Ufahamu kuhusu nyota za angani


Ahsante sana kaka mkubwa kifyatu umeeleweka vizur kwa upande wangu

swali iv uko kwenye sayar nyingine kuna mvua maana hapa dunia asilimia kubwa ya upatikanaji wa mvua uletwa na misitu pamoja na bahar vip uko mars au sayar nyingine
 
Ahsante sana kaka mkubwa kifyatu umeeleweka vizur kwa upande wangu

swali iv uko kwenye sayar nyingine kuna mvua maana hapa dunia asilimia kubwa ya upatikanaji wa mvua uletwa na misitu pamoja na bahar vip uko mars au sayar nyingine
Kwa sasa Mars haina mvua. Lakini kama tukichimba maji na kumwagilia miti basi baada ya muda mrefu hali inaweza ikajipa na kukawepo na mvua a maji kama hapa duniani.

Mvua ni kitu cha kawaida katika sayari nyingi tu. Mifano:
  • Sayari ya Venus inayesha tindikali - Sulphuric Acid (kwenye anga zake za juu) na pia kuna radi.
  • Titan (mwezi wa sayari ya Saturn) inanyesha methane (gesi iliopoa na kuwa kama maji).
  • Kwenye sayari za Saturn na Jupiter inanyesha ALMASI. Yes, DIAMONDS ndiyo mvua za huko bosi. Tuhamie huko nini mkuu?
Kwa hiyo mvua ni kitu cha kawaida.
 

Mkuu mimi nilidhani mvua ni lazima iwe ya maji yaani(H02)
 
Ahsante mkuu umenijibu vyema
 
Hivi kifyatu ukiachilia mvua kwenye hizo sayari je kwenye hiyo mars na hizo sayari nyingine kuna waterbodies kwa maana ya bahari, mito na maziwa makubwa.. Na je vipimdi vya majira havijaachana sana na dunia.

Udongo wake unapishana na huu wa kwetu kwa kiwango gani? Uko chini maji yanatoka wapi kwenye hiyo mars.
 
Inaaminika kuwa hapo zamani Mars ilikuwa na hali kama hii hapa kwetu (mito, bahari, nk.). Kwa sababu ya ongezeko kubwa la CO2, joto liliongezeka (greenhouse effect) na maji yalievaporate. Lakini yapo maji aridhini (hasa kwenye poles).

Mars ina vipindi vya majira kama hapa duniani bali kwa sasa hamna mvua. Udongo wake una concentration kubwa ya chuma (iron) na ni mwekundu kama ilivyo sehemu nyingi Tanzania kama vile kwenye milima ya usambara (onga osie shemkunde, kitaa mghoshi?) au nyanda za kaskazini na kusini.
 

Bro huko jupiter kwenye mvua ya Almas sio pakwenda kuish sabab kutakuwa hamna heshima raha ya utajir upatikane kwa watu wachache sasa huko sayar yote ina Almas kutakuwa hamna deal uko labda kwenda kuzizoa na kuja nazo dunian kuuza na kula bata [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] (jokes)
 
Mkuu Kifyatu

Naomba kujuzwa kama kila sayari katika universe yetu ina mchanga (Ardhi) kama huu wetu..

Je nini chanzo cha mchango au ardhi kutokea duniani?
 
Mkuu Kifyatu

Naomba kujuzwa kama kila sayari katika universe yetu ina mchanga (Ardhi) kama huu wetu..

Je nini chanzo cha mchango au ardhi kutokea duniani?
Sayari za Mercury, Venus, Sisi (Earth) na Mars zina miamba na hii baada ya muda hubadilika (weathering) na kuwa vumbi au udongo katika sehemu ya juu. Sayari kubwa kama Jupiter, Saturn, Neptune, Uranus, huwa ujazo wake mkubwa ni hewa na pengine mwamba mdogo katikati. Jupiter ina vumbi jingi sana angani (huonekana kama kimbunga kisichoisha cha rangi ya kahawia). Pengine mwamba wake katikati nao umetengeneza udongo kupitia weathering.

Chanzo cha mchanga au udongo ni mabadiliko ya hali ya hewa yanaopasua hiyo miamba na kuifanya changarawe, mchanga na vumbi, kama ilivyo hapa kwetu duniani.
 
mkuu kifyatu
tunaomba utujuze vzr kuhusu Planet X637Z-43, inasemekana hii sayari imejaa mmea wabangi, km kuna uotoo sikunauwezekano binadam kuishi najee ikoumbali gani katika mfumo wetu wajua
 
Ahsante mkuu kwa kuniongezea maarifa
 
mkuu kifyatu
tunaomba utujuze vzr kuhusu Planet X637Z-43, inasemekana hii sayari imejaa mmea wabangi, km kuna uotoo sikunauwezekano binadam kuishi najee ikoumbali gani katika mfumo wetu wajua
Kutokana na vyanzo vyangu hii habari ya kuwa kumegunduliwa sayari iliyojaa "mmea" si kweli. Ilikuwa ni utani kuwafanya vijana wasiopenda sayansi washtuke kidogo.

Kama ingekuwa kweli basi wengi wangependa kwenda huko.
 
Kifyatu, Hizi blackholes ziko kibao katika hii universe yetu. Blackhole ya galaxy yetu wala sio kubwa kupita zote. Basi kama Mungu anaishi kwenye hizi blackholes, hii yetu itakuwa ni moja ya mitaa yake tu.


Hapo kifyatu, umenena kwakweli dah ubarikiwe.
 
Hapana, chochote kinachoanguka kutoka angani (hasa in liquid form) ni mvua.
Mkuu Kifyatu

Niliwahi kuona na pia kusikia mvua ya mawe (mabonge ya mabarafu) yakianguka kutoka juu hii tuiitaje? Na nini chanzo cha hayo mabonge ya barafu?
 
Mkuu Kifyatu

Niliwahi kuona na pia kusikia mvua ya mawe (mabonge ya mabarafu) yakianguka kutoka juu hii tuiitaje? Na nini chanzo cha hayo mabonge ya barafu?
Hizi mvua za mawe (hail) zinatokea mara nyingi tu kwa mwaka hapa ninapoishi. Anga za juu kunakuwa na baridi zaidi ya hapa chini. Sasa kama mawingu mazito (hasa yanayoambatana na upepo mkali na radi) yakiachilia maji yake (mvua) kwa wingi kwa wakati mmoja basi yale maji yanaganda na kuanguka kama barafu (au mvua ya mawe).
 
Mkuu kifyatu na wengine wote mmetisha sana kwa elimu ya humu ndani..

Mi nina swali moja, kuhusu tafiti za uwezekano wa kuishi sayari ya MARS, maana nilikuwa napitia mahala fulani nikaona kutokana na kuwa mbali na JUA ukifananisha na DUNIA, joto la huko ni kidogo kulinganisha na letu

Licha ya hivo, inapofika usiku joto linashuka sana na kuwa na baridi kali kutokana kutokuwepo kwa trace gases ambazo hufanya kazi ya kutunza joto. Sasa kwa hili haliwezi kuwa kikwazo? Je linaweza kuwa na suluhu?
 
Tukiweza kuijaza Mars na hewa ya Oxygen maisha yanawezekana hata kama kuna baridi. Hapa Duniani Waeskimo wanaishi north pole ambako kumeganda karibuni mwaka mzima.
 
Mkuu Kifyatu kadri unavyojibu maswali hapa ndio unatandia zulia la maswali mengine kwa sisi maamuma!.
Mi naomba kujua hao waeskimo ni kina nani?.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…