Sikua nimeliona hili swali lako la jana.
Kuhusu aliens hata mimi nina shauku sana kujua ukweli uko wapi. Wacha hatua tulizopiga kitaaluma tangu 1950 lakini ukiangalia maajabu kama ya pyramids na accuracy ya ujenzi wake, technolojia za waMayans, Einstein alikuwa anaota nini mpaka kutuletea mahesabu yake ya relativity, nk. Utaona mara kwa mara kunakuwa na mlipuko wa elimu mpya inayotokea na inayotusogeza mbele kitaaluma na sijui ni kwa nini.
Mkuu inawezekana hata wewe na shauku zako za kujua mambo inawezekana unakamkono ka hawa aliens (jokes).
Mimi niko open kabisa kujuzwa kuhusu hawa eliens.
- Pengine ni malaika?
- Au ndio mkono wa Mungu mwenyewe?
- Hivi ni kweli katika universe yote hii hakuna viumbe wenye kufikiri na maarifa kama au zaidi ya sisi?
- Pengine aliens tunao lakini hatuwaoni (sio carbon-based kama sisi)?
- Inawezekana kuwa wanatubadilisha (wanatuumba) kwa kutufanyia genetic-mutations (kama jua letu linavyotufanyia) badala ya genetic cross-overs (yaani kuzaa na sisi) kama tunavyozaana?
Maswali ni mengi mkuu. Kuna mengi hatuyajui na ndio maana sipuuzii dhana yoyote ile nitakayoisikia.