baraka bb
JF-Expert Member
- Mar 20, 2016
- 2,691
- 3,884
Asante baraka bb kwa mrejesho. Hujakosea kuhusu mbolea (na nitaelezea) lakini nitakupa alama ya B+ kwa sababu hukuelezea:
Mvua kubwa haisababishwi na radi bali radi husababishwa na mawingu mazito ambayo yanaleta mvua kubwa.
- radi inatoaje mbolea na
- kwa nini radi pekee ndio ilioleta uhai wetu viumbe wote hapa duniani.
Sasa nielezee hizo point mbili za juu:
Radi inatoaje mbolea?
78% ya hewa yetu tunayopumua ni Nitrogen. Hii hewa tunaivuta lakini hatuitumii (nikimaanisha tunaitoa kama tunavyoivuta). Tunatumia Oxygen tu kwa uhai wetu. Unaweza ukafikiria kuwa sasa faida ya hii Nitrogen ni nini?
Mimi na mkuu neo1 tulizungumzia kitu kinachoitwa plasma hapo awali. Wakati wa radi ule umeme na moto mkali wake unatengeneza plasma ya hewa yoyote ile inayoipitia. Lakini hasa hii plasma ya Nitrogen ni muhimu kwa sababu katika hali hiyo, nitrogen plasma ikianguka aridhini na mvua inakuwa rahisi kuchanganyika (react) na madini nyingine aridhini na kutengeneza NITRATES. Ni hizi nitrates ambazo ndio mbolea inayoweza kutumika na mmea kutengeneza chakula chake na kukua. Hewa ya Nitrogen kama ilivyo angani haiwezi kuchanganyika na madini aridhini kutengeneza Nitrates, inahitaji radi kutengeneza plasma ya Nitrogen kwanza.
Kwa nini radi pekee ndio ilioleta uhai wetu viumbe wote hapa duniani?
Ili mmea utengeneze proteins unahitaji Nitrogen ambayo inaipata kama nitrates kutoka aridhini. Bila ya hizi nitrates basi mmea usingeweza kutengeneza proteins, na ungekufa. Wanyama wakila hii mimea wanachukua hizo proteins za mmemea na kutengeneza protein zao. Bila ya hizi proteins za mimea, wanyama (viumbe hai pamoja na sisi binadamu) wa(tu)singekuwepo hapa duniani. Kwa hiyo mkuu baraka bb, kila unapotunisha misuli yako basi uishukuru RADI kwa kuwezesha huwa na hizo proteins zilizojenga mwili wako.
Mars
Mkuu neo1 uliuliza swali kuhusu sayari ya Mars na ni nini cha kufanya ili watu na mimea iwepo (or something like that). Nilikujibu kuwa tunahitaji kupanda miti kwa sababu 96% ya hewa yake ni Carbon Dioxide inayohitajika na miti halafu miti itapumua Oxygen tunayoihitaji sisi watu na wanyama. Lakini nilitoa ilani kuwa hewa ya Mars ina 2-3% Nitrogen. Nikasema hii inaweza kuleta utata kidogo. Nilimaanisha kuwa kama hii asilimia ndogo ya nitrogen itaathiri upatikanaji wa NITRATES za kutosha kupitia radi, nitrogen plasma na mvua. Sijui jibu sahihi la hofu yangu hii.
Ahsante sana kaka mkubwa kifyatu umeeleweka vizur kwa upande wangu
swali iv uko kwenye sayar nyingine kuna mvua maana hapa dunia asilimia kubwa ya upatikanaji wa mvua uletwa na misitu pamoja na bahar vip uko mars au sayar nyingine