Ufahamu kuhusu nyota za angani

Ufahamu kuhusu nyota za angani

Napoangaliaga angani wakati wa usiku huwa naona nyota zingine ambazo hazina mwanga wa rangi moja,yan inabadilika badilika mara nyekundu,kijan,bluu.
Je hizi nyota ni za aina gani? mana kuna mtu katika stori za utoto alinambia eti zile ni satelaiti
Pia nyota chanzo chake cha mwanga ni kipi?
Karibuni wadau wa Sayansi ya anga
Thanks mkuu.
 
Ni kweli jua ndiyo nyota kubwa kuliko zote kwenye mfumo wetu wa jua (solar system) ambao una sayari 9 tu. Nyota unazoziona zinang'aa ziko mbali mno, wala haziko kwenye mfumo wetu huu wa kwetu, yaani ziko nje ya solar sytem. Jirani ya mfumo wetu, yaani jirani yetu aliye karibu sana na mfumo wetu wa jua (hayuko kwenye mfumo wetu) ni nyota inayoitwa alpha centauri, ambaye yuko umbali wa unaokadiriwa kuwa 4.4 light years kutoka hapa kwenye mfumo wetu wa jua, kwa maana kwamba umbali huo, ni umbali ambao ukiwa na ndege au chombo kingine chochote kile chenye uwezo wa kutembea kwa kasi ya km laki3 kwa sekunde moja (300,000km per second), au sawa na roundtrip zaidi ya 10 za kutoka Dar kwenda Mwanza (na kurudi), au zaidi ya 20 za Dar Mwanza, kwa sekunde moja tu, kinaweza kuchukua muda wa miaka 4.4 kufika kwa jirani yetu nyota ya alpha centauri ambaye ndiyo jirani aliye karibu zaidi na sisi. Mbali na hayo, jirani yetu kwenye galaxy yetu, yaani galaxy ambayo iko karibu sana na sisi kwenye universe inaitwa andromeda na iko umbali unaokadiriwa kufikia 2,000,000 light years (miaka-mwanga millioni mbili). Hii ndiyo galaxy iliyo karibu sana na sisi, hakuna nyingine ambayo ni jirani na sisi kuzidi hii. Hata hivyo, the entire universe ambayo ina millions of galaxies, inasemekana kwamba inatanuka kwa kiwango cha mara 300 trillion trillion kwa sekunde moja,..., jaribu ku-imagine hii scenerio, yaani possibly naweza kufananisha na kitu kilicho kidogo size ya mchanga kiwe kinatanuka na kuwa size ya tuseme, Tanzania nzima (mfano) kwa sekunde moja, halafu mtindo huo huo ndiyo uendelee kwa kutanuka namna hiyo kila umbile linalopatikana kila baada ya sekunde moja, you can imagine how incomprehensible the size of the universe is. Unaona maajabu haya ya ulimwengu huu tunaoishi? Who's behind all these mystical, miraculous and adventurous actions and creations? Are they really by coincidencial, randomly unorganised forces only? Really no thanks!
Ndugu yangu kusema ukweli mimi kuna kipindi nilikuwa naamini kuwa Mungu yupo, sasa hivi siamini tu ila pia nimeshahakikisha kwa evidence ambazo siwezi kuziprove kwa mtu mwingine, na hivyo nakusihi wewe uamini kuwa Mungu yupo and there is a day utahakikisha kama mimi nilivyohakikisha. You believe by hearing, you prove by seeing or experiencing. Kitu kikishakuwa knowledge maana yake kimeshadevelop beyond faith level!

