Ufahamu kuhusu nyota za angani


Navyojua Satellites zinatembea lakini sina uhakika zaidi....wajuzi wanaweza kutusaidia zaidi
 
Ukichunguza utakuta Huyu ni mwalimu anayefundisha taifa la kesho.
Kuna tofauti Kati ya sayansi ya Shule ya msingi, secondary Hata vyuoni na exploration, Nivea umekariri sayansi ya Shule ya msingi. Pole sana
 
Mkuu unaweza ukanifafanulia kuhusu Virgo?
VIRGO ni mkusanyiko wa nyota (constellation) unaofananishwa na mwanamwali alieshika mashuke ya ngano na wanajimu wa zamani. Hii ndio sababu ya huu mkusanyiko pia huitwa MASHUKE na wanajimu wa kiswahili.

Lakini pia Virgo ni mkusanyiko wa nyota katika njia ya jua linayopita (au tunapoliona) wakati dunia inalizunguuka jua. Hii njia ya jua inajulikana kama "ECLIPTIC". Jua linakuwepo kwenye huu mkusanyiko (constellation) kuanzia August 23 hadi September 22. Kuna jumla ya mikusanyiko 12 katika hii njia ya jua na Virgo ni mmojawapo kati ya hiyo 12.
 
Madhumuni ya vyombo hivyo ni nini? Vimeenda kutafiti nini? Vimelenga kwenda sehemu moja au vinazunguka tu kupiga picha?
 
Mkuu hapa umeeleza mambo makubwa sana mawili, hilo la radio signal sijalielewa na huo muda wa hizo signal mbona sijaelewa? Hiyo signal madhumuni yake ni nini? Na hao Aliens uliowataja wanategemewa wapatikane wapi ili wakione chombo hicho?
 
Madhumuni ya vyombo hivyo ni nini? Vimeenda kutafiti nini? Vimelenga kwenda sehemu moja au vinazunguka tu kupiga picha?
Vimelenga kuuchunguza ulimwengu, binadamu kama binadamu ni muhimu kujua mazingira yanayotuzunguka
 
Mkuu hapa umeeleza mambo makubwa sana mawili, hilo la radio signal sijalielewa na huo muda wa hizo signal mbona sijaelewa? Hiyo signal madhumuni yake ni nini? Na hao Aliens uliowataja wanategemewa wapatikane wapi ili wakione chombo hicho?
Yani ni hivi wanaanga katika uchunguzi wao waliona kuna sayari inaweza kuwa na uhai ndani yake, yani kuna viumbe wanaishi sasa kwa kuwa sayari iko mbali sana na kuifikia kwa technology tuliyonayo sasa haita wezekana sababu sayari ipo umbali wa miaka 25,000 ya mwanga

yani kama ukituma chombo chenye speed sawa na ya mwanga itachukua miaka 25,000 kufika kwenye hiyo sayari

wanaanga hao wakatuma radio signal kwenda kwenye hiyo sayari ili kama kuna viumbe wapate hizo signal na wajue kwamba kuna viumbe wengine sehemu fulani

Mfano labda hapa duniani itokee siku tupate signal kutoka anga za mbali kabisa, lazima tutajua kama kuna viumbe wengine wapo mahali fulani ndio wanatuma hizo signals ili tufahamiane lakini mpaka sasa hicho kitu hakijawahi kutokea, zaidi zaidi huwa tunapokea signals ambazo ziliachwa na mlipuko wa bing bang signal za bing bang zinapatikana kwenye TV za zamani zile hasa za chogo unapo washa zile chenga za makelele za mwanzo
 
Popote pale chombo kitapo angukia baada ya mwaka 2025

Kama kitangukia kwenye sayari yenye aliens kama wapo basi itakuwa ni mwanzo wa sisi na wao kutafutana na kujuana, maana zile Voyager zina details zote kuhusu ikiwapo mfumo wa DNA yetu na pia location yetu pia

Kama watapata hizo details itakuwa rahisi wao kututafuta sisi kama nao wana technology kubwa

ila zote hizi ni nadharia tu, wameweka hivyo kama hayo mambo yatatokea kweli, hii ni sawa sawa na kufanya lakini huna uhakika nalo wala hujui nini kitatokea wameweka kama tahadhari

vyombo vingi vya anga huwa vina purpose nyingi vingi huwa vinaenda kuchunguza sayari mfano new horizon, Juno nk na vikimaliza mission zao huwa zinaenda anga za mbali mfano kama ilivyotokea kwa voyager mission ya msingi ilikua ni kuchunguza Jupiter lakini baada ya mission kuisha chombo kikaendelea na safari zake kwenye anga za mbali na kutoka kabisa kwenye mfumo wa jua na huko kinatuma taarifa mara kwa mara kwa kinachoyaona
 
Mkuu Kifyatu kwa hapa umeniacha kabisa, hilo la kutozeeka sijakuelewa naomba ufafanuzi wa kina.
Vilevile post namba 223 hujaijibu naomba uijubu.
 
Mkuu hili ndilo somo gumu zaidi kulielewa tangu nianze kujifunza physics na mathematics. Yaani sijui utanieleweshaje nielewe. Yaani chombo kiundwe kitakachotumia speed ya mwanga na kuweza kusafiri kwa kwa dakika 5, umbali ambao ningesafiri kwa miaka 30 kama ningetumia kifaa cha kawaida. Then baada ya dakika tano kuisha nikirudi nikute miaka 30 imepita? Inawezekana kweli?
 

hapo hata me sikuwahi kuelewa na akileta jibu hapa la kueleweka nakutumia elfu5 Mkuu
 
Hivi katika ulimwengu kuna majini mapepo na mizimu, tunaviweka kwenye kundi gani hivi viumbe? Kuna tofauti gani na hao Aliens?
 
Mkuu jua ndio nyota kubwa kuliko zote. So a sun is a star too
Msaada zaidi: just google ''Sun"
Kuna nyota ni kubwa kuliko jua letu....ili tusichanganye watu. Our sun is also a star ikiwa na maana kama tutakuwa umbali wa zaidi ya 1 light year... basi jua letu litaonekana dogo sana kama tuonavyo nyota za mbali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…