenda into the future. Kuna katatizo kadogo tu hapa. Kwa sasa speed limit ya universe ni speed of light. Tukiweza kupata njia ya kusafiri kwa kasi kubwa zaidi ya speed of light basi usafiri kwenda future utawezekana.
Ukisafiri kwa kasi yoyote ile muda wako unatembea taratibu kuliko sisi tuliokaa. Ukiweza kusafiri katika kasi ya mwanga basi muda wako unasimama.Mkuu! hapa umenikanganya kidogo hivi ukitaka kwenda future uipite speed of light au uwe sawa na speed of light?
Mkuu tukushukuru wewe kwa kuuleta huu uzi zaidi ya miaka miwili iliopita. Asante.mkuu Kifyatu umeutendea haki uzi huu na unaongea vitu deep sana,,i salute you