I would like to update this 2007 post of mine as follows:

At present, the closet known galaxy to the Milky Way is the Canis Major Dwarf Galaxy, a.k.a the Canis Major Overdensity. This stellar formation is about 42,000 light years from the galactic center, and a mere 25,000 light years from our Solar System
However, our nearest neighbour Spiral galaxy remains to be the Andomeda galaxy,positioned at a distance of about 2.537 million light years from our own galaxy
 
Malizia story yako....kuna kitu inaitwa nyota ya jaa/Jah...yenye bahati. Ukiamka usiku iko tofauti na nyingine, ukiigundua basi inasemekana chochote utakachoomba utakipata interms of wealth.
... Nyota ya Jaha ni Haley Comet ambayo hupita duniani kila baada ya miaka 75, kama sijakosea sana, kwa hiyo kuonekana kwake ni vigumu sana maana hutumia kama siku Saba tu kukatisha Anga la dunia kwa maana hiyo ikipita kama una miaka 20 kwenda juu ni vigumu sana kuja kuiona tena katika Uhai wako!
Mara ya mwisho kupita hapa duniani ilikuwa ni mwaka 1986 na inatazamiwa kupita tena anga la dunia yetu hii miaka AROBAINI ijayo!!!
Unaweza ukapata picha ya ukubwa wa dunia ukifikiria tu kwamba toka ilipokatisha eneo hili la anga ya dunia miaka THELATHINI iliyopita nyota hii inaendelea kupuyanga kwa kasi ya kutisha, na itaendelea kufanya hivyo kwa miaka AROBAINI ijayo, katika hapo nyota hiyo ambayo njia yake sio ya mviringo kuinzunguka dunia bali ipo parable kama yai...itafika mwisho wa parable yake na kupinda kona kurejea duniani ambapi itapita karibu nasi usawa wa nyota nyingine miaka AROBAINI ijayo!!
Nilibahatisha kuiona mwaka 1986 nikiwa pale nyumbani Tanga kwa wiki nzima wakati ikikatisha duniani. Nikiwa na miaka 27, kwa maana hiyo sitegemei kuiona tena wakati ikikatisha tena anga hili mwaka 2056..miaka 75 baadaye, japo miaka 36 imeishapita na imebaki miaka kama 40 hivi...!!! Hiyo nyota ya Jaha, Haley's Comet. Una nafasi moja tu ya kuiona katika maisha yako yote!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Imethibitika kisayansi kuwa ukisafiri kwa kasi kubwa basi aging process yako inazoroto. Na ukisafiri kwa kasi ya mwanga basi ukuaji wako unasimama kabisa .

Kwa hiyo ukisafiri masafa marefu ambayo yangekuchukua miaka 30 kwa kutumia dakika 5, wewe ndie utakaeona umetumia dakika 5 lakini sisi uliotuacha hapa tutaona umekwenda kwa miaka 30. Ukirudi, umri wako utakuwa umeongezeka kwa dakika 5 wakati sisi hapa duniani umri wetu utakuwa umeongezeka kwa miaka 30. Hii ndio maana ya traveling into the future.
hapa narecomend series ya manifest ... Wadau wazidi kuelewa zaidi kuhusu Time Travel ....
 
Habari wakuu, kwa idhini yenu naomba kuufufua uzi huu lakini naona huzuni nikicheki last seen ya mkuu Kifyatu na pia neo1 zinaashiria kukosekana muda mrefu hapa jukwaani.

yonga @

vinginevyo tungejadili mengi kwa uzuri zaidi na ziada ya elimu.
 
Black holes hutokea pale nyota inapofikia mwisho wa maisha yake na kufa, hiyo nyota hugandamizwa na kupungua size kwa kuwa na umbo dogo hivyo kuwa na nguvu ya uvutano (gravity) kubwa zaidi.

Baada ya black hole kutengenezwa huanza kuvuta na kumeza vitu vilivyo karibu yake mfano huweza kuungana na black holes nyingine, humeza nyota nyingine hivyo kuzidi kukua na kupngezeka ukubwa.

Kutokana na ukubwa wa uwezo wake wa nguvu ya kuvuta vitu, hakuna kitu chochote kinachoweza kupenya ukiwemo mwanga. Mwanga unapoingia kwenye black hole hauwezi kupenya au kuwa reflected kutokana na nguvu ya uvutano iliyopo ndani hivyo basi kila kiingiacho hakiwezi kutoka.
Je black hole inapomeza nyota humeza na sayari zake zote zingukayo hiyo nyota?
 
Yeah is the biggest star, and it produce its own light and heat.. sema sasa jua halisogea (halifanyi movement) lakini nyota zingine zinatembea angani pamoja na vimondo(comets)
Mitaala ibadilishwe tu!!
 
Ivi kumbe wale waliochora Solar sytem na kutuambia jua ni biggest atom wametudanganya!
Kwanza toa neno atom hapo halihusiki kabisa na halimaanishi chochote kwenye mada unayoizungumzia, pili once ukisema solar system maana yake mfumo wa jua(solar=jua) hivo jua ndilo kubwa kuliko sayari ambalo ndizo zinalizunguka jua(star) lakini unapaswa kujua kuwa kuna mifumo ya jua mingi sana yaani billions of solar systems in the universe hivo kuna majua makubwa kuliko hili letu. Sijua kama umeelewa hii concept.
 
Malizia story yako....kuna kitu inaitwa nyota ya jaa/Jah...yenye bahati. Ukiamka usiku iko tofauti na nyingine, ukiigundua basi inasemekana chochote utakachoomba utakipata interms of wealth.
Leo nitaamka usiku lazima...iwe kweli au si kweli
 
kwahiyo sisi tupo ndani ya nyota dunia??????
hapa sayansi imeongopa
mbna jua lipo mbali kabisa mkuuuuuuu
Wanaposema dunia ipo ndani ya nyota(jua) maana yake ipo kwenye mfumo wa hiyo nyota(jua) kwa lugha ya kigeni wanasema solar system, epuka kutumia neno uongo kwenye mambo ambayo huyaelewi ama umeelekezwa lakini umeshindwa kuelewa.
 
Jamani samahani ndugu zangu wote Mimi mkristo ila na soma sana Quran kujifunza mambo, katika Quran MUNGU MKUU anasema kuna mbingu saba ambazo ameziumba na anasema mbingu ya kwanza ambayo niyakwetu ndio aliyoipamba sana kwa nyote ili hali hizo mbingu sita azijapambwa kama hiii, na Ulikuwa maalumu kwa ajili yetu, pia Mola anasema anaendelea kuujenga kila Siku ulimwengu, kumbuka haya yamezungumzwa kwenye Quran Tukufu ata kabla sayansi ya juu kutambulika je Ina maana tunaposema kuna nyote katika galaxy nyingine tunapingana na MUNGU MKUU!?
Kwanza kabisa unatakiwa kujua nini maaa ya mbingu
 
Jamani samahani ndugu zangu wote Mimi mkristo ila na soma sana Quran kujifunza mambo, katika Quran MUNGU MKUU anasema kuna mbingu saba ambazo ameziumba na anasema mbingu ya kwanza ambayo niyakwetu ndio aliyoipamba sana kwa nyote ili hali hizo mbingu sita azijapambwa kama hiii, na Ulikuwa maalumu kwa ajili yetu, pia Mola anasema anaendelea kuujenga kila Siku ulimwengu, kumbuka haya yamezungumzwa kwenye Quran Tukufu ata kabla sayansi ya juu kutambulika je Ina maana tunaposema kuna nyote katika galaxy nyingine tunapingana na MUNGU MKUU!?
What if Mbingu=universe, hapo vipi? Je umejaribu kufikiri hivi?
 
NYOTA ni kama jua lakini ziko mbali sana na dunia kushinda jua.NYOta ni kubwa kushinda jua.
Umenena vyema dunia inaingia mara milioni moja kwa jua na nyota ni kubwa kuliko jua imagine huo kubwa na inasemekana zinatoa joto ndio maana jua wanasema ni nyota linashare features na nyota nyingine
 
Haya, BISMILLAH.

Nyota ni nini?
Nyota ni kama jua letu, lakini ziko mbali sana.

Nyota ziko mbali kiasi gani?
Mwanga unasafiri kwa kasi (speed) ya 299,793 km/sekunde au 1,079 milioni km/saa. Mara nyingi umbali wa nyota hupimwa kwa muda utakaotumiwa na mwanga kusafiri mpaka kutufikia sisi. Kwa mfano, mwanga kutoka jua letu unasafiri kwa takriban dakika 8 hivi kutufikia sisi (au, jua liko umbali wa 8 light-minutes kutoka hapa duniani). Nyota iliyo karibu sana na sisi ni ile iitwayo alpha-Centauri (kwenye constellation ya Centaurus) ambayo iko umbali wa 4.4 light-years kutoka hapa (mwanga kutoka alpha-centauri huchukua miaka 4.4 kutufikia) ndio maana nyota zinaonekana ndogo sana ukifananisha na nyota yetu (jua) hapa duniani. Jua letu ni moja ya nyota ndogo sana. Kuna mizinga ya nyota kama Betelgeuse (kwenye Constellation ya Orion) ambayo ina ukubwa wa majua yetu 1,000 na iko umbali wa 643 light-years kutoka hapa.

Chanzo cha mwanga wa nyota.
Nyota zote (pamoja na jua letu) zinatoa mwanga, joto, na nishati nyingine kutokana na nguvu za nyuklia aina ya fusion. Fusion inachukua atom mbili za hewa ya hydrogen na kuziunganisha ili kutengeneza atom moja ya hewa ya Helium. Uzito wa zile atom mbili za hydrogen ni mkubwa kuliko uzito wa atom ya helium iliyotengenezwa. Hii tofauti ya uzito "m" haipotei bali hubadilika kuwa nishati (E) kufuatia kanuni ya mkulu Albert Einstein kuwa E=mC2. Hii C ni ile kasi (speed) ya mwanga tuliyozungumzia hapo juu.

(Nguvu za nyuklia pia zinaweza kupatikana kwa kupasua (Fission) atom nzito kama za Urani (Uranium). Njia hii inatumika kwenye mitambo ya nyuklia inayozalisha umeme, mabomu, nk. Njia hii ya fission ni less efficient kuliko ile inayotokea kwenye jua kupitia fusion.)

Kwa kuwa nyota zote zina ujazo mkubwa sana wa hewa ya hydrogen, inachukua mabilioni ya miaka kuimaliza hii hydrogen. Kwa hiyo usiwe na wasiwasi, jua letu litaendelea kuwaka kwa mabilioni mengine ya miaka.

Rangi ya nyota nyingine kubadilika badilika (Nyekundu/bluu)
Nyota nyingi ziko moja moja, kama jua letu. Lakini kuna nyota nyingine zinakuwa pacha (mbili karibu karibu au Binary-stars). Zikiwa hivi basi zina-spin. Sisi hapa duniani tukiziangalia tunachoona ni matokeo ya hii spin (naomba mtu anisaidie maana ya spin).

Wakati moja ya hizi nyota ikiwa inakuja kwetu mwanga wake unaonekana kama una wave-length fupi (wave-length ya rangi ya bluu.) Ile nyota inayo tukimbia mwanga wake unaonekana kama una wave-length ndefu (wave-length ya rangi nyekundu). Hali hii inafanya tuone nyota ina-twinkle na rangi mbili, nyekundu na bluu. Hii inajulikana kama Doppler-effect iliyogunduliwa na mwanasayansi Christian Doppler mwaka 1842 alipowasilisha mada yake kwenye kongamano huko Prague kuhusu hizi binary-stars na rangi zake (alikuwa ni Astro-Physicist Kutoka Austria).

Nawasilisha.

I am sorry if this is an overkill.
Thank u !
 
Back
Top Bottom