Sawa mkuu nitakujibu kuhusu Pleiades (Subaru au KILIMIA kwa kiswahili). Unajua kuna imani kuwa aliens wa kwanza waliokuja hapa duniani (na kuchanganya DNA zao ili kutupata sisi binaadam wa kileo) na kujenga pyramids, Mayan technology na vinginevyo wametoka katika sayari liliyopo katika moja ya nyota za Pleiades?
Kwa nini mkuu una shauku ya kujua zaidi kuhusu Pleiades au Kilimia?
Kuna imani pia kuwa hawa aliens kutoka Pleiades bado tunao hapa duniani bali wanachagua wakati gani waonekane na wakati gani wasionekane. Hii sio sayansi (haijathibitishwa kisayansi) bali ni dhana tu ya wale wanaoamini kuwa kuna aliens.