Ufahamu kuhusu nyota za angani

Asante, elezea pia kuhusu Galax yetu ni kitu gani?
 
Mkuu nilikuwa na google Leo lakini cha kushangaza naambiwa kutoka duniani mpk Venus ni mbali zaidi kuliko kutoka duniani mpk kwenye jua hii imekaaje
Fikiria watu wawili mnaizunguka nyumba. Kama wewe uko mbele ya nyumba na mwenzio yuko nyuma ya nyumba basi umbali kutoka kwako hadi kwenye nyumba ni mdogo kuliko umbali toka kwako hadi kwa mwenzio.

Sasa hivi Venus iko upande mmoja wa jua na sisi tuko upande mwengine wa jua. Kwa hiyo Venus iko mbali sana kutoka hapa duniani kuliko jua lilivyo.
 
Kuna sayari waliyoigundua miezi michache iliyopita ndani ya mwaka huu wakisema kuna uhai na akajitokeza tajiri mmoja kutengeneza chombo kitakachokuwa na speed ya mwanga ili kufika huko. Hiyo ndiyo iko karibu na solar system?
 
Nimekupata mkuu
 
Kuna sayari waliyoigundua miezi michache iliyopita ndani ya mwaka huu wakisema kuna uhai na akajitokeza tajiri mmoja kutengeneza chombo kitakachokuwa na speed ya mwanga ili kufika huko. Hiyo ndiyo iko karibu na solar system?
Hapana. Hayupo anayeweza kutengeneza chombo kinachoweza kusafiri kwaa spidi ya mwanga. Mwanga unasafiri kilometa laki tatu kwa sekunde moja (300,000km/s), mwendokasi ambao chombo hicho kinaweza kwenda na kurudi kati ya Dar es salaam na Bukoba mara 15 ndani ya sekunde moja tu!
 
Kuna uhai kwenye huu mwezi unaofanana na dunia yetu?
 
Duh mpk nimeogopa hiyo speed yake.
Lakini si kuna kule wamarekani walikituma kwenda Pluto walisema na karibiana kidogo speed na speed ya mwanga hicho kilikuwa kinaenda kilometers ngapi kwa sec?
 
Duh mpk nimeogopa hiyo speed yake.
Lakini si kuna kule wamarekani walikituma kwenda Pluto walisema na karibiana kidogo speed na speed ya mwanga hicho kilikuwa kinaenda kilometers ngapi kwa sec?
Hakijazidi 30,000km/h...........speed ya mwanga hata 10% bado hutajaweza kufikia
 
Mbona hamna cha ajabu hapo,ikumbukwe jua ni nyota ambayo ipo kwenye mzunguuko wa sayari zetu na mojawapo ya hizo sayari ni hio Venus,kwahio yes it is possible .

Jua ndio nyota pekee ilio karibu na sayari zilizo ktk mzunguuko wetu na pamoja na sayari yetu pia earth
 
Mi nilidhani tofauti ya sayari na nyota ni uzalishaji wa energy.
Kwamba nyota inajitegemea na sayari inategemea mwanga kutoka kwenye nyota!!
 
Mi nilidhani tofauti ya sayari na nyota ni uzalishaji wa energy.
Kwamba nyota inajitegemea na sayari inategemea mwanga kutoka kwenye nyota!!
upo sahihi mkuu, nyota inatengeneza energy yake yenyewe lakini sayari hazitengenezi energy zao ili kutoa mwanga ile yote ni reflection kutoka kwenye mwanga wa jua

Mfano sayari ya venus ambayo ina ng'aa sana usiku,mng'ao ule unatokana na anga ya venus kuwa na mawingu mazito yenye asidi ya sulphuric, ile sulphuric asidi ikikutana na gas inatengeneza crystals ambazo ni highly reflective

Kwa hiyo mwanga wa jua ukipiga kwenye venus asilimia 70 una bounce na ndio maana tunaiona venus ina ng'aa sana usiku
 
Unataka kusema kuwa sio sababu ya ukaribu wetu na hiyo sayari ......???
 
Mi nilidhani tofauti ya sayari na nyota ni uzalishaji wa energy.
Kwamba nyota inajitegemea na sayari inategemea mwanga kutoka kwenye nyota!!
Ni sawa ulichosema. Lakini kama mwezi unavyotoa nuru kutoka kwenye jua ndiyo hivyo Venus, Mercury, na sayari zote tuzionazo angani hutoa nuru ya jua inayotua kwenye uso wake.

Ukiangalia kwa makini utaona nyota zote mwanga wake unameremeta (twinkle) lakini sayari mwanga wake haumeremeti.
 
Unataka kusema kuwa sio sababu ya ukaribu wetu na hiyo sayari ......???
Ukaribu unasaidia pia, lakini acidic cloud iliyocover Venus ndio sababu kuu kabisa inayofanya venus iwe na mwanga mkali vile

Mfano mwezi pale ulipo una reflect asilimia 12 tu ya mwanga wa jua ila kwa kuwa mwezi upo karibu zaidi ndio maana una ng'aa sana

Ingekuwa mwezi nao una acidic cloud au una reflect 70% ya mwanga wa jua kama venus, mwezi ungekuwa una ng'aa sana, ila kuwa mwezi hauna atmosphere wala clouds yeyote ile ni miamba tu ndio maana hau reflect mwanga mwingi wa jua

Ila kama venus ingekuwa karibu na dunia kama ilivyo kwa mwezi ingekuwa ina ng'aa sana kama vile mwanga wa mchana ulivyo
 
Nimekusoma,vipi bro we unaamini ipo siku binadamu anaweza kuunda chombo cha kutembea kwa spidi ya mwanga .......???
 
Hivi sayari ya Venus na nyota ya Sirius IPI inangaa sana?
 
Nimekusoma,vipi bro we unaamini ipo siku binadamu anaweza kuunda chombo cha kutembea kwa spidi ya mwanga .......???
speed ya mwanga hatuwezi kufikia close na speed ya mwanga tunaweza tukafikia yaani speed ya 177,000 miles/ second ambapo kwa speed tukisema tukitume chombo kwenye alpha centauri( nyota iliyokaribu na mfumo wetu wa jua itatuchukua miaka 5 tu ila kwa kutumia chemical energy spacecraft itachukua zaidi ya. miaka 50,000 kufika kwenye hiyo nyota

sasa kazi ipo kwenye kutengeneza anti matter space vehicle

Mpaka sasa wanasayansi wameweza kutengeneza anti matter ambayo inafikia uzito wa nanograms 18

zimetengenezwa pale fermilab tevatron particle accerelator ni 15 nanograms,CERN ( 1 nanogram) DESY(Germany) 2 nanograms

Hicho kiwango cha antimatter kilichotengezwa mpaka sasa hivi dunia nzima nishati yake haiwezi hata kuchemsha kikombe cha chai, nanogram ni ndogo sana

1 gram ya anti matter inaweza kutengeneza mlipuko kama wa nuclear bomb
Kutengeneza gram 1 ya anti matter inahitajika 25 million billion kilowatt of energy na ina cost million billion dollars
Labda descendants wetu miaka ijayo wataweza kutengeneza anti matter

anti matter ikikutana na matter ya kawaida inatengeneza kiasi kikubwa cha energy, cosmic rays wanasayansi wanasema zina anti matter

Prolpusion system nyingine ambayo inaweza kufikia speed ya light ni warp drive ila bado sijaijua vizuri na bado ni science fiction kizazi hiki hatauweza kutengeneza

Labda mkuu kifyatu aje atuelezee wrap drive kama anaijua kiundani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